Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

94 Njoo Nyumbani, Mwanangu!

Ulikuwa wa kawaida na mnyofu; ulijawa na maadili.

Hiyo tabasamu nzuri ilinawiri usoni mwako.

Kijana ukilala unono mikononi mwa mama yako,

ujana ukimzingira kushoto na kulia.

Ulikuwa fahari na furaha ya mama yako,

na alikuwa mwamba wako wa kutegemea.

Sasa ujana huo umeponyoka pole pole na kutokomea,

na furaha yake ya kung’aa haiwezi kuonekana tena,

wala sauti yake tamu ya kuimba haisikiki tena.

Mwanangu, uko wapi? Huwezi kumsikia mamako akilia?

Njoo nyumbani, mwanangu! Njoo nyumbani, mwanangu!

Nani anayeweza kumwokoa mwanangu?

Nani anayeweza kumleta nyumbani?

Yuko mpweke sana, na asiyejiweza;

amepoteza umaasumu wake wa asili, na kutupa maadili yake mbali.

Anaonekana mwenye kuchoka sana, na sauti yake ni ya unyonge sana;

yeye si fahari ya mama yake tena,

na mama yake si mwamba wake wa kutegemea tena.

Mwanangu, ni nani aliyeiba moyo wako?

Ee! Mwanangu, ni nani aliyevunja ndoto zako?

Ni nani aliyekutoa mikononi mwa mama yako?

Mwanangu, uko wapi? Huwezi kumsikia mamako akilia?

Njoo nyumbani, mwanangu! Njoo nyumbani, mwanangu!

Nani anayeweza kumwokoa mwanangu?

Nani anayeweza kumleta nyumbani?

Njoo nyumbani, mwanangu! Mama yako anakusubiri.

Iliyotangulia:Kuenda Nyumbani

Inayofuata:Maisha ya Mwanadamu Mpya

Maudhui Yanayohusiana