Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

79. Jikosoe Kabla ya Kuwakosoa Wengine

Chongxin Mkoa wa Shanxi

Inasemwa katika ushirika mmoja: "Viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuwa na moyo wenye upendo, uvumilivu, ufahamu, na lazima wawatendee watu kwa njia inayofaa. Lazima waendeshe mambo yao kwa mujibu wa kanuni za kweli na kuwatendea watu bila mapendeleo" ("Masuala 12 ya Haraka Ambayo Makanisa Kutoka Maeneo Yote Yanapaswa Kutatua" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirikiano na Mipango ya Kazi ya Kanisa II). Katika siku za nyuma, sikuwahi kuvijali sana vifungu vya kuwasiliana kwa karibu kuhusu jinsi viongozi na wafanyakazi wanavyopaswa kutenda kwa njia ya huruma, kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni za kweli, na kuwatendea watu kwa haki kwa sababu siku zote nilijiamini kuwa mpole kabisa. Sikuwa kama wengi wa watu wasaliti, watu wanafiki wa ulimwengu wa kidunia. Pia, tangu kuwa kiongozi, sikuwa nimeyakomesha maoni ya wengine au kumtenga mtu yeyote kutoka katika majadiliano. Hii ikiwa ndiyo hali, nilijisifu kuwa mwaminifu, mwenye haki na wa kutopendelea. Wakati wowote niliposikia juu ya viongozi wa uongo na wafanyakazi kutowatendea watu haki au kucheza na kukuza wapenzi huku wakiwakandamiza na kuwatenga wengine, daima ningewadharau. Nilidhani kuwa viongozi na wafanyikazi kama wale lazima ni wakatili na, kwa hivyo, wasiostahili kuhudumu kama viongozi au wafanyakazi. Baada tu ya uzoefu wa hivi karibuni ambao ulifunua asili yangu ya kweli na kuniruhusu kupata ufahamu juu yangu mwenyewe ndipo nilitambua mimi si mtu mwaminifu wala mwadilifu niliyefikiri kuwa. Badala yake, niligundua kuwa nilikuwa nikiwatendea watu kulingana na hisia na mapendeleo. Katika uchunguzi wa manufaa yangu mwenyewe, nilikuwa tu mjanja, mwenye hila, mbinafsi na mwovu kama mtu mwingine yeyote. Kwa njia tu ya hukumu na adabu ya neno la Mungu ndipo niligundua kwamba njia yenye manufaa zaidi, njia ya haki zaidi na isiyo ya mapendeleo ya kuwatendea watu ni kwa kufanya kulingana na kanuni za kweli. Zaidi ya hayo, nilitambua umuhimu wa maana sana, kama kiongozi, wa kuwatendea watu kwa haki.

Mnamo Juni 2013 nilisafiri kwenda jimbo jingine kushirikiana kwenye kazi fulani ya kanisa. Katika wilaya hii, mmoja wa viongozi wawili alikuwa dada kutoka makazi yangu ya kudumu, "dada A." Katika siku za nyuma, tulikuwa tumeshirikiana katika kazi mbalimbali na tulikuwa na uhusiano mzuri sana. Kama unavyoweza kufikiri, nilifurahi sana kumwona tena mbali sana na nyumbani na baada ya muda mrefu. Kiongozi huyo mwingine, "dada B," alikuwa amechaguliwa kama kiongozi na alikuwa mndani zaidi na mwenye akili thabiti. Alikuwa amepandishwa cheo wakati tu sisi viongozi tulipokuwa tukienda katika mfungo wa kujiendeleza kiroho. Kama ilivyotokea kuwa, dada wale wawili na mimi tuliishia kufanya mfungo wetu katika familia sawa yenyeji. Kutokana na siku zetu zilizopita, dada A na mimi bila shaka tulikuwa wandani wa karibu sana tangu mwanzo. Yeye na mimi tuna hulka sawa—sisi sote tu wacheshi kabisa—hivyo kwa kawaida nilimpenda na nilikuwa radhi kushirikiana ikiwa tungekutana na masuala yoyote. Baadaye, nilianza kutambua kuwa uhusiano huu wa karibu ambao tulikuwa nao haukufaa kwa kazi yetu na haungeruhusu manufaa ya sisi sote wawili, hivyo nikaanza kusita kwa makusudi, kuasi dhidi ya mwili wangu. Wakati huo, nilikuwa na wasiwasi kwa kiasi fulani kwa sababu dada hao wawili hawakuwa wakifanya kazi vizuri pamoja; wote walikuwa na ubaguzi wao. Wakati wowote dada B alipohisi kushurutishwa, nilihakikisha kuwasiliana kwa karibu naye na kumpa moyo na mwongozo. Pia ningetumia muda mfupi na dada A kimakusudi kwa hofu kwamba dada B angehisi kuwachwa au mwenye huzuni. Wakati wowote nilipoona kuwa dada A alikuwa amefunua tabia yake ya kujivuna na ya ubinafsi, ningemshughulikia na kumkosoa bila kusita hata kidogo. Singempendelea au kumlinda tu kwa sababu tulikuwa marafiki wa karibu. ... Nilidhani kwamba, kwa kufanya hivyo, nilikuwa nikiwatendea dada zangu kwa haki na kwa mujibu wa nia ya Mungu. Sikujielewa, lakini Mungu alinibaini. Katika siku zilizofuata, Yeye angefunua hali yangu ya kweli ya kishetani, akitoa uovu wangu la ndani kwa mwanga wa hukumu.

Mwanzoni mwa mfungo wetu, ili kuhakikisha kwamba tuliimaliza kazi yetu kwa kasi na kujitolea katika kujiendeleza kiroho, tuligawa kazi sawasawa kati ya sote watatu: Dada A angekuwa na jukumu la kupanga na kutekeleza mambo yote ya nje, wakati dada B na mimi tungewajibika kuyashughulikia masuala yoyote yaliyotokea ndani ya makanisa. Katika mradi mmoja, sikuwa nimetekeleza wajibu wangu, nikapuuza kuwasilisha habari za mradi huo kwa dada yangu na kumwacha kujitegemea mwenyewe. Baada ya yeye kukamilisha mradi huo, pia nilipuuza kwenda kuchunguza kazi yake na, kwa sababu hiyo, kulikuwa na matatizo katika mradi huo. Athari, kiongozi wetu alituandikia barua akionyesha makosa yetu na nia zetu. Nilisikitishwa sana, na nikadhani: Baada tu ya kufika hapa, tayari nimefanya kosa la msingi kama hilo; mimi ni nyangarika na nimejifanya kuonekana kama mpumbavu kamili! Je, kiongozi huyo atanifikiriaje sasa? Je, kiongozi atasema kuwa sina ukweli na siwezi kutekeleza kazi? Nilipofikiri juu ya yote haya, ghafula nilihisi chuki kubwa kwa dada yangu. Nilichukia kwamba alikuwa amenisababisha mimi kujifanya kuonekana mpumbavu. Katika mazingira haya mapya, nilipuuza kujifunza kutoka kwa makosa yangu na sikuyapima makosa yangu ili kurekebisha makosa yangu. Zaidi ya hayo, sikuwa radhi kulibeba jukumu na, kulinda hadhi yangu na sifa, nilikwenda kinyume na dhamiri yangu nzuri na kufanya jambo lenye kudharauliwa—nilimpa wajibu wote dada yangu. Sikuweza kuamini kuwa nilikuwa nimefanya vitendo vile vibaya —nilikuwa mtu wa aina gani? Katika hatua hii, niliweza kuhisi lawama ya Roho Mtakatifu na hukumu iliyowekwa juu ya dhamiri yangu. Hata hivyo, moyo wangu ungekuwa mgumu wakati ambapo nilifikiria jinsi dada yangu alivyoharibu sifa na hadhi yangu. Sikushindwa tu kujiweka wazi kwa dada yangu, hata nilimdharau sirini na kufuatilia ajenda yangu mwenyewe katika kuwasiliana kwetu kwa karibu kwa neno la Mungu. Ikiwa sikuwa nikimlaumu dadangu papo hapo, nilikuwa nikihepa jukumu lolote na kugeuzia lawama dadangu ili kumfanya kila mtu kufikiri kuwa suala hilo lilikuwa tokeo la makosa yake. Hata nilimhukumu dada bila ufahamu wake: nikiwa na shaka kama Roho Mtakatifu alikuwa akimfanyia kazi na ikiwa angeweza kufanya kazi hii. Mwishoni, nilipata kile nilichotarajia: Mungu alinifundisha nidhamu na niliteseka kutokana na vidonda vya kinywa. Hata hivyo, sikurekebisha njia zangu, nikawa hodari katika uasi wangu dhidi ya Mungu na kumchukia dada yangu. Sikutenda ukweli na nikawa mtu aliye na hatia, nisiweze kabisa kumtendea dada yangu kwa haki. Nilitupa jicho la kutoridhia juu ya kazi yake yote—ilionekana kwangu kuwa hakuweza kufanya chochote chema. Nilikuwa nimekwisha kupoteza kusudi langu la kwanza la msaada wa upendo na kumtendea kwa dharau, nikijitia hamnazo kama ya biashara. Nilijua kuwa kulikuwa na kitu kibaya na mtazamo wangu, lakini asili yangu ya kishetani ilinisababisha kushindwa kukabiliana na ukweli na kuchukua jukumu la makosa yangu. Badala yake, nilitumia hadhi yangu kutawala kwa hila na kwafundisha waliokuwa chini yangu nidhamu, nikiishi kwa kanuni kwamba "Anachosema bwana hutendeka"; hii, kanuni yenye sumu hakika ilitoka kutoka kinywa cha joka kuu jekundu lenyewe. Vile nilivyomtendea dada haikuwa tofauti na mamlaka dhalimu ya mabavu ya joka kubwa jekundu. Katika matendo yangu, mtu angeweza kuona uso mbaya wa kutisha wa Shetani ukifichuliwa kikamilifu. Mara ya kwanza, dada hakuonyesha hisia mbaya. Licha ya kushughulikiwa, alijaribu kuona nia ya Mungu na kuingia kwa njia ya utendaji. Hata hivyo, sikuweza tu kufumbia macho hilo: Kitu kiliponikumbusha "tukio lile" katika kazi yetu ya sasa, siku zote nililazimika kulitaja ili kumshughulikia. Polepole, dada hakuwa makini sana katika kazi yake. Alisita kufanya kitu chochote mwenyewe na hakuweza kushirikiana kikamilifu. Nilipoona jinsi alivyofanya, nilikuwa na hasira sana. Kisha, ilipokuwa dhahiri kwamba dada wawili walikuwa na shida katika kushirikiana, nilipandwa na mori kabisa. Nilidhani: Nimekuja hapa kuwasaidia dada wawili katika kazi yao, lakini wakati wote huu sijaweza kutatua masuala yao—je, hii halinifanyi mimi kuwa bure kabisa? Niliendelea kuwashughulika wawili hao na nilihisi kuwa nilikuwa na majukumu mengi, lakini yote hayakuwa na uwezo wa kufanikisha lolote kabisa. Bila kujali ni kiasi gani niliwasiliana kwa karibu na wawili hao, nilionekana kutoweza kuyarekebisha mambo. Nilikuwa sina uwezo wa kutatua masuala yao, na, hata zaidi, wote wawili walikuwa na ubaguzi dhidi yangu na walilalamika juu ya jinsi nilivyopendelea. Nikikabiliwa na hali hii, sikujua cha kufanya. Nilikuwa nimetumia uwezo wangu wote na hakukua na lolote ambalo ningeweza kufanya. Zaidi ya hayo, nilikuwa nimekwisha kuchoshwa na wawili hao na nikadhani kuwa yote ilikuwa shauri lao, kwa sababu hawakuwa radhi kutenda ukweli na kufanya mabadiliko mazuri.

Nikiwa bila tumaini kabisa, nilimwomba Mungu, nikitafuta mwongozo. Wakati wa sala, nilikumbuka kifungu katika ushirika kutoka hapo juu ambacho husema, "Katika siku za nyuma kulikuwa na semi mbili, 'Jikosoe kabla ya kuwakosoa wengine' na 'Mtu aliye na kosaanawezaje kuwakosoa wengine?' Zungumza kuhusu uzoefu wako mwenyewe. Kwa kuzungumzia uzoefu wako, unawasaidia wengine na kujikosoa. Unawasaidia wengine kwa kujikosoa mwenyewe, na, wakati huo, unaweza pia kuwakosoa wengine. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kufanya kazi yako. ... Kadiri unavyozidi kuwa mwadilifu, ndivyo unavyozidi kushikilia hisia ya haki na kunena bila mapendeleo na kwa haki, ndivyo watu wengi watakavyozidi kukupenda, kupenda kukusikiliza unapowasiliana kwa karibu na kuyathibitisha maneno yako. Kama tu unavyosema, ndivyo watakavyofanya. Utahitaji tu kusema neno moja, na watafanya kulingana na matakwa yako. Bila kujali unalosema, hakuna mtu atakayelalamika, hata kama unasema kwa ukali. ... Ukibaki kuwa na uaminifu, ukiwatendea watu wote kwa haki na daima kuwasaidia watu kwa moyo wenye upendo, hatimaye utaweza kuwaleta watu katika kweli. Utakuwa na uwezo kabisa wa kuwaleta watu katika uhalisi wa neno la Mungu na wokovu Wake" ("Jinsi Viongozi na Wafanyakazi Wanavyotakiwa Kuongoza na Kufanya Kazi" katika Ushirikiano na Kuhubiri Kuhusu Kuingia katika Maisha I). Kisha nikafikiria kifungu hiki cha neno la Mungu: "Bila Mungu, uhusiano kati ya watu ni uhusiano wa mwili tu. Sio uhusiano unaofaa, bali ni uendekezo wa tamaa za mwili—ni uhusiano ambao Mungu anachukia, Asioupenda … kuwa huna uhusiano unaofaa na Mungu kamwe. Unajaribu kumdanganya Mungu na kuficha ubaya wako mwenyewe. Hata ingawa unaweza kushirikisha uelewano kiasi lakini unabeba ubaya moyoni mwako, kila kitu unachofanya ni kizuri tu kwa kiwango cha mwanadamu. Mungu hatakusifu—unatenda kulingana na mwili, sio kulingana na mzigo wa Mungu. Iwapo unaweza kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu na kuwa na ushirikiano wa kufaa na wale wote wanaompenda Mungu, ni hapo tu ndipo utakuwa uko tayari kwa matumizi ya Mungu. Kwa njia hii, haijalishi jinsi unavyopatana na wengine, haitakuwa kulingana na falsafa ya maisha, lakini itakuwa kuishi mbele ya Mungu, kuufikiria mzigo Wake" ("Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupitia neno la Mungu na ushirika wa mtu, mara moja nilikuja kutambua kwamba ukitaka kufanikiwa katika kazi yako kama kiongozi au mfanyakazi, lazima kwanza uwe sahihi, uwe na uwezo wa kuwatendea wengine kwa usawa, na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Katika kuwasiliana kwa karibu na wengine, unapaswa kushiriki uzoefu wako binafsi bila nia zozote zilizofichika za kuwasaidia wengine. Njia hii ya kutenda hutimiza nia ya Mungu na itajipatia makubaliano ya wengine. Chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, nilituliza moyo wangu na kutafakari juu ya mtazamo wangu kwa dada wawili: Mwanzoni niliweza kutoa msaada wenye upendo kwa dada aliyepandishwa cheo hivi karibuni, lakini hiyo ilikuwa tu kwa sababu hali yetu haikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na faida yangu binafsi. Dada alipofanya kosa ambalo liliharibu sifa na hadhi yangu, hali yangu ya kweli ilifichuliwa. Kama "mchawi mbaya" katika mahubiri ya sabini na tano, ambaye, akiwa na rungu au jambia, hukomesha yote yanayomzuia. Juu juu, ingeonekana kwamba nilikuwa tu nikishughulikia masuala ya kazi ya dada, lakini kwa kweli nilikuwa nikitoa nje kukata tama kwangu mwenyewe. Kwa sababu hiyo, nilizungumza kwa njia isiyo ya adabu na kwa ukali ambayo ilimfanya dada kuhisi kuwa nilikuwa nikimwangalia kwa dharau na kumtukana. Nilipoona jinsi dada huyo alivyochukulia vibaya kushughulikiwa kwake, sikumhurumia tu, ila pia nilimchukulia kwa dharau na maudhi. Nilipopandishwa cheo mara ya kwanza ili kutimiza wajibu wangu, kulikuwa na vitu vingi ambavyo sikujua wakati huo huo pia. Nikiwa nimekazwa na sifa na hadhi yangu mwenyewe, pia nilijaribu sana kutenda na utendaji wangu uliathiriwa. Ilikuwa mbaya sana kwamba mara nyingi ningechukua muda wa kulia faraghani; wakati mmoja nilifika ambapo Roho Mtakatifu aliacha kufanya kazi ndani yangu. Hata hivyo, kiongozi wangu na wafanyakazi wenzangu hawakunidharau, wakifanya kazi kwa bidii ili kunisaidia na kunitia moyo mpaka hatimaye nikawa huru kutoka kwa shida yangu na kujisikia kujitokeza tena upya. Hata hivyo, dada yangu alipokuwa akipitia hali hiyo hiyo, nilifumbia macho siku zangu za zamani. Sikushindwa tu kushiriki uzoefu wangu mwenyewe katika kuwasiliana kwa karibu ili kumsaidia dada yangu, ila pia nilimlaumu, kumpiga wakati ambapo alikuwa chini na kufurahia kuteseka kwake. Hapo tu ndipo nilipotambua hali mbaya ya ubinadamu wangu na kwamba "msaada" wangu wa kudhaniwa kwa dada yangu katika siku za nyuma wote ulikuwa umekuwa unafiki na udanganyifu. Kwa sababu nilikuwa na mapendeleo ndani ya moyo wangu, bila kujali jinsi nilivyomtendea kwa ukunjufu, au jinsi mzigo wangu ulivyokuwa mkubwa, sikutenda kwa moyo wa upendo wa kweli na sikumtendea kwa haki. Baada ya kumtendea kwa namna hii, nilitarajiaje dada kuweka imani yake kwangu? Kwa mintarafu tadada niliyekuwa karibu naye, licha ya kuwa nilimwekea viwango vikali, bado kulikuwa na sehemu ya kihisia katika uhusiano wetu. Nilichukua jukumu la dada mkubwa kwake. Wakati mwingine nilimkemea kama mzazi anavyomkaripia mtoto wake: Ningekuwa na wasiwasi wakati alipofunua upotovu wake, lakini wasiwasi huu ulitokana na uhusiano wa kihisia. Nilikuwa nikifanya kulingana na mwili wangu na kuonyesha upotovu wangu, sio kutokana na hisia ya mzigo kwa Mungu Kadiri nilivyozidi kumtendea dadangu kwa njia hii, ndivyo hali ya kihisia iliyofunga mwili wetu ilivyozidi kuwa nzito. Hii haikusaidia kwa njia yoyote au kuwa na faida kwa dada yangu. Hapo ndipo nilipogundua sababu ya msingi ya kushindwa kwangu kufanikiwa katika kazi: Sikukuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Licha ya ukweli kwamba niliwasiliana kwa karibu neno la Mungu nilipowasaidia dada kuyatatua matatizo yao, bado nilikuwa na mapendeleo yangu mwenyewe na nilijitahidi kulinda maslahi yangu ya kimwili badala ya kuelekeza moyo wangu kwa Mungu na kufanya kazi ili kutimiza matakwa ya Mungu. Kutoka nje, ingeonekana kwamba nilikuwa nikiubeba mzigo wangu, lakini kwa kweli nilikuwa nikimhadaa Mungu na kuficha asili yangu ya ajabu. Mungu hawakubali wale ambao hawana nia njema, kwa hivyo nilishindwa kufanikiwa na hata nikawa na matokeo yasiyotamaniwa. Kupitia kutafakari, nilitambua mimi sio mtu mpole, mwenye haki au mwenye kutopendelea hivyo. Kwa hakika, mimi ni mbinafsi, mlaji njama na mwovu mbaya. Katika hatua hii, nilifikiria ushirika mwingine kutoka hapo juu, "Katika nyaraka za baadaye, Paulo alikuwa mwepesi wa kumdunisha Petro. Mara moja, hata alimshutumu Petro mbele ya umati. Hakuweza kughairi. Hii inajulikana vyema kuwa ilifanyika. ... Sasa, Petro alimwainishaje Paulo? Alisema, 'Ndugu Paulo amepokea ufunuo wa Mungu, sikiliza injili yake ya ushuhuda kwa Mungu. Amepokea ufunuo wa Mungu. Sio tu kwamba Petro hakumtukana Paulo, hata akamwita ndugu. Je, Petro alikuwa amemtendea Paulo haki na bila mapendeleo? Alimtendea kwa haki. Utathmini wake kwa Paulo ulikuwa wa haki na wa usawa. Kwa nini Petro alitaja uwezo wa Paulo? Petro alikuwa mtu ambaye alikuwa ameboresha tabia yake ya maisha, alikuwa akimjua Mungu na aliweza kuwatendea watu kwa haki. Paulo, kinyume chake, alikuwa na kiburi na ubinafsi, akikosa kutokubali kumtii mtu yeyote katika kupenda makuu kwake" (" Mtu wa Aina Gani Atatimilizwa na Mungu" katika Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia katika Maisha VII). Nilipolinganisha matendo yangu na yale ya Petro na Paulo, ilionekana kwangu kwamba nilikuwa hata mbaya zaidi kuliko Paulo kwa kila njia. Kama kiongozi aliyekabiliwa na kushughulikia masuala yaliyotokea katika kazi yetu, sikushindwa tu kuchukua kikamilifu jukumu la masuala hayo, kuongoza njia katika kutenda ukweli, kutafuta ukweli na dada zangu, kutatua matatizo yaliyokuwako na kulinda maslahi ya familia ya Mungu, lakini pia nilimtukana na kumdhuru dada yangu katika kutafuta faida yangu binafsi. Kwa hakika sikuwa nimeboresha tabia yangu hata kidogo. Nikimwangalia dada yangu: Kuanzia mwanzo hadi mwisho alibakia katika kukubali kwa utulivu, kamwe bila kujaribu kuibua suala nami. Tabia yake ilikuwa hukumu kwangu—maonyesho ya ubaya wangu kama wa panya. Vitendo vyangu vilikuwa chini ya ubinadamu—hakukuwa na wema wowote katika kile nilichokifanya. Hakika, tabia yangu haikufaa kwa kiongozi.

Nilipotafakari juu ya yote haya, nilihisi hasa kusononeka. Kabla ya hapo, sikuzote nilifikiri kwamba nilikuwa na upole sana na nilikuwa nimewatendea watu kwa haki sana. Baada ya kufanya mambo hayo ya aibu, nilikuwa na hofu zaidi na zaidi. Ikiwa mtu angeweza kufafanua nafsi yangu mbaya, bila shaka ingefanana na mnyama mbaya, mwenye jino kali lenye sumu na lenye kutoa damu kinywani mwake. Siku moja nilisoma kifungu kinachofuata kutoka katika "Jinsi ya Kuandika Mahubiri Mema" katika Ushirikiano na Kuhubiri Kuhusu Kuingia katika Maisha IX: "Wale ambao hawapendi ukweli ni wakatili, wale wanaochukia ukweli ni waovu." Nilijisikia kuchomwa moyoni, kama kwamba mstari huu ulikuwa hukumu ya Mungu kwangu. Kristo na Roho Mtakatifu hutawala juu ya familia ya Mungu kwa haki na bila mapendeleo: Wangewezaje kuvumilia kuwepo kwa kitu chochote ambacho hakikufuatana na ukweli? Vitendo vyote vya udhalimu vya kishetani lazima vikutane na hukumu yenye haki ya Mungu. Nilipofikiri juu ya uovu wangu na ukatili, dhamiri yangu ililemewa na lawama. Kuishi gizani na maumivu bila fursa ya kutokea, sikujua sana jinsi ya kukabiliana na dada zangu. Yote niliyoweza kufanya ni kwenda mbele ya Mungu na kutafuta uongozi Wake kupitia maombi: "Mungu mpendwa, nimechanganyikiwa na kuteseka sana, nimepoteza njia yangu. Sijui jinsi ya kukabiliana na dada zangu, na hata zaidi sina habari kuhusu jinsi ya kutimiza majukumu yangu. Ninakuomba unipe nuru kuhusu suala hili la ukweli." Nilipomaliza maombi yangu, nilifungua kanuni ya nambari 42 ya kanuni 162, "Kanuni ya Kuwatendea Watu Kwa Haki" na kusoma yafuatayo ya neno la Mungu, "Je, neno la Mungu linahitaji nini kama kanuni ya kuwashughulikia wengine? Lipendeni alipendalo Mungu, lichukieni alichukialo Mungu. Yaani, watu wanaopendwa na Mungu ambao kwa kweli wanaufuata ukweli na ambao huyafanya mapenzi ya Mungu, ndio watu mnaopaswa kuwapenda. Wale wasioyafanya mapenzi ya Mungu, wanamchukia Mungu, wanamkaidi Mungu, na wanadharauliwa na Mungu, ni watu tunaopaswa kuwadharau na kuwakataa. Hilo ndilo neno la Mungu linahitaji" ("Ili Uweze Kujielewa, Lazima Uelewa Mitazamo ya Mizizi yenye Kina ndani yako" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). "Kuhusu hali za watu, wengine waliwahi kupinga, wengine waliasi, wengine walizungumza maneno ya malalamiko, walijishughulisha na mienendo mibaya, walifanya vitendo dhidi ya kanisa au walifanya mambo yaliyoharibu familia ya Mungu. Matokeo yao yataamuliwa kwa kuzingatia asili yao na upana kamili wa tabia zao. … Tabia ya kila mtu ni tofauti, hivyo kila mtu anapaswa kutazamwa kikamilifu kulingana na asili na tabia yake binafsi" ("Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). "… uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwandamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada za binadamu—unawekwa katika matendo kupitia maadili ya neno la Mungu. … Uhusiano unaofaa kati ya watu unaundwa juu ya msingi wa kumpa Mungu moyo wako; haufanikishwi kupitia jitihada za binadamu" ("Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika ushirika wa mtu, kinasema, "Tunapaswa kuwatendea kaka na dada zetu kama washiriki wa familia ya Mungu. Tunapaswa kuonyesha kukubali, uvumilivu na upendo. Hatupaswi kudanganya wala kuwa na chuki bila sababu, bali tumtendee kila mtu kwa usawa na kwa haki" ("Sifa Ambazo wale Wote Wanaomtumikia Mungu Wanapaswa Kumiliki na Jinsi ya Kumtumikia Mungu kulingana na dhamira Yake" katika Ushirikiano na Kuhubiri Kuhusu Kuingia katika maisha II). Kwa njia ya neno la Mungu na ushirika wa mwanadamu niligundua kuwa njia halisi ya kuwatendea wengine kwa haki ni kwa kupenda kile ambacho Mungu hupenda na kuchukia kile ambacho Mungu huchukia. Wale wanaotafuta ukweli, na kupenda ukweli na wanaoweza kutekeleza mapenzi ya Mungu ni kaka na dada zangu na ni wale ambao ninapaswa kuwapenda. Hata kama wamepotoka, wenye upinzani au wamefanyia uovu familia ya Mungu, mtu anapaswa bado kuwatendea kwa usahihi. Wanapaswa kupimwa kulingana na asili yao, upeo kamili wa matendo yao na hali ambayo walitenda kwayo. Hawapaswi kuhukumiwa kulingana na tukio moja pekee. Hii ni kanuni ambayo tunapaswa kuwatendea wengine kwa haki. Zaidi ya hayo, dada na kaka wanapaswa kutendewa kwa usawa na bila ubaguzi. Bila kujali kama tunampenda dada au kaka, tunapaswa kufuata kanuni hii. Kwa njia hii tu ndipo tutatenda kulingana na ukweli na mapenzi ya Mungu. Kupitia uzoefu huu, nilitambua kwamba kuwatendea watu kwa haki si rahisi kama nilivyofikiria. Katika siku za nyuma, nilidhani kuwa utendeaji bila haki ulimaanisha kuwa mkali na kuonyesha mtazamo mkatili kwa wengine. Nilidhani kuwa kuwatendea watu kwa moyo mkunjufu na wenye upendo kulikuwa kuwatendea haki. Leo, kwa njia ya neno la Mungu, nilitambua kwamba kwa kuchunguza tu hali kulingana na ukweli na kuwatendea watu kulingana na kanuni za ukweli ndipo tunawatendea watu kwa haki na kwa mujibu wa tabia zao halisi. Haijalishi kama tunachukua mtazamo mkali au mkunjufu, alimradi tufanye kulingana na ukweli, tutakuwa tukifuata nia ya Mungu. Vinginevyo tutapata chuki la Mungu na matendo yetu hayatakuwa na faida kwa mtu yeyote. Kwa njia hii, nilitambua kwamba sikuwa nikiwafanyia wengine haki wakati nilipokuwa nikifanya hayo "matendo mema" yote kulingana na tabia yangu ya asili. Badala yake, nilikuwa nimetenda kulingana na maoni yangu mwenyewe, mapendeleo na falsafa za kidunia. Nilikuwa tu nikilinda hadhi yangu kati ya watu na kukuza picha yangu mwenyewe. Niligundua pia kuwa ili kuwatendea watu kwa haki, mtu lazima awe na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa njia hii, bila kujali kama mtu anamsaidia kaka au dada kwa upendo, au kuwashughulikia, tendo la mtu kwao litakuwa na upendo wa Mungu kama msingi. Moyo wa mtu unaelekezwa kwa Mungu na kuweka katika kazi ya kutenda kweli, kufuata nia ya Mungu na kutimiza matakwa ya Mungu. Moyo uko tayari kukubali ukaguzi wa Mungu. Wakati ambapo upendo wa moyo haujatumiwa ili kudumisha mahusiano kati ya watu, hauna unafiki, uzuri wa uongo, nia au hisia za mwili. Upendo kama huo unawakilisha uhusiano wa kweli wa kiroho, kukubaliana kwa pande mbili kwa upendo. Ni katika kuwatendea watu kwa njia hii tu ndipo tunalingana na kanuni ya kweli na kuwafaidi watu wote.

Baadaye, nilisoma yafuatayo kutoka kwa ushirika mwingine, "Kuwatendea wengine kwa haki ni kanuni ambayo kila kiongozi anapaswa kumiliki. Ukiisaliti kanuni hii, hii inathibitisha kuwa wewe ni mkatili. ... Nyote mna nia mbaya na wa sifa ya chini ya maadili—haya huzungumzia mzizi wa suala hili. Siko tayari kuajiri watu kama hao" ("Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Neno la Mungu ‘Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako’ (II)" katika Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia katika Maisha VII). "Unaamuaje kama kiongozi amehitimu? Kwanza, anazungumza kwa njia ya haki? Pili, anawatendea watu kwa haki? Viwango hivi viwili ni muhimu kabisa. Ikiwa anaweza kukidhi viwango hivi viwili, kwa hakika yeye ni mtu mwenye uadilifu na aliyelingana na nia ya Mungu. Ikiwa pia ana ufahamu wa ukweli na anajua jinsi ya kutenda ukweli, unaweza kuwa na hakika kwamba atafanikiwa katika kazi yake" ("Muhtasari Kuhusu Kuwa Mtu Mwaminifu: Masuala Kumi Kila Mtu Anatakiwa Kutatua ili Kuwa Mwaminifu na Umuhimu wa Kuwa Mwaminifu" katika Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia katika Maisha V). Kupitia kusoma kwangu vifungu hivi nilikuja kuelewa kuwa kuwatendea wengine kwa haki ni kanuni ambayo kila kiongozi lazima aunge mkono. Ni wale tu wenye upole na wanaopenda ukweli wataokuwa na nia sahihi, kumweka Mungu mioyoni mwao, kuwapenda watu wa Mungu waliochaguliwa na kuwatendea watu kwa haki bila mapendeleo. Ni mtu wa aina hii tu anayeweza kuhudumu haki, kufuata na ukweli katika kila tendo lake, na kupata uvutiwaji wa wengine. Mtu wa aina hii kwa kawaida hufanikiwa katika kazi yake. Kwa mintarafu ya viongozi wakatili na wenye nia mbaya, mara nyingi wao hutenda kama afisa wa koti wenye kusaliti: Hawajishughulishi kabisa na kulinda maslahi ya familia ya Mungu au kuwatendea watu wa Mungu waliochaguliwa kwa moyo wenye upendo. Yote wanayofanya ni kuleta msiba kwa familia ya Mungu. Kama vile hawa wafanyao mabaya, wachochezi hawa wa ghadhabu ya watu, viongozi wa uongo na wapinga Kristo hawashindwi tu kufanya kazi yoyote halisi, lakini pia huwatendea kaka na dada zao kama watumishi wa chini wanaopaswa kutukanwa na kuteswa. Mara moja, wao hukandamiza, huwafundisha nidhamu, na hata kuwatenga, na kuwatoa nje kaka na dada zao. Wao huwakuza watu wanaojipendekeza walio chini huku wakizuia vipaji halisi. Wao hulichochea kanisa lote kuwa na ghasia. Chini ya ukali wa nguvu hizi za giza, kaka na dada hufanya kazi katika mateso na kukata tamaa. Sio tu kwamba hawapati ukuzaji na kuimarishwa, maisha yao yanaharibiwa na mioyo yao huumizwa sana. Kadiri nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kuogopa. Nilitambua kwamba kama viongozi hawawatendei wengine kwa haki, uharibifu ni mkubwa sana. Ikiwa mshiriki wa kawaida wa watu waliochaguliwa na Mungu hawezi kuwatendea wengine kwa haki, inaweza kusababisha ubaguzi na kuachana kwa pande mbili. Itaathiri tu hali ya watu wachache na kuingia katika kweli. Kwa upande mwingine, kama viongozi hawawezi kuwatendea watu kwa haki, huwadhuru na kuwaangamiza watu, huingilia moja kwa moja kazi ya familia ya Mungu na ni ya kudhuru kwa maslahi ya familia ya Mungu. Katika ushirika inasemwa, "Kufikia matarajio ya wajibu wa mtu kama kiongozi au mfanyakazi kwa watu waliochaguliwa na Mungu, unapaswa kuweka umuhimu katika kutatua masuala halisi ya wateule wa Mungu kwa mujibu wa ukweli wa neno la Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutatua kwa haki kila aina ya masuala ya kweli ambayo kanisa linazikabili, kuwatendea watu kwa haki, na kujiepusha na kukandamiza na kushikilia mamlaka juu ya watu waliochaguliwa. Hiki ndicho kiwango cha chini ambacho kinapaswa kufikiwa na viongozi na wafanyakazi katika kila ngazi za kanisa. Ikiwa mtu kweli anatafuta ukweli, vitendo vyake kwa hakika vitapata kibali na uungwaji mkono wa wateule wa Mungu. Mtu kwa kweli akiwa na uhalisi wa ukweli fulani, hatafichua kiburi chake kila wakati au kuchukua msimamo wa juu na wenye nguvu. Hakika hatazungumza kwa maneno ovyo ovyo, akiwa na utawala juu ya, kuwafunga, kuwazuia, au kuwashtaki wengine kwa nasibu. Badala yake, atawasaidia wateule wa Mungu kwa moyo wenye utulivu na wenye upendo. Atawashauri, kuwahimiza na kuwaongoza wengine katika ufahamu wao na utendaji wa ukweli. Kwa fadhili, atawasiliana ukweli kwa karibu ili kutatua masuala na kufikia matokeo. Hii ndiyo maana ya kiongozi mzuri au mfanyakazi. Siku hizi, kuna viongozi na wafanyakazi fulani ambao hawaonekani kuwa na uhalisi wa ukweli hata kidogo. Hata hivyo wanafurahia majivuno yao, kusema kwa upuuzi na hawana nafasi ya Mungu au watu wateule wa Mungu mioyoni mwao. Hawawahudumii wateule wa Mungu au kutimiza majukumu yao ili kulipiza upendo wa Mungu. Wanakanyaga maji hatari na tayari wamekanyaga njia ya mpinga Kristo. Wasipobadili njia zao, watafukuzwa na kuondolewa na Mungu." "Ni wale tu wanaompenda Mungu kweli watakaowatendea wateule wa Mungu kwa moyo wenye upendo. Huu ni ukweli. Wale ambao hawapendi wateule wa Mungu na wasioweza kuwatendea kwa haki na kwa mujibu wa kanuni za ukweli hakika hawampendi Mungu. Ni wale tu wanaompenda Mungu kweli wanaoweza kuwapenda wengine kama wanavyojipenda. Wale ambao hawana upendo kwa Mungu hawawezi kabisa kuwapenda wengine. Wale wanaowapenda wateule wa Mungu hakika wana uwezo wa kumpenda Mungu—hamna shaka" ("Unapaswa Kupata Uzoefu wa Kuingia kwa Uhalisi wa Ukweli wa Neno la Mungu Ili Uweze Kupata Ukamilifu wa Mungu" katika Mahubiri ya Ugavi wa Maisha). Nilipoona ushirika huu, moyo wangu ulihisi kuadibiwa. Niligundua kuwa nilikuwa tayari katika eneo lenye hatari, nikitembea katika njia ya mpinga Kristo. Nilitambua pia kuwa sikuwa na uwezo wa kuwatendea kaka na dada zangu kwa haki na kwa moyo wenye upendo. Hili halikuwa onyesho la mara moja la upotovu, bali ni ishara ya asili yangu mbaya na ya udanganyifu. Katika mzizi, shida yangu ilikuwa kwamba sikumpenda Mungu moyoni mwangu. Katika miaka yangu yote ya imani, nilikuwa bado sijafikia ukweli hata mdogo wa ukweli na bado sikuwaa nimeingia kwenye njia ya ukamilifu wa Mungu. Ni wale tu wanaompenda Mungu wanaoweza kufikiri juu ya nia Yake na kujua ni nini Anachojali na kuwa na wasiwasi nacho sana. Ni wale tu wanaompenda Mungu wanaohangaika juu ya wasiwasi Wake na kufikiria mawazo Yake, wakijitahidi kwa nguvu kamili kuwaleta wateule wa Mungu kwenye njia sahihi ya imani. Ni wapenzi wa Mungu tu wanaweza kufuata mfano wa Kristo katika kukuza moyo wa huruma na wenye kuonyesha masikitiko, katika kuvumilia wengine na moyo wa subira na upendo. Ni wale tu wanaompenda Mungu wanaoweza kufanya misheni ambayo Mungu amewaaminia; wanahisi wasiwasi isipokuwa pale ambapo wametumikia familia ya Mungu na kuwa hawawezi kukabiliana na Mungu mpaka watakapotatua masuala ya wateule wa Mungu. Kama ilivyo, wanafahamu kile ambacho kaka na dada zao hawana na kile wanachohitaji. Wanaweza kuhisi mateso ya kaka na dada na wanatoa vyote katika kurekebisha vitu vyote. Kwa upande wangu, sikuwa na upendo wa Mungu moyoni mwangu, na hivyo, sikuwa na uwezo wa kuwapenda kaka na dada zangu. Yote niliyopenda ilikuwa faida yangu binafsi. Yote niliyojali ilikuwa ni sifa yangu na hadhi yangu. Matokeo yake, niliwatendea kaka na dada zangu kwa dharau. Maslahi yangu mwenyewe yalipokuwa katika hatari, nilikwenda kwa kadiri ya kufundisha nidhamu, kukandamiza, kuadhibu na kulipiza kisasi kwa wengine ili kutoa hasira zangu. Niliona kwamba nilikuwa mtendaji maovu kabisa. Katika siku za nyuma, yaliyo hapo juu yalisimulia kupitia kuwasiliana kwa karibu kwamba kadiri cheo cha mtu kama kiongozi au mfanyakazi ulivyokuwa mkuu, ndivyo mtu anapaswa zaidi kuwa tayari kuwa mtu asiyejitanguliza. Kadiri kazi ya mtu ilivyo juu, ndivyo mtu anavyotakiwa kujitolea zaidi kama mhudumu kwa wateule wa Mungu. Hata hivyo, sikujitoa kama mtumishi tu, lakini, kama ofisa wa jeshi la joka kuu jekundu, niliwakubali na kuwaidhinisha wale waliokidhi maslahi yangu na kushiriki maoni yangu wakati nilikandamiza na kumtenga mtu yeyote ambaye niliona kuwa ni hatari. Kama mnyama mwovu, nilizunguka nikiwaangamiza wasiofuata kanuni wowote. Nilipotafakari nyuma juu ya hali yangu wakati huo, nilihisi hisia kubwa ya aibu. Hapo tu ndipo nilitambua jinsi asili yangu ilivyokuwa ya kudharauliwa. Ikiwa ningeendelea kutekeleza majukumu yangu katika tabia hii ya kishetani, hatimaye ningewekwa wazi na kutupwa nje kwa ajili ya maovu yangu yote.

Asante Mungu kwa zawadi Yake ya neema. Isingekuwa ufunuo wa Mungu, nisingeweza kamwe kutafakari juu ya matendo yangu mwenyewe na labda hata ningefanya vitendo zaidi vya uovu. Pia nilipitia upendo mkubwa na huruma ya Mungu. Mungu hakuniadhibu kwa kile nilichokifanya—hii inaashiria kwamba Mungu bado ananiokoa. Ninaweka nadhiri kutafuta ukweli kwa bidii, kutafakari juu ya makosa yangu ya zamani na kuweka jitihada mpya katika kuelewa asili yangu mwenyewe ili kufukua vipengele hivyo ambavyo havilingani na Mungu. Kupitia kupatiwa nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu na kuongozwa na hisia ya hatia katika dhamiri yangu, nilikuwa nimekwisha kuweka pembeni ubatili wangu, na kufungua vikwazo vya ushawishi mwovu wa Shetani. Dada zangu na mimi tulijiweka wazi bila ubaya, tulionyesha asili za kishetani za kila mmoja, na kufikia maelewano makuu wa kila mmoja wetu. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nimetoka gizani kwa ghafula na kuingia katika mwanga. Nilikuwa nimepitia furaha iliyokuja na kutenda ukweli na kumwaibisha Shetani. Nilihisi zaidi kuwa na utulivu, moyo wangu ulikuwa mwepesi zaidi, na sikuhisi hatia zaidi katika dhamiri yangu. Katika kuwasiliana kwa karibu na dada zangu, hakuna mtu aliyehisi kuzuiwa tena. Kila mtu angeweza kujiweka wazi bila kusita. Ghafula niliangua wimbo wa uzoefu wa maisha: "Katika Familia Ya Mungu, tunakutana na kila mmoja": " Katika familia ya Mungu, tunakutana kila mmoja, mkusanyiko wa watu wakimpenda Mungu. Bila upendeleo, kupendana kwa karibu, furaha na utamu ukijaza mioyo yetu. Jana tuliacha majuto na hatia; leo tunaelewana, tunaishi katika upendo wa Mungu. … Katika familia ya Mungu, tunakutana kila mmoja, lakini hivi karibuni tutatengana. Kulemewa na utendaji na mapenzi ya Mungu, tutaachana kwa ajili ya kazi ya Mungu. Tukikusanyika, tunacheka na kuongea kwa uchangamfu; tunapoondoka, tunatiana moyo. Upendo wa Mungu, kiini chetu cha kuwa waaminifu hadi mwisho. Kwa sababu ya siku nzuri za usoni, tutafanya chochote tuwezacho." Ilipofikia sehemu ambayo husema, Nilikabwa na machozi. Baada ya kuwa mateka wa asili potovu ya Shetani ndani yangu, mara moja nilizongwa na majuto makubwa. Ukweli kwamba mimi na dada zangu tungeweza kufikia mapatano ya pamoja leo katika uwepo wa upendo wa Mungu na kupendana kama familia ni uthibitisho wa kazi ya Mungu ndani yetu. Hukumu Yake na kuadibiwa na Yeye vilitushinda na kutuokoa kutoka kwa upotovu wetu mkubwa. Nilipofika kwenye sehemu inayosema, "lakini hivi karibuni tutatengana. Kulemewa na utendaji na mapenzi ya Mungu, tutaachana kwa ajili ya kazi ya Mungu," Moyo wangu uliomboleza na sikuweza kuimba tena. Nilihisi kujuta hata zaidi kwa kupotoshwa na Shetani, na, kwa nia mbaya, kumtukana na kuepuka dada yangu, na kumsababishia athari isiyorekebishika. Nilikuwa pia nimedakiza kazi ya familia ya Mungu.... Nilitumai tu kwamba tahakiki hii ya majuto ilijikita moyoni mwangu, na kwamba huzuni ingebadilika kuwa nguvu na uamuzi wa kuyakosoa makosa yaliyopita kupitia utimilifu wa majukumu yangu. Mara nilipokuwa nimepindua hali yangu, niliona kuwa kulikuwa na mengi ambayo ningeweza kujifunza kutoka kwa dada yangu. Yeye ni mpole sana na huchukua mzigo wa majukumu yake yote. Huu ni uwezo wake, maeneo ambayo yeye hufanya vizuri zaidi kunipiku. Nilifikiria kifungu kutoka kwa ushirika: Watu wanapounganishwa, wanaweza kugeuza uchafu kuwa dhahabu. Ninaapa kufanya mwanzo mpya na dada zangu, kutumia nguvu zao na kufidia udhaifu wao. Nitaingia katika ukweli pamoja nao, na kubeba mzigo wa wajibu wetu ili kukamilisha kazi maalum ya Mungu. Ninaamini kwamba ikiwa sisi ni wa moyo mmoja na akili moja na kuchanganya juhudi zetu, hata shida mbaya zaidi na maafa hazitatuzuia na tutapata baraka za Mungu katika kazi yote tunayofanya.

Kupitia uzoefu huu, sikuja tu kuelewa kweli ubinadamu na asili yangu, bali pia niliona jinsi tabia zangu zilivyoonyesha kuwa nilikuwa nikitembea katika njia mbaya. Nilitambua umuhimu mkubwa wa viongozi wa kumcha Mungu na kujiepusha na uovu, kutafuta ukweli na kutambua kazi ya Mungu, kuishi kwa upole, na kuwatendea watu kwa haki. Matendo haya yanaamua njia ambayo mtu huchukua katika huduma kwa Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, ninaapa kutafuta tu ukweli na kutenda kulingana na ukweli na kanuni ili nipate kulingana na Mungu hivi karibuni.

Iliyotangulia:Ni Upendo wa Mungu Tu Ulio Halisi

Inayofuata:Kujijua kwa Hakika kwa Kuuelewa Ukweli Tu

Unaweza Pia Kupenda