Swali la 39: Kwa miaka elfu mbili, dunia nzima ya kidini imeamini kwamba Mungu ni Utatu, na Utatu ni nadharia bora zaidi ya mafundisho yote ya Kikristo. Hivyo, tafsiri ya “Utatu” inashikilia kweli? Utatu una uwepo kweli? Kwa nini unasema kwamba Utatu ni uwongo mkuu mno wa ulimwengu wa kidini?

Jibu:

Nyote mnategemeza uthibitisho wenu kwamba Bwana Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu kwa kile kilichorekodiwa katika Biblia, na kisha mnapomwona Bwana Yesu akimwomba Mungu Baba, hili linadhibitisha zaidi kwenu kwamba Bwana Yesu na Mungu wana uhusiano wa Baba na Mwana. Ongezea kwa hilo ushuhuda wa Roho Mtakatifu na ushuhuda na uwekeaji mipaka wa mitume, na basi mna hakika kwamba Mungu ni Utatu. Kwa miaka elfu mbili, dunia ya dini imekuwa na hakika kwamba Mungu mmoja wa kweli aliyeziumba mbingu na dunia na vitu vyote ni Utatu, hasa kwa sababu Mungu alipata mwili ili Aifanye kazi ya ukombozi, na pia kwa sababu ya suitafahamu zilizoibuka kutokana na watu kukosa kuuelewa ukweli wa kupata mwili. Ingawa watu wengi wanahisi kwamba ufafanuzi wa Utatu haufai kamwe, kwa kuwa hawajui ukweli wa kupata mwili wanamwekea Mungu mipaka kwa njia hii isiyoaminika. Isingekuwa kuja kwa Mwenyezi Mungu, kufichua siri za kupata mwili na kuchambua hili, uwongo mkubwa zaidi wa dunia ya dini tangu kuumbwa kwa dunia, hakuna mtu angeweza kutambua kosa katika ufafanuzi wa Utatu. Kwa kweli, tangu dunia ilipoumbwa, Mungu hajawahi kusema kwamba Yeye ni Utatu, wala Bwana Yesu mwenye mwili hakusema hivyo, na wala Roho Mtakatifu hajawahi kushuhudia kwamba Mungu ni Utatu—huu ni ukweli unaokubalika. Ufafanuzi wa Utatu ulitokea baada ya kuja kwa Bwana Yesu mwenye mwili, wakati ambapo kuliibuka miongoni mwa watu ufahamu wenye makosa kuhusu Mungu ikitokana na kukosa kwao ufahamu wa ukweli kuhusu kupata mwili. Ndani ya Biblia, watu wengi humwona Roho Mtakatifu akimshuhudia Bwana Yesu kuwa Mwana mpendwa, na wanamwona akimwomba Mungu Baba, kwa hiyo kunaibuka mawazo na fikira kuhusu Mungu, kana kwamba Mungu ni watu watatu—Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, watu wengi hawajui wanapaswa kumwomba Mungu yupi, wala hawajui ni Mungu yupi Anayetawala vitu vyote na kuamua vitu vyote. Watu wengine huhisi kwamba kumwomba Mungu mmoja si sahihi, kwa hivyo wanataka kuwajumuisha wale wengine wawili; wengine wanahisi mashaka wakimwomba Bwana Yesu pekee, kwa hiyo lazima wamjumuishe Yehova Mungu pia. Hili linawakanganya watu na kuvuruga mioyo yao. Wanafunzi wa wakati huo kwa kweli walimwuliza Bwana Yesu hali ya kweli ilikuwa ipi kuhusu Mungu Baba, na Bwana Yesu alijibu wazi, akisema: “Nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua…? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi?” (Yohana 14:9-10), “Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30). Baba na Mwana ni kitu kimoja, Mungu mmoja—huu ni ukweli kamili, bila kosa.

Hebu tuone ni nini Mwenyezi Mungu anasema: “Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba ‘Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.’ Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati huo huo awe ndani na juu ya ulimwengu. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. Ikiwa ni kama usemavyo, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi Hawa si watatu? Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, Mwana ni kingine, na Baba vilevile ni kingine. Nafsi Zao ni tofauti na viini Vyao ni tofauti, iweje basi ziwe kila moja Yao ni sehemu ya Mungu mmoja? Roho Mtakatifu ni Roho; hili ni rahisi kueleweka kwa wanadamu. Ikiwa ni hivyo basi, Baba ni Roho zaidi. Hajawahi kushuka kuja duniani na Hajawahi kupata mwili; Yeye ni Yehova Mungu katika mioyo ya mwanadamu, na kwa hakika Yeye vilevile ni Roho. Basi kuna uhusiano gani kati Yake na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Baba na Mwana? Au ni uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu? Je, kiini cha kila Roho ni sawa? Au Roho Mtakatifu ni chombo cha Baba? Hili linaweza kuelezwaje? Aidha kuna uhusiano gani kati ya Mwana na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Roho wawili au ni uhusiano kati ya mwanadamu na Roho? Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kuelezewa! Ikiwa Wote ni Roho mmoja, basi hapawezi kuwepo na mjadala kuhusu nafsi tatu, kwani zote zinamilikiwa na Roho mmoja. Kama Zingekuwa nafsi tofauti, basi Roho Zao Zingetofautiana katika nguvu zao na kamwe hawangekuwa Roho mmoja” (“Je, Utatu Upo?” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Hata hivyo, wengine wanaweza kusema: ‘Baba ni Baba; Mwana ni Mwana; Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, na mwishowe, Watafanywa kitu kimoja.’ Je, Utawafanyaje kitu kimoja? Baba na Roho Mtakatifu Wawezaje kufanywa kitu kimoja? Ikiwa Walikuwa wawili kiasili, haijalishi Wamewekwa pamoja kwa namna gani, je, Hawataendelea kuwa sehemu mbili? Unaposema kuwa kuwafanya kuwa kitu kimoja, huko si kuunganisha sehemu mbili kutengeneza kitu kamili? Je, Hawakuwa sehemu mbili kabla ya kufanywa kitu kizima? Kila Roho ana kiini kinachotofautiana, na Roho wawili Hawawezi kufanywa kuwa kitu kimoja. Roho si chombo cha kutengenezwa, si kama chombo chochote katika ulimwengu. Kulingana na mitazamo ya wanadamu, Baba ni Roho mmoja, Mwana ni mwingine, na Roho Mtakatifu tena ni mwingine, halafu Roho Hawa huchanganyika sawa na glasi tatu za maji kuunda kitu kimoja kizima. Je, hizo si sehemu tatu zimefanywa kuwa kitu kimoja? Haya bila shaka ni maelezo ya kimakosa! Je, huku si kumgawa Mungu? Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanawezaje kufanywa kuwa kitu kimoja? Je, Wao si sehemu tatu zenye asili tofauti?” (“Je, Utatu Upo?” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe?” (“Je, Utatu Upo?” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Mungu wa Utatu hayupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, na sembuse Baba na Mwana hutumia kwa pamoja Roho Mtakatifu kama chombo. Huu wote ni uongo mkubwa zaidi na haupo kabisa katika dunia hii! Hata hivyo uongo huu una asili yake na haukosi msingi kabisa, kwani akili zenu si punguani, na mawazo yenu hayakosi mantiki. Badala yake, ziko sawa na yenye ubunifu kwa kiasi kikubwa, kwamba haziwezi kuzuiwa hata na Shetani yeyote. La kusikitisha ni kwamba mawazo haya ni uongo mtupu na hayapo kabisa! Hamjaona ukweli halisi haswa; mnabuni na kujiundia dhana, na kuzitengeneza kuwa hadithi ili kuteka imani ya wengine kwa uongo na kupata mamlaka miongoni mwa wanadamu wapumbavu wasio na busara, ili kwamba waamini katika ‘mafundisho yenu ya kitaaluma’ makuu na mashuhuri. Je, huu ni ukweli? Je, hii ndiyo njia ya uzima ambayo wanadamu wanafaa kupokea? Huu ni upuuzi! Hakuna hata neno moja linafaa!” (“Je, Utatu Upo?” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo. Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!” (“Je, Utatu Upo?” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanachambua uwongo huu wa Utatu kwa ukali na uwazi kabisa: Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, Mungu ndiye Roho Mtakatifu na kuna Roho Mtakatifu mmoja pekee, kwa hiyo kuna Mungu mmoja pekee. Mungu ni Roho Mtakatifu na Roho Mtakatifu ni Mungu; ni njia tofauti tu ya kusema hivyo. Mungu mwenye mwili ndiye Roho Mtakatifu aliyepata mwili na asili ya mwili Wake bado ni Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi tunavyomwita tunapoomba, Mungu, Roho Mtakatifu na Mungu mwenye mwili wote ni Mungu mmoja, Roho mmoja. Huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuukana. Jinsi Mwenyezi Mungu anavyosema, “Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati huo huo awe ndani na juu ya ulimwengu. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote!” (“Je, Utatu Upo?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Sote tunajua vyema kwamba kuna Mungu mmoja pekee, ambaye ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anapojivika mwili na kuwa mwanadamu, kwa nini basi hatumtambui Mungu tena? Nasi tunamgawa Mungu mara tatu kabla ya kumwunganisha tena kuwa mmoja, tukimfafanua Mungu kama Utatu. Huu kweli ni upuuzi! Inaweza kuonekana kutoka kwa hili kwamba sisi wanadamu kweli hatuelewi masuala ya kiroho. Kwa kweli, bila kujali kile tunachosema kuuhusu, Utatu unajipinga; wakati wowote tunapousikia, unatuacha tukiwa na hisia kwamba haufai kabisa, kwamba ni wa wasiwasi kiasi. Tunajua wazi mioyoni mwetu kwamba kuna Mungu mmoja pekee, kwa hiyo Mungu huyu kweli Anaweza kuwa Utatu? Je, ni sawa kutumia ufafanuzi wa Utatu kumfafanua Mungu? Je, ni ufahamu wa kweli kuhusu Mungu? Kupitia uchunguzi na utambuzi wa Mwenyezi Mungu, inakuwa dhahiri kwetu sote jinsi ufafanuzi wa Utatu ulivyo wa upuuzi, na kwamba hakika ni uwongo mkubwa zaidi wa dunia ya dini. Je, kusema kwamba Mungu mmoja ni watatu si kumchonga vipandevipande tu? Je, si kukufuru kusisitiza kwa ukaidi kwamba Mungu mmoja, Roho mmoja, ana sehemu tatu? Mungu amekuwa mvumilivu kwa wanadamu kwa miaka elfu mbili, hadi siku za mwisho wakati ambapo Mungu amekuwa mwili mara nyingine ili kufunua na kuchambua kabisa kile kinachomuumiza zaidi—uwongo wa upuuzi zaidi wa dunia nzima ya dini—na kuwafanya wanadamu wote wapate uwazi na kuelewa kwamba kuna Mungu mmoja pekee, ambaye ni Roho Mtakatifu, na kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu mmoja wa kweli, ambaye ni Bwana wa uumbaji. Ingawa Mungu anapata mwili, bado Yeye ni Mungu mmoja. Hawezi kabisa kugeuka kuwa Mungu wawili au Roho wawili, na hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu. Bwana Yesu alikuwa Yehova Mungu aliyejivika mwili; Bwana Yesu alikuwa dhihirisho la Yehova Mungu. Hiyo ni kwa sababu asili ya mwili Wake ni Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu ni Yehova Mungu, kwa hivyo Wao si Mungu mmoja? Ikiwa sisi, kama wanadamu, hatuwezi kamwe kuona ukweli rahisi kama huo vizuri, je, hilo halimaanishi hatuna ufahamu wa masuala ya kiroho? Si ajabu Bwana Yesu alisema: “Nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo?” (Yohana 14:9). Inavyoonekana, sisi wanadamu wapotovu kweli hatuwezi kumjua Mungu kwa urahisi, na Mungu Mwenyewe asingefichua siri ya ukweli wa kupata mwili, basi hakuna mtu angeweza kuielewa. Bwana Yesu alionekana kwa mwanadamu binafsi ili kuzungumza na kufanya kazi na, aidha, hili lilirekodiwa katika Biblia. Kwa miaka elfu mbili, hakuna mtu amemjua Bwana Yesu kwa kweli sembuse yeyote kuelewa ukweli wa kupata mwili. Wangekuwa wameelewa kwa kweli, basi hawangemfafanua Mungu kama Utatu. Katika dhana zetu tunaamini kwamba Yehova Mungu ni Mungu aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote na ambaye Anatawala vitu vyote, kwamba Bwana Yesu ni Bwana wa watakatifu wote, Kristo, Mwokozi, na kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu anayefanya kazi, hivyo kuupa Utatu mgawanyo dhahiri wa kazi. Kila mmoja wa hao watatu anayeunda Utatu ana miliki Yake mwenyewe—Mmoja anawajibikia mbingu, Mmoja anawajibikia nchi, na Roho Mtakatifu anawajibikia kufanya kazi ndani ya mwanadamu. Tukizigawa kazi za Mungu kwa njia hii, je, hili halikanushi uweza wa Mungu na hekima Yake yote kabisa? Mungu ni Mungu anayejumuisha yote; Yeye ni mwenye kudura. Tukikiri kwamba Mungu ni mwenye uweza, mwenye kupatikana kila mahali na mwenye kudura, kwa nini basi tumgawe Mungu mara tatu? Kwamba tunaweza kumgawa Mungu mara tatu inaonyesha kwamba hatuelewi uweza wa Mungu na asili Yake ya kujumuisha yote. Hatukiri uweza wa Mungu, tukifikiri kwamba Yeye hawezi kufanya mambo haya, na kwa hiyo tunamgawa kwa njia hii, kana kwamba ni jambo la maana kwa Mungu pekee kufanya kazi kwa namna hiyo—huu ni mgao unaotegemezwa kikamilifu kwa fikira na mawazo ya mwanadamu. Ni dhahiri kwamba Mungu ni Mungu mmoja, kwa hiyo, je, kusisitiza kumkata Mungu awe sehemu tatu ni tendo la mtu anayemcha Mungu? Je, mtu wa aina hii ana uchaji wowote wa Mungu? Je, tendo hili si la majivuno na la kujidai sana? Je, si kumkata Mungu na kumwekea mipaka kwa njia hii ni kumwasi na kumkufuru kwa kweli? Tunaweza kuona kutoka kwa uchambuzi na ufunuo wa Mwenyezi Mungu wa ufafanuzi wa Utatu kwamba wanadamu wapotovu kumfafanua Mungu kama Utatu ni jambo linalomuumiza Mungu zaidi. Ni sawa na kumkata Mungu mara tatu, kisha kumwunganisha tena kuwa mmoja. Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, kwa hiyo wanadamu wangeruhusiwa vipi kumkata Mungu kwa njia hii? Kwa hiyo, Mungu anasema katika “Je, Utatu Mtakatifu Upo?”: “Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Mungu wa Utatu hayupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, na sembuse Baba na Mwana hutumia kwa pamoja Roho Mtakatifu kama chombo. Huu wote ni uongo mkubwa zaidi na haupo kabisa katika dunia hii!” “Hakuna wakati ambapo wazo hili la Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu linaweza kuwa na mashiko; ni uongo ambao ni nadra kuonekana na halipo!” (Neno Laonekana katika Mwili). Huku ni Mungu akichambua na kufunua uwongo wa Utatu kwa ulimwengu mzima. Kama, tunapoyaona maneno ya Mungu, bado hatuwezi kuyaelewa na bado hatuukubali ukweli, basi tunamwasi Mungu na tunaweza tu kushutumiwa na kuondoshwa na Mungu.

Kimetoholewa Kutoka Katika Majibu ya Mswada wa Filamu

Neno Utatu lilitoka kwa kinywa cha nani? Je, ni kushuhudia kwa Roho Mtakatifu ama lilisemwa na Bwana Yesu Mwenyewe? Ama ni muhtasari kutoka kwa wanadamu wapotovu? Kwanza, Mungu hakusema hili; pili, Roho Mtakatifu hakutoa nuru hivyo; tatu, hakuna nabii au mtume alilisema. Kwa hivyo, msemo huu si neno la Mungu, bali badala yake umetoka kwa vinywa vya wanadamu na umejumlishwa na wanadamu wapotovu. Sote tunajua kuwa kuna Mungu mmoja tu. Mungu mwenye mwili ana dutu ya Uungu. Baada ya Yeye kukamilisha kazi Yake katika mwili na kurudi kwa ulimwengu wa roho, Atakuwa na utambulisho wa asili wa Mungu. Utambulisho wa asili wa Mungu ni Roho, Mungu mwenye mwili ni udhihirisho wa Roho katika mwili wenye kufa, ilhali dutu bado ni Roho. Kwa hivyo, kuna Mungu mmoja tu. Wakati mwingi Anatekeleza kazi Yake miongoni mwa wanadamu kama Roho. Wakati ni muhimu kufanya kazi kama Mungu mwenye mwili, Anapata mwili lakini hiyo ni kwa muda mfupi tu. Kwa hivyo, haijalishi jinsi inavyosemwa, kuna Mungu mmoja tu. Mungu ni Roho. Baada ya Yeye kukamilisha kazi Yake kupitia kwa kupata mwili kuwili, Hatapata mwili tena; Mungu kufuatia hiyo atakuwa Roho milele. Watu watatu ndani ya mmoja—Baba Mtakatifu, Mwana Mtakatifu, Roho Mtakatifu hawako hata kidogo na njia hii ya kuongea haidumu. Mungu hakuwahi kusema kwamba Yeye ni watu watatu ndani ya mmoja, Yehova Mungu hakusema hili katika Agano la Kale, Bwana Yesu kama Mungu mwenye mwili hakusema hili katika Agano Jipya, katika kazi Yake ya kufuatia Roho Mtakatifu hakusema hili. Kwa hivyo, kauli hii haidumu kabisa. Je, Bwana Yesu aliionyesha vipi? “Mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19). Wakati watu wanabatiza, wanaweza kuita jina la Bwana, jina la Roho Mtakatifu, na pia wanaweza kuita jina la Mwana, lakini hii kwa hakika si kuunganisha pamoja majina ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, haimaanishi hili. Si sahihi kwa watu wa dini kugeuza kauli hii kuwa virai. Kwa sababu wakati huo watu wengi walikuwa hawana uhakika kuhusu utambulisho wa Bwana Yesu, Bwana Yesu aliwaruhusu kuliita jina la Bwana. Lakini kwa kweli wakati watu walikuwa na uhakika kwamba Yesu alikuwa Bwana, kwamba Alikuwa Mungu mwenye mwili, wangeliita jina la Yesu moja kwa moja. Hakukuwa na haja ya wao kuliita jina la Bwana, sembuse haja ya wao kuliita jina la Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, kuna sababu kwamba Mungu alisema maneno hayo wakati huo, kwa kuwa watu wengi hawakuwa wamemkubali Bwana Yesu, wala hawakukiri Bwana Yesu. Kwa hivyo, Alisema maneno kama hayo ambayo yanaeleweka zaidi na kukubaliwa na watu, lakini wakati watu wa dini wanaona kuita majina tatu ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama virai, basi ni jina la nani wanaloliita hata hivyo? Wanadamu wamekosea, jina moja litatosha na hilo ni kuita jina la Yesu. Yesu ni Baba. Bwana Yesu aliwahi kusema, “Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30). Baba na Mwana kwa asili ni moja, sivyo? Yeyote anayeita majina ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haelewi roho, ameelewa kimakosa maneno ya Bwana Yesu; je, maelezo kama hayo ni sahihi au la? Ni sahihi sana. Kwa nini wanadamu wapotovu hawaelewi neno la Mungu, lakini wanaelewa maneno ya Bwana Yesu kwa njia isiyo sahihi na wanamgawanya Mungu kwa vipande hivi tatu? Ni kwa sababu mwanadamu hana welekevu wa kutumia kuelewa ukweli. Kwa hivyo, wakati ambapo Mungu mwenye mwili aliongea na wanadamu, ugumu fulani ulitokea, na Aliwaambia kwamba wangeweza kuita neno la Baba, kwamba wangeweza pia kuita neno la Mwana, na wale ambao wangeweza kumkubali Bwana Yesu kama Mungu mwenye mwili wangeweza kuliita jina la Mwana, na wale ambao hawangeweza kukubali kwa kweli wangeweza kuliita jina la Roho Mtakatifu. Tunaweza kuona huruma ya Mungu kwa mwanadamu na pia tunaweza kutambua wema wa Bwana Yesu kwa udhaifu na ujinga wa mwanadamu. Kuhusu suala hili, Mungu hakuwa mwenye kuchagua sana na tunapaswa kuelewa maana ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia: Swali la 38: Katika miaka ya hivi karibuni, makundi ya kidini na madhehebu mbalimbali katika ulimwengu wa kidini yamekosa matumaini zaidi na zaidi, watu wamepoteza imani yao ya asili na upendo na wamekuwa hasi zaidi na zaidi na dhaifu. Pia tunahisi kunyauka kwa roho na tunahisi kuwa hatuna chochote cha kuhubiri na kwamba sote tumepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Tafadhali tuambie, kwa nini ulimwengu wote wa kidini umekosa matumaini hivyo? Mungu kweli anauchukia na umetelekezwa na Mungu? Tunafaaje kuelewa laana ya Mungu ya ulimwengu wa kidini katika Kitabu cha Ufunuo?

Inayofuata: Swali la 40: Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, huonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na bado Yeye hukabiliwa na uasi mkali na uchukuliwaji wa hatua kali wa ukatili wa ulimwengu wa kidini na serikali ya Kikomunisti ya China. Serikali ya CCP hata huhamasisha vyombo vyake vyote vya habari na majeshi kumshutumu Kristo, kukufuru dhidi Yake, kumtia mbaroni na kumwangamiza. Wakati Bwana Yesu alizaliwa, Mfalme Herode alisikia kuwa “Mfalme wa Israeli” alikuwa amezaliwa na akaamrisha watoto wote wa kiume wauawe Bethlehemu na wa chini ya umri wa miaka miwili; ingekuwa afadhali kwake kuwaua watoto elfu kumi kuliko kumwacha Kristo aishi. Mungu amekuwa mwili ili kuwaokoa wanadamu, hivyo kwa nini ulimwengu wa kidini na serikali kana Mungu hushutumu na kukufuru dhidi ya kuonekana na kazi ya Mungu? Kwa nini wanaipinda nguvu ya nchi yote na kutumia jitihada zote kumtundika Kristo msalabani? Kwa nini wanadamu ni waovu sana, na kwa nini wanamchukia Mungu hivyo na kujiweka dhidi Yake?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Tofauti kati ya njia ya toba na njia ya uzima wa milele

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki