5. Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:

Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima kwanza umpe Yeye moyo wako, na kuutuliza moyo wako mbele za Mungu. Ni baada tu ya kuumimina moyo wako mzima kwa Mungu ndipo unaweza kuingia hatua kwa hatua katika maisha ya kiroho yanayostahili. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Roho Mtakatifu leo ni nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu, na kuendelea kwa Roho Mtakatifu kumpa nuru mwanadamu wakati wa kipindi hiki ni mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu. Na mwelekeo ni upi katika kazi ya Roho Mtakatifu leo? Ni uongozi wa watu ndani ya kazi ya Mungu leo, na ndani ya maisha ya kiroho ya kawaida. …

Kwanza, lazima uumimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu. Lazima usiyafuatilie maneno ya Mungu katika siku za zamani, na lazima usiyasome wala kuyafananisha na maneno ya sasa. Badala yake, lazima uumimine moyo wako kabisa katika maneno ya sasa ya Mungu. Kama kuna watu ambao bado wangependa kuyasoma maneno ya Mungu, vitabu vya kiroho, au maelezo mengine ya mahubiri kutoka kwa siku za zamani, ambao hawafuati maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi wao ni wapumbavu zaidi ya watu wote; Mungu huchukia sana watu kama hao. Kama uko radhi kukubali nuru ya Roho Mtakatifu leo, basi mimina moyo wako kabisa katika matamshi ya Mungu leo. Hili ni jambo la kwanza ambalo lazima utimize.

Kimetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika kumwamini Mungu, angalau lazima utatue suala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi maana ya imani yako katika Mungu imepotea. Kuanzishwa kwa uhusiano wa kawaida na Mungu kunaweza kufikiwa kabisa kwa moyo ulio kimya katika uwepo wa Mungu. Kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu kunamaanisha kuweza kutokuwa na shaka na kutoikana kazi yoyote Yake na kuweza kuitii kazi Yake. Kunamaanisha kuwa na nia zisizo na makosa katika uwepo wa Mungu, kutofanya mipango kwa ajili yako mwenyewe, na kuzingatia masilahi ya familia ya Mungu kwanza katika mambo yote; kunamaanisha kukubali uchunguzi wa Mungu na kuitii mipango ya Mungu. Lazima uweze kuutuliza moyo wako katika uwepo wa Mungu katika yote ufanyayo. Hata kama huyaelewi mapenzi ya Mungu, bado unapaswa kutekeleza wajibu na majukumu yako kadiri uwezavyo. Mara tu mapenzi ya Mungu yanapofichuliwa kwako, lichukulie hatua, na hutakuwa umechelewa mno. Wakati ambapo uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa kwa msingi wa maneno ya Mungu. Kula na unywe maneno ya Mungu, kisha uyatie matakwa ya Mungu katika vitendo, rekebisha maoni yako, na uepuke kufanya chochote ili kumpinga Mungu au kulivuruga kanisa. Usifanye chochote ambacho hakifaidi maisha ya ndugu zako, usiseme chochote kisichowasidia wengine, na usifanye jambo lolote la aibu. Kuwa mwenye haki na mwenye heshima katika jambo unalotenda na uhakikishe kuwa kila kitendo chako kinapendeza mbele za Mungu. Ingawa wakati mwingine mwili unaweza kuwa dhaifu, lazima uweze kuweka masilahi ya familia ya Mungu kwanza, bila tamaa ya kupata faida ya kibinafsi, na lazima uweze kutenda kwa haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa namna hii, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Katika kila jambo unalofanya, sharti uchunguze ikiwa nia zako hazina makosa. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa. Chunguza nia zako, na ukiona kwamba nia mbaya zimejitokeza, uweze kuziacha na kutenda kulingana na maneno ya Mungu; hivyo utakuwa mtu aliye sawa mbele za Mungu, ambayo inaonyesha kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba yote unayoyafanya ni kwa ajili ya Mungu, si kwa ajili yako. Katika yote unayofanya na yote unayosema, uweze kuuweka moyo wako uwe sawa na uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, wala kutenda kulingana na mapenzi yako mwenyewe. Hizi ni kanuni ambazowaumini katika Mungu wanapaswa kutenda. Mambo madogo yanaweza kufichua nia na kimo cha mtu, na kwa hivyo, ili mtu aweze kuingia kwenye njia ya kukamilishwa na Mungu, lazima kwanza arekebishe nia zake na uhusiano wake na Mungu. Ni wakati tu uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida ndipo unaweza kukamilishwa na Yeye; ni wakati huo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, ufundishaji nidhamu, na usafishaji wa Mungu vifanikisha athari zake zilizokusudiwa ndani yako. Hiyo ni kusema, ikiwa wanadamu wanaweza kumweka Mungu mioyoni mwao na wasifuatilie faida ya kibinafsi au kufikiria matarajio yao wenyewe (kwa njia ya mwili), lakini badala yake wabebe mzigo wa kuingia katika uzima, wajitahidi kabisa kuufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu—ikiwa unaweza kufanya hivi, basi malengo unayoyafuatilia yatakuwa sawa, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Kimetoholewa kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Tunapoanzisha uhusiano wa kufaa na Mungu, tunapaswa kuanzia wapi? Jambo muhimu zaidi ni kuzungumza kutoka moyoni wakati wa kuomba kwa Mungu. Kwa mfano, unasema katika sala, “Ee Mungu, naona kwamba ndugu zangu wengi wanaweza kujitolea nafsi zao zote ili kujitumia kwa ajili Yako, lakini kimo changu ni kidogo sana. Nafikiria riziki yangu na mustakabali wangu, na pia iwapo nitaweza kuvumilia taabu ya mwili. Siwezi kuyaacha mambo hayo. Kweli nina deni Lako. Wanawezaje kuwa na kimo kama hicho? Usuli wa familia zetu ni sawa, lakini wanaweza kujitumia kwa ajili Yako wakati wote—mbona siwezi? Nakosa ukweli mwingi sana. Daima nafikiri juu ya matatizo ya mwili; imani yangu ni ndogo sana. Ee Mungu, naomba Unipe nuru na mwangaza, Ukiniruhusu kuwa na imani ya kweli Kwako na kujitumia kikamili kwa ajili Yako punde kabisa.” Huku ni kuzungumza kutoka moyoni. Ikiwa una aina hii ya mawasiliano ya dhati na Mungu kila siku, Ataona kwamba wewe ni mwaminifu, kwamba humfanyii vitu kwa namna isiyo ya dhati tu, kumpa maneno matamu Yeye au kumuunga mkono kwa maneno matupu tu. Kisha Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake. Huu ndio mwanzo wa kuanzisha uhusiano ufaao na Mungu. Sisi ni viumbe walioumbwa, na Yeye ni Muumba. Sisi viumbe tulioumbwa tunapaswa kuwa na nini mbele ya Muumba wetu? Utiifu, ridhaa, imani na ibada ya kweli. Lazima tutoe mioyo yetu kwa Mungu kikamilifu; lazima tumwache aongoze, kutawala na kupanga. Kwa kuomba na kutafuta kwa njia hii, uhusiano wetu na Mungu utakuwa wa kufaa.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Kuna kanuni kadhaa za kuanzisha uhusiano wa kufaa na Mungu. Ya kwanza ni kwamba lazima uamini katika uweza na hekima Yake, na lazima uamini kwamba maneno yote ya Mungu yatatimizwa. Huu ndio msingi. Ikiwa huamini kwamba maneno ya Mungu hakika yatatimizwa au kuamini katika uweza wa Mungu, basi huna imani ya kweli. Pili, lazima utoe moyo wako kwa Mungu na kumwacha Mungu kuamua katika mambo yote. Tatu, lazima ukubali uchunguzi wa Mungu, na hili ni muhimu. Usipokubali uchunguzi wa Mungu wa maombi na ushirika wako, matendo yako na maneno yako, utawezaje kuwa na ushirika wa kweli na Mungu? Utaweza kumwambia kile kilicho moyoni mwako? Unapozungumza, unaomba tu kwa ajili yako; lina nia mbaya, na limejaa maneno matupu, majisifu na uongo. Usipokubali uchunguzi wa Mungu, utawezaje kutambua mambo hayo? Punde utakapokubali uchunguzi wa Mungu, wakati umesema kitu kibaya, kuzungumza maneno matupu, au kutoa viapo vya kawaida, utatambua mara moja, “Je, sijaribu kumdanganya Mungu? Mbona hili linahisi kama kumdanganya Mungu?” Huku ni kukubali uchunguzi wa Mungu, na hii ndiyo maana ni muhimu sana. Nne, lazima ujifunze kutafuta ukweli katika mambo yote. Usitegemee falsafa ya Shetani; usitegemeze vitu kwa iwapo utafaidika au la. Lazima utafute ukweli na kutenda kulingana na ukweli. Bila kujali faida au hasara yoyote ya binafsi, lazima utende ukweli na kusema ukweli, na pia kuwa mtu mwaminifu. Kupitia hasara ni aina ya baraka; utabarikiwa zaidi na Mungu unapopitia hasara. Ibrahimu alipitia hasara nyingi, na daima aliafikiana katika kuingiliana kwake na wengine. Hata watumishi wake walilalamika, “Kwa nini wewe ni dhaifu sana? Acha tupigane nao!” Ibrahimu alikuwa akifikiri nini wakati huo? “Hatupigani nao. Kila kitu kiko mikononi mwa Mungu, na ni sawa kupitia hasara kiasi.” Kama matokeo, Mungu alimbariki Ibrahimu hata zaidi. Ikiwa faida zako binafsi zimetiwa hatarini kwa sababu ya kutenda kwako ukweli na humlaumu Mungu, basi Mungu atakubariki. Tano, lazima ujifunze kutii ukweli katika mambo yote; hili pia ni muhimu. Bila kujali ni nani anayesema kitu kinachokubaliana na ukweli, bila kujali iwapo ana uhusiano mzuri na sisi au la, na bila kujali jinsi tunavyohisi kumhusu, alimradi kile anachosema kinakubaliana na ukweli, tunapaswa kukitii na kukikubali. Hili linaonyesha nini? Kuwa na moyo wa uchaji kwa Mungu. Ikiwa mtu anaweza hata kumtii mtoto wa miaka tatu ambaye maneno yake yanakubaliana na ukweli, je, mtu huyu bado ana majivuno yoyote? Bado yeye ni mtu mwenye majivuno? Tabia yake imebadilishwa. … Sita, kuwa mwaminifu kwa Mungu katika kutimiza wajibu wako. Huwezi kamwe kusahau kutimiza wajibu wako kama kiumbe aliyeumbwa—usipofanya hivyo, hutawahi kamwe kumridhisha Mungu. Yeyote asiyetimiza wajibu wake ni takataka na ni wa Shetani. Kama unaweza kutimiza wajibu wako mbele ya Mungu basi wewe ni mmoja wa watu wa Mungu—hii ndiyo alama. Ukitimiza wajibu wako vizuri, wewe ni kumbe ambaye amefikia kiwango kilichowekwa; ukikosa kutimiza wajibu wako, basi hujafikia kiwango kilichowekwa na hutapata idhini ya Mungu. Kwa hiyo, ikiwa unaweza kuwa mwaminifu kwa Mungu katika kutimiza wajibu wako na kisha uwasiliane na Mungu, Atakosa kukubariki? Atakosa kuwa nawe? Saba, simama upande wa Mungu katika mambo yote; kuwa wa moyo na akili moja na Mungu. Wazazi wako wakisema chochote kisichokubaliana na ukweli, kinamchopinga na kumwasi Mungu, basi unapaswa kuweza kusimama na Mungu na kubishana nao, kuwakana, na kukataa kukubali kile wanachosema. Je, huku si kuwa na ushuhuda? Je, hili linaweza kumwaibisha Shetani? (Ndiyo, linaweza.) … Ikiwa watu wanaweza kutii kanuni hizi saba, wanaweza kupata idhini ya Mungu, na kisha uhusiano wao na Mungu utakuwa wa kufaa kabisa. Hizi kanuni saba ni muhimu sana!

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Iliyotangulia: 4. Inamaanisha nini kuomba kwa kweli?

Inayofuata: 6. Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Sababu ya Bwana Yesu kuwalaani Mafarisayo, na ni nini kiini cha Mafarisayo

Kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.

1. Makusudi ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki