15. Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Maneno Husika ya Mungu:

Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo pia matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikiwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo katika mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na hali ikiwa mbaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. … Sio hivyo kwa watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na nidhamu na lawama ya Roho Mtakatifu hayatumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi ndani ya mwili, wanaishi ndani ya akili zao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu sembuse ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu hawana uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Maneno na matendo yao mengi yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini, si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kukutana pamoja kwa watu hawa si linguine ila dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mkutano wa wale wote walio miongoni mwao unaweza tu kuitwa mkutano mkubwa wa watu wa dini, na bali hauwezi kuitwa kanisa. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinaonekana chenye kunuka dini, wanachoishi kwa kudhihirisha katika maisha yao kinaonekana kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, sembuse kustahiki kupokea nidhamu au nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyo na uhai, na funza wasio na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu, sembuse kujua kazi yote ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni watu wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini!

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikiwa, katika imani yao, watu wanachukulia ukweli kuwa seti ya kanuni ya kufuatwa, basi si imani yao ina uwezekano wa kugeuka kuwa taratibu za dini? Na tofauti kati ya taratibu hizi za dini na Ukristo ni ipi? Wanaweza kuwa wa kina na wenye maendeleo zaidi katika jinsi wanavyosema mambo, lakini iwapo imani yao imegeuka tu kuwa seti ya kanuni na aina ya utaratibu, basi hilo halimaanishi kwamba imegeuka kuwa Ukristo? (Ndiyo, linamaanisha hivyo.) Kuna tofauti kati ya mafundisho ya kale na mapya, lakini ikiwa mafundisho hayo ni aina ya nadharia tu na yamekuwa tu aina ya utaratibu, aina ya mafundisho kwa watu—na, vilevile, ikiwa hawawezi kupata ukweli kutoka kwayo au kuingia katika uhalisi wa ukweli—basi si imani yao ni sawa na Ukristo? Kimsingi, je, si huu ni Ukristo? (Ndiyo, ni Ukristo.) Kwa hivyo katika tabia yenu na utendaji wa wajibu wenu, ni katika vitu vipi ambavyo mna maoni na hali ambazo ni sawa na ama zinazofanana na zile za waumini wa Ukristo? (Katika kufuata kanuni, na katika kujihami kwa maneno na mafundisho. ) (Katika kuzingatia sura ya kuwa watu wa dini na kuonyesha tabia nzuri, na kuwa wanaomcha Mungu na wanyenyekevu.) Mnatafuta kuwa na tabia nzuri kwa nje, kufanya kila mwezalo kujionyesha kuwa na sura ya dini, kuzungumza kanuni za dini, kusema mambo ambayo ni sahihi kidini, kufanya mambo yanayokubalika kiasi katika fikira na mawazo ya binadamu, na kujifanya kuwa waadilifu. Mnazungumza maneno na kanuni kwa kujigamba, mkiwafundisha watu kufanya mema, wawe watu waadilifu, na kuelewa ukweli; mnajidai kuwa watu wa dini, na mnaonyesha hali ya juujuu ya dini katika kila kitu msemacho na kufanya. Hata hivyo, kwa vitendo, hamjawahi kutafuta ukweli; punde tu mnapokabiliwa na tatizo, mnatenda kulingana na mapenzi ya binadamu, mkimtupa Mungu kando. Hamjawahi kutenda kulingana na kanuni za ukweli, hamjawahi kuelewa kinachozungumziwa katika ukweli, yale yaliyo mapenzi ya Mungu, viwango anavyohitaji kutoka kwa mwanadamu ni vipi—hamjawahi kuyachukulia mambo haya kwa uzito ama kujishughulisha nayo. Je, haya matendo ya nje na hali hizi za ndani za watu—yaani, imani kama hii—zinajumuisha kumcha Mungu na kuepuka uovu? Ikiwa hakuna uhusiano kati ya imani ya watu na ufuatiliaji wao wa ukweli, basi wanamwamini Mungu au la? Bila kujali idadi ya miaka ambayo watu wasio na uhusiano na kufuatilia ukweli wanaweza kumwamini, je, wanaweza kupata uchaji Mungu wa kweli na halisi na kuepuka uovu au la? (Hawawezi.) Kwa hivyo tabia ya nje ya watu kama hao ni ipi? Wanaweza kuitembea njia ya aina ipi? (Njia ya Mafarisayo) Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa na nini? Je, si ni kwa maneno na nadharia? Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa, wakivalia maneno na nadharia ili kujifanya kama Mafarisayo zaidi, wa dini zaidi, kama watu ambao hudhaniwa kwamba humtumikia Mungu zaidi? Asili ya mbinu hizi zote ni ipi hasa? Je, ni kumwabudu Mungu? Ni imani ya kweli Kwake? (La, siyo.) Kwa hivyo wanafanya nini? Wanamdanganya Mungu; wanapitia tu hatua za mchakato fulani, na kujihusisha katika taratibu za dini. Wanapeperusha bendera ya imani na kufanya kaida za dini, wakijaribu kumdanganya Mungu ili kufikia lengo lao la kubarikiwa. Hawamwabudu Mungu hata kidogo. Mwishoni, je, si kundi kama hilo la watu litaishia tu kama wale walio ndani ya kanisa ambao hudhaniwa kwamba wanamtumikia Mungu, na ambao hudhaniwa kwamba wanamwamini na kumfuata Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Je, Mungu huwaita nini wale waliomwamini Yehova? Uyahudi. Waligeuka kuwa aina ya kundi la dini. Na Mungu huwafafanuaje wale wanaomwamini Yesu? (Ukristo.) Machoni pa Mungu, Uyahudi na Ukristo ni vikundi vya dini. Kwa nini Mungu anawafafanua hivyo? Miongoni mwa wale wote ambao ni washiriki wa mashirika haya ya dini yaliyofafanuliwa na Mungu, je, kuna wowote wanaomcha Mungu na kuepukana na uovu, kufanya mapenzi ya Mungu, na kufuata njia ya Mungu? (La.) Hili limekuwa dhahiri. Machoni pa Mungu, wale wote wanaomfuata Mungu kwa maneno tu wanaweza kuwa wale ambao Mungu amewatambua kuwa waumini? Je, wote wana uhusiano na Mungu? Je, wote wanaweza kuwa walengwa wa wokovu wa Mungu? (La.) Hivyo siku itakuja ambapo mtashushwa na kuwa kile ambacho Mungu anaona kama kundi la dini? (Inawezekana.) Kushushwa hadi kiwango cha kundi la kidini, hiyo inaonekana isiyowazika. Watu wakiwa sehemu ya kikundi cha dini machoni pa Mungu, je, wataokolewa na Yeye? Je wao ni wa nyumba ya Mungu? (La, sio.) Kwa hivyo jaribu kufupisha: Watu hawa ambao wanamwamini Mungu wa kweli kwa maneno tu lakini ambao Mungu anawaamini wao kuwa sehemu ya kikundi cha dini—wanaitembea njia gani? Je, inaweza kusemekana kwamba watu hawa wanaitembea njia ya kupeperusha bendera ya imani bila kamwe kufuata njia Yake, ya kumwamini Mungu lakini kutomwabudu, na badala yake kumtelekeza? Yaani, wanaitembea njia ya kumwamini Mungu lakini kutofuata njia ya Mungu na kumwacha Mungu; njia yao ni ile ambayo wanamwamini Mungi lakini wamwabudu Shetani, wanamwabudu ibilisi, wanajaribu kutekeleza usimamizi wao wenyewe, na kujaribu kuanzisha ufalme wao wenyewe. Je, hiki ni kiini cha hilo? Je, watu kama hawa wana uhusiano wowote na mpango wa Mungu wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu? (La.) Bila kujali ni watu wangapi wanamwamini Mungu, mara tu imani zao zinapofafanuliwa na Mungu kama dini au kikundi, basi Mungu ameamua kuwa hawawezi kuokolewa. Kwa nini nasema hivi? Katika kundi au umati wa watu ambao hawana kazi na mwongozo wa Mungu na ambao hawamwabudu hata kidogo, wanamwabudu nani? Wanamfuata nani? Katika umbo na jina wanamfuata mtu, lakini ni nani wanayemfuata hasa? Katika mioyo yao wanamtambua Mungu, lakini kwa kweli, wao huathiriwa na utawala wa hila, mipangilio na udhibiti wa binadamu. Wanamfuata Shetani, ibilisi; wanafuata nguvu ambazo zina uhasama kwa Mungu, ambazo ni maadui wa Mungu. Je, Mungu anaweza kuokoa kundi kama hili la watu? (La.) Kwa nini? Je, wana uwezo wa kutubu? (La.) Wao hupeperusha bendera ya imani, wakitekeleza shughuli za binadamu, wakitekeleza usimamizi wao wenyewe, na wanakwenda kinyume na mpango wa Mungu wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Matokeo yao ya mwisho ni kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; Mungu hawezi kamwe kuwaokoa watu hawa, hawawezi kamwe kutubu, tayari wamekamatwa na Shetani—wamo mikononi mwa Shetani kabisa. … Ikiwa hawawezi kufuata njia ya Mungu na hawawezi kuitembea njia ya wokovu, matokeo yao ya mwisho yatakuwa yapi? Matokeo yao ya mwisho yatakuwa sawa na wale wanaoamini Ukristo na Uyahudi; hakutakuwa na tofauti. Hii ni tabia ya Mungu ya haki! Bila kujali umeyasikia mahubiri mangapi, na umeelewa ukweli kiasi gani, ikiwa hatimaye bado unawafuata watu na kumfuata Shetani, na hatimaye, bado huwezi kufuata njia ya Mungu na huwezi kumcha Mungu na kuepukana na uovu, basi watu kama hawa watachukiwa na kukataliwa na Mungu. Kadiri ionekanavyo, watu hawa ambao wanachukiwa na kukataliwa na Mungu wanaweza kuzungumza mengi kuhusu maandiko na mafundisho, wamekuja kuelewa ukweli mwingi, na ilhali bado hawawezi kumwabudu Mungu; hawawezi kumcha Mungu na kuepukana na uovu, na hawawezi kuwa na utiifu mkamilifu kwa Mungu. Machoni pa Mungu, Mungu anawafafanua kama dini, kama kikundi tu cha wanadamu, genge la wanadamu, na kama makao ya Shetani. Wanajulikana kwa jumla kama kikundi cha Shetani, na wanadharauliwa kabisa na Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Tunamaanisha nini tunapoongea kuhusu “kumfuata Mungu”? Tunaongea kuhusu kupitia kazi ya Mungu na kukubali ukweli. Iwapo hukubali ukweli, iwapo hupitii kazi ya Mungu, basi hutapitia hukumu na adabu ya Mungu, ambayo inamaanisha humfuati Mungu. Je, tunawaita vipi wale ambao hawamfuati Mungu lakini ambao humwamini Mungu? Tunawaita waumini wa dini. Je, imani ya aina hii ya wale wanaomwamini Mungu haiko ndani ya dunia ya dini? Wanamwamini Mungu aliye mbinguni pekee, lakini hawamfuati Mungu, hawapitii kazi ya Mungu, wanashikilia tu Biblia yao, wanashikilia tu wanaloita andiko. Kila siku, wanasoma aya na kusali kwa njia ya dini, na inakoma hapo. Haina uhusiano wowote na maisha yao wenyewe, na jinsi wanavyoishi. Wanafanya tu chochote wanachofikiri wanapaswa kukifanya. Hii ndiyo inajulikana kama kuwa muumini wa dini. Hawakubali kazi ya Mungu, wala hawapitii kazi ya Mungu. Kwa hivyo, imani yao iko hapo tu kujaza uwazi ulioko katika roho zao, kuridhisha mioyo yao inayoteseka, na kutafuta aina fulani ya riziki. Je, watu wenye imani kama hii wataweza kuwa na ushuhuda mkubwa, mzuri kwa Mungu? Hakika hawataongea kuhusu kuwa na ushuhuda, kwa sababu hawajadili gharama, wala matumizi, wala utiifu, wala uzima. Kwa sababu ya hili, hawashuhudii. Kwa hivyo, wakati wowote wanapoteswa, kuna wachache sana kati yao ambao wanaweza kusimama imara. Wakati maisha yao yako hatarini, wote wanamsaliti Mungu. Pengine wengine wenu mtakanusha kile ambacho nimesema karibuni, pengine mtaniambia: “Katika Enzi ya Neema na katika Enzi ya Sheria, je, hakukuwa na mashahidi wengi?” Hilo si makosa. Hao mashahidi walikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, wao pia walikuwa wafuasi wa Mungu katika enzi hizo, kama tu tulivyo leo. Hawakuwa sehemu ya waumini wa dini. Wale waliopitia kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria walikuwa watu waliomfuata Mungu katika Enzi ya Sheria. Wale waliopitia kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema walikuwa watu waliomfuata Mungu katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Ufalme, wale kati yetu ambao hupitia kazi ya Mungu katika siku za mwisho pia ni wafuasi wa Mungu. Hata hivyo, sasa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho akitekeleza kazi Yake binafsi, kwa waumini ambao bado wako katika Enzi ya Neema na wale katika Enzi ya Sheria, imani zao zimegeuka kuwa imani za dini.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Kwanza, lazima tuelewe jinsi ambavyo jamii za kidini zilivyoundwa na tofauti kati ya kanisa na dini. Ni muhimu sana kuyafafanua masuala haya. Tunaona kutoka kwenye Biblia kwamba wakati wa kila hatua ya kazi ya Mungu, watu wateule wa Mungu waliongozwa na kuchungwa na wale ambao Mungu mwenyewe aliwaweka na kuwateua. Kwa mfano, wakati wa Enzi ya Sheria, Mungu alimtumia Musa kuwaongoza moja kwa moja watu wa Israeli, na Akamfanya Musa aunde mfumo wa kikuhani. Baada ya kazi ya Musa kukamilika hakukuwa na watu zaidi duniani ambao waliteuliwa moja kwa moja na Mungu kuwaongoza Waisraeli. Makuhani wakaanza kuchaguliwa na watu. Huu ni usuli wa uundaji wa jamii ya kidini ya dini ya Kiyahudi. Kuanzia hapo, mfumo wa kikuhani katika Uyahudi umekuwa ukiundwa kwa chaguzi kutoka katika jamii za kidini. Mara nyingi zaidi, jamii za kidini zilizidi kuwa potovu hatua kwa hatua kwa sababu makuhani ambao si sahihi walichaguliwa. Wakati ambapo Bwana Yesu mwenye mwili alionekana na kufanya kazi wakati wa Enzi ya Neema, jamii za kidini zilikuwa zimeanguka kwa kiwango kwamba zilipinga na kumlaani Kristo na kuwa maadui wa Mungu. Huu ni ukweli ambao kila mtu wakati huo aliweza kushuhudia. Bwana Yesu alipokuja duniani kufanya kazi Yake ya ukombozi, Yeye binafsi aliwachagua mitume kumi na wawili. Roho Mtakatifu pia alianza kufanya kazi wakati ule, na alikuwa pamoja na mitume wa Bwana Yesu. Katika wakati huu kusanyiko la wale waliokuwepo duniani ambao waliikubali kazi ya Bwana Yesu waliitwa kanisa, na walichungwa kikamilifu na watu walioteuliwa na Mungu, kwa maneno mengine, watu waliotumiwa na Roho Mtakatifu. Katika wakati huu, kanisa la kweli liliundwa, na hiki ndicho chanzo cha kanisa. Zaidi ya miaka thelathini baada ya kufufuka na kupaa kwa Bwana Yesu kwenda mbinguni, wengi wa mitume kumi na wawili walikuwa wamekufa kwa ajili ya imani, na kanisa duniani halikuchungwa tena na mitume waliokuwa wameteuliwa moja kwa moja na Bwana Yesu. Kwa hiyo, aina mbalimbali za vikundi vya kidini viliundwa. Huu ndio usuli wa uundwaji wa jamii za kidini wakati wa Enzi ya Neema. Baada ya hapo, bila kujali iwapo watu walikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu au la, ilimradi waliweza kuzungumza kuhusu Biblia, wangeweza kuliongoza kanisa. Ilimradi walikuwa na karama, watu wangekubaliana nao na kuwafuata. Wangeweza kufanya kazi na kuhubiri kama walivyopenda bila mtu yeyote kuwazuia, hivyo madhebebu mbalimbali yalianza kuundwa. Kanisa ni nini, na dini ni nini? Tunaweza kusema kwamba makundi yanayoongozwa na kuchungwa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu ni makanisa, huku yale yanayoongozwa na kuchungwa na watu ambao hawatumiwi na Roho Mtakatifu ni dini. Huu ndio mgawanyiko rahisi kabisa na wa kweli kabisa. Makanisa ya kweli yana kazi ya Roho Mtakatifu Kazi ya Roho Mtakatifu kwa nadra sana huonekana katika dini, na hata ikionekana, ipo tu katika watu wachache ambao kweli wanamwamini Mungu na wanafuatilia ukweli. Hii ndiyo tofauti kati ya kanisa na dini. Kwa makanisa, ni jambo la muhimu sana kama wachungaji wanashughulikiwa na kutumiwa na Roho Mtakatifu au la. Ikiwa mchugaji ni mtu ambaye anafuatilia ukweli na anatembea kwenye njia sahihi, basi kazi ya Roho Mtakatifu ipo. Ikiwa mchugaji si mtu ambaye anafuatilia ukweli na anatembea kwenye njia ya Mafarisayo, basi kazi ya Roho Mtakatifu haipo. Ilimradi watu wanaweza kutofautisha kati ya wachugaji wa kweli na wa uongo, basi wanaweza kulipata kanisa la kweli.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia: 14. Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Inayofuata: 16. Mpinga Kristo ni nini? Mpinga Kristo anaweza kutambuliwaje?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Iwapo Kristo kweli ni Mwana wa Mungu au ni Mungu Mwenyewe

Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho.

3. Kwa nini kila hatua mpya ya kazi ya Mungu hukabiliwa na uasi mkali na shutuma ya ulimwengu wa kidini, na chanzo cha jambo hili ni nini

Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu.

3. Tofauti kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya Neema na katika Enzi ya Ufalme

Katika mikutano maalum ya zamani au mikutano mikuu iliyokuwa katika sehemu mbalimbali, ni kipengele kimoja tu cha vitendo kilichozungumziwa. Vitendo kama hivyo ni vile vilivyotiwa katika vitendo katika Enzi ya Neema na hapakuwa na mfanano wowote na ufahamu wa Mungu kwani maono ya Enzi ya Neema yalikuwa tu maono ya kusulubiwa kwa Yesu, na hapakuwa na maono ya juu zaidi. Mwanadamu hakuhitajika kujua zaidi ya kazi Yake ya ukombozi wa mwanadamu kupitia kusulubiwa, na kwa hivyo katika Enzi ya Neema hapakuwa na maono mengine ya kufahamiwa na mwanadamu. Kwa njia hii, mwanadamu alikuwa na ufahamu mdogo sana wa Mungu na mbali na upendo na huruma za Yesu, kulikuwa na vitu vichache tu vya mwanadamu kuweka katika vitendo, vitu ambavyo vilikuwa tofauti na hali ya leo.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki