Sura ya 58. Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu

Katika kukifahamu kiini cha Kristo, kipengele kimoja ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya kupata mwili Kwake na binadamu; aidha, watu ambao wanafahamu kiini cha Kristo wana uwezo zaidi kuwa hakika kuhusu Mungu kuwa mwili na uwezo zaidi wa kuamini kuwa Yeye kweli Yupo, kuwa Yeye si nabii, mtume, wala mwenye kufunua, na hasa si mtu mdogo aliyetumwa hapa na Mungu; bali Yeye ni mwenye mwili, Yeye ni Kristo, Naye ni Mungu Mwenyewe. Hata kama mwili ulikuwa sehemu miongoni mwa watu, Alikuwa mtu wa kawaida na kiini cha Uungu. Kiini cha Kristo kinaeleweka kwa njia ya kuelewa tabia ya Mungu, kupitia kazi Yake, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yake. Matokeo ya kuelewa kiini cha kupata mwili ni kuwa kunawaruhusuwatu kupambanua ukweli kwamba Mungu hasa ni kuwa mwili, na kwamba kupata mwili huku kwa kweli ni Mungu. Ni kwa njia hii pekee ndiyo watu wanaweza kuanzisha imani ya kweli katika Mungu na kufikia kutii kwa kweli na pendo la kweli. Ni wakati tu unapofikia matokeo haya ndipo yatathibitisha kuwa una ufahamu wa kiini cha Mungu.

Sasa, watu hawana ufahamu wa Kristo, wao tu husoma maneno ya Mungu na kukiri kuwa kuna Roho, wakifikiri kwamba[a] ikiwa maneno ni sahihi, basi Roho bila shaka ni wa kwel. Wanadharau mwili na hawajui ni nini asili ya mwili au jinsi mwili na Roho vinahusiana. Watu wengi wanaamini kuwa mwili ni wa kuonyesha maneno pekee, Yeye hutumika tu katika kuzungumza na kufanya kazi. Hiyo ndiyo huduma Yake. Yeye huongea Anaposukumwa, na baada ya kuongea, Hana lolote la kufanya, kama mrija wa sauti. Kama hivi ndivyo ilivyo, basi wao hawatambui kupata mwili au Kristo; wao wanamtambua Yeye kama nabii tu. Baadhi ya watu hata hufikiri: "Kristo ni mtu. Bila kujali ni nini kiini cha kupata mwili, au ni tabia ipi Anayoonyesha, Yeye hana uwezo wa kuwakilisha Mungu Aliye mbinguni kabisa na hana uwezo wa kuwakilisha kabisa Bwana wa uumbaji ambaye anadhibit vitu vyote ulimwenguni. Kwa kuwa Yeye ni kupata mwili kwa Mungu na ni Mungu mbinguni ambaye huja chini katika dunia, mbona Hajui jinsi mbingu na dunia na vitu vyote vilivyoumbwa Anapoulizwa? Kwa nini hakuna miujiza yoyote isiyo ya kawaida? Kama Ana mamlaka, basi mbona Asiangamize joka kuu jekundu? "Watu wanaosema haya hawaelewi vitu vya kiroho, hawelewi kupata mwili kuna maana gani, nao hasa hawaelewi wigo wa usimamizi wa kazi wakati wa kupata mwili, kusudio la wokovu ni nini, ni nini inaonyeshwa, na ni nini watu wanapaswa kuelewa. Kiini cha kupata mwili ni kiini cha Mungu; Yeye anaweza kuwakilisha Mungu kufanya kitu chochote, Yeye ni Mungu Mwenyewe na Anaweza kufanya kitu chochote Anachotamani. Hata hivyo, kwa njia ya kuchukua mwili wakati huu, Yeye hutekeleza hatua ya mwisho ya kazi ndani ya masafa ya usimamizi; haihusiki na utawala wa kila kitu au kuwa na mamlaka juu ya falme mbalimbali, haihusishi vitu hivyo, kwa hiyo, unachopaswa kuelewa ni mambo ambayo watu wanaweza kuwasiliana nayo na mambo ambayo watu wanaweza kuelewa katika hatua hii ya kazi. Yaani, wao wanapaswa kuelewa kiini cha hatua hii ya kazi, na maonyesho ya kile Mungu anacho na maana yake na tabia Yake. Je, kile ambacho Kristo Anaonyesha ni kiini cha Mungu? Je, ni tabia ya Mungu? Bila shaka ni hivyo. Je, ni kamili? Hivi sasa Nitawambia, si kamili; ni kile ambacho tu watu wanaweza kuona kwa macho yao wenyewe, kile ambacho watu wanaweza kuwasiliana nacho, na kile ambacho watu wanaweza kuelewa katika mioyo yao katika kipindi cha kupata mwili; si kamili, ni kazi tu ambayo inapaswa kufanyika kulingana na mpango wa Mungu.

Kwa kutoa mfano ambao watu wanaweza kuelewa kwa urahisi kuhusu kupata mwili: Mungu alijigawanya Mwenyewe na Akakuja chini duniani. Je, Roho wa Mungu Yu kwingineko? Ndiyo. Yeye hutawala kila kitu ulimwenguni, kuna Mungu mmoja tu aliye na mamlaka; Mungu ni Mwenyezi, na sasa Yeye huja chini katika dunia-Akiwa mwili, tofauti na jinsi watu hudhania kuwa Yeye huchukua mwili na kufanya tu kazi duniani, na hajali kuhusu kazi nyingine yoyote. Hapo zamani NImewauliza baadhi ya watu: Je, bado kuna Mungu mbinguni na ilhali sasa Mungu amekuja chini duniani Akiwa mwili? Wao hutafakari kwa kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi hakuna Mungu mbinguni. Wao wanakosa tena. Mungu hutawala kila kitu katika ulimwengu, Yeye ni Roho; Yeye sasa huja duniani, lakini Yeye bado Ana mamlaka ya mambo ya mbinguni na pia Anafanya kazi duniani. Je Roho Wake huondoka mara kwa mara? Baadhi ya watu hutafakari: Labda inampasa kuondoka, labda wakati mwingine mwili hajui chochote; wakati mwili Wake unaishi kwa kawaida, basi Roho Anaondoka, na unapokuja wakati wa kuzungumza, basi Roho Anarudi tena; wakati wa kulala, labda Roho Anashughulika na mambo mengine, na wakati wa kuamka, Roho Anarudi tena, kuzungumza na kufanya kazi pamoja na mwili. Ikiwa hakuna kazi, basi wakati wa kula, Roho Anapata muda wa kwenda na kufanya kitu kingine, na mwili unaweza kuishi kama binadamu wa kawaida. Watu wengi wanatafakari kwa njia hii. Kuna hata baadhi ya watu ambao wana wasiwasi: Sijui jinsi pesa za Mungu zimetengwa, zinaweza kutolewa kwa faragha kwa watu wengine kutumia? Mawazo ya watu kwa kweli ni magumu Watu hawa wanahodhi mawazo maovu; wanawezaje kufuatilia ukweli? Katika yote, kuelewa Mungu—iwe ni kuelewa kiini cha kupata mwili, au kuelewa tabia ya Mungu-hakuna iliyo rahisi sana; yaani, unajaribu tu kuelewa mambo ambayo una uwezo wa kuyapitia na mambo ambayo una uwezo wa kuyagusa wakati wa muda wa kazi ya Mungu kuwa mwili. Usifikiri kwa pupa mambo ambayo huwezi kukutana nayo. Kwa mfano: Baada ya mwili wa Mungu kuondoka, ni umbo upi Atatokea nao ili kufanya kazi tena? Je, bado Atakuja chini duniani na kukutana nasi? Kama kuwa mwili kwa kweli kulitaka kudhihirisha miujiza sasa, na kuuliza Baba aliye mbinguni na kuuliza Roho, je Roho Angeweza kufanya kitu? Baadhi ya watu pengine wamekuwa na mawazo kuhusu masuala haya. Je, Yesu hakulaani mti ule wakati huo? Mti ulewa mtini ulikauka wakati huo. Mungu wa leo ana uwezo wa kufikia kiwango hiki? Baadhi ya watu husema: "Kupata mwili kwa Mungu ni kawaida na wa vitendo, na Hafanyi mambo yasiyo ya kawaida." Baadhi ya watu husema: "Yeye huwa hafanyi mambo yasiyo ya kawaida? Kama Angekuwa na kiini cha Mungu, basi ni kwa nini maneno Yake ni bure?” Kwa sasa, idadi kubwa ya watu wote huzingatia mambo haya ya nje, mambo haya kimsingi hayahusishi kiini cha Kristo, na kuelewa mambo haya kwa kweli ni bure; kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji kuelewa kwako, na wakati utakapokuja wa wewe kuelewa, utaelewa, haijalishi kama unaelewa ama huelewi mambo haya, hayana hata athari kidogo juu ya imani za watu katika kupata mwili kwa Mungu, imani yao kwa Kristo, au kufuata kwao kwa Kristo. Unaweza kujua, lakini bado hutaongezeka katika imani hata kidogo. Ni nini ambacho watu wamepata kutoka kwa manabii kudhihirisha miujiza katika siku za zamani?

Pasipo kujali wingi wa miujiza manabii wale waliweza kutenda, wao si Mungu. Kama Ana kiini cha Mungu na bado Hafanyi miujiza, Yeye bado ni Mungu; kama Yeye Ana kiini cha Mungu, lakini Hadhihirishi miujiza, haimaanishi kwamba Yeye hawezi kuyadhihirisha. Kuna faida kwa nyinyi kutafuta kuelewa kiini cha Mungu sasa; ndiyo tu njia sahihi ya kumwamini Mungu. Mnapaswa kujua kwamba katika kipindi cha kazi wakati wa kupata mwili, kile ambacho watu wanaweza kuwasiliana nacho na kuona zaidi ni kile Mungu anacho na maana yake, pamoja na kiini Chake na tabia Yake Hii ni nafasi ya kipekee ya kumjua Mungu. Ufahamu wa matendo ya Mungu na tabia ambayo watu walinena kuhusu hapo kale si rahisi kupata, kwa sababu watu hawakuwa na uwezo wa kuwasiliana na Mungu.Awali, Musa alielewa Yehova na kuona baadhi ya matendo Yake. Je, alikuwa na ufahamu wa vitendo kiasi kipi? Je, ni kubwa kuliko ile ya watu siku hizi? Je, ni ya vitendo zaidi ya ile ya watu siku hizi? Bila shaka hapana. Wakati Yehova Alikuwa Anafanya kazi wakati huo, matendo Yake yalidhihirishwa kwa wingi katika Israeli; watu wengi waliona Yehova Akidhihirisha miujiza na hata kuna watu ambao waliona mgongo wa Yehova. Watu wengi pia waliwaona malaika, lakini hatimaye, ni watu wangapi walimjua Mungu? Wachache sana! Kwa hakika hapakuwa na watu waliomjua Mungu kwa kweli. Ni watu tu wa siku za mwisho ambao wanamwelewa Mungu sana kwa kupitia kazi Yake katika kipindi cha wakati wa kupata mwili Kwake, kwa sababu watu wanaambiwa kila kitu ana kwa ana: Azma ya kazi ambayo mimi Hufanya, mapenzi Yangu, mtazamo Wangu kwa binadamu, na hali na kiini ni ya binadamu aliyepotoka. Ni kwa kupitia tu mambo haya ambapo watu wanaweza kuona kuwa daima Mungu Amekuwa Mungu wa aina hii, mapenzi Yake daima yamekuwa ya njia hii kwa binanadamu, Mungu siku zote Amekuwa na tabia ya aina hii na daima matendo Yake yamekuwa ya ajabu kiasi hiki; hekima Yake daima imekuwa ya kina kiasi hiki, huruma Yake kwa binadamu daima imekuwa halisi kiasi hiki, na wakati huu imejidhihirisha kweli. Yeye daima hukuruhusu kuwa na uzoefu wa upendo Wake na stahamala kwa bianadamu kwa kweli hayana mipaka. Mapenzi Yake ya kuokoa watu ni dhahiri katika kazi Yake na kwa maneno Yake, na Yeye Anawaruhusu watu kuyapitia kwa kweli. Kwa hivyo, kuelewa kwako kwa kiini cha kupata mwili ni kutoka wakati wa kupata mwili. Ila kwa kipindi cha muda huu, kuelewa kwako hakutakuwa kwa vitendo. Baada ya kazi Yake kukamilika na kuondoka, kama wewe utasema kwamba Nitaendelea kuzoea kazi ya Mungu, hiyo haitakuwa halisi kama ilivyo sasa, kwa sababu sasa macho yako yanaweza kuona, na unaweza kweli kuihisi; zaidi ya hayo, daima imefanyika ana kwa ana kwa njia hii na hatua kwa hatua watu wamepata kuyapitia kibinafsi. Kile Petro alipitia wakati huo haikuwa halisi kama yale watu wanapitia siku hizi. Awali, katika kipindi kile Yesu alifanya kazi katika nchi ya Yudea, Petro alifuata na kupitia baadhi ya mambo, lakini ilikuwa nafiki na ukomavu wake ulikuwa mdogo wakati huo, hata hivyo, baada ya Yesu kuondoka, alitafakari kwa makini na kuonja na alikuwa na uwezo wa kuhisi baadhi ya mambo. Wakati huo, Yesu pia alionyesha baadhi ya kile Mungu anacho na alicho, wema wa Mungu, rehema ya Mungu, wokovu wa Mungu kwa binadamu, stahamala ya Mungu isiyo na mipaka na neema kwa binadamu, na watu kwa wakati huo walikuwa na uwezo wa kupitia baadhi ya vitu hivi. Baadaye, mambo ambayo watu walipitia hayakuwa na kina kama yale watu hao waliyoyaonja wakati huo. Aidha, katika kipindi ambacho watu walikuwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu na walifuata mapenzi ya Mungu katika sala, kile walipitia hakikuwa yakini. Wakati mwingine, hawakuwa wanakihisi kwa dhahiri na hakuna ambaye angethubutu kuthibitisha kama walielewa kwa usahihi au la. Mwishowe, Petro alienda gerezani na watu hao wakamwokoa, lakini kwa kweli, nia ya Yesu wakati huo ilikuwa kuruhusu asulubiwe kama wosia wa mwisho. Wakati maisha ilifika kikomo, Mungu alimruhusu kutoa ushuhuda kwa njia hii na kuwa na hatima nzuri. Hii ilikuwa njia ya Petro. Awali, wakati Petro alifika mwisho wa njia yake, hakuelewa nia ya kweli ya Yesu. Ni baada tu ya Yesu kumwambia ndipo alijua nia ya Yesu. Kwa hivyo, ukitaka kuelewa kiini cha Mungu, wakati unaofaa zaidi wa wewe kuelewa ni wakati wa kupata mwili Kwake. Unaweza kuona na kuhisi, unaweza kusikiliza na kusikia, na unaweza kuhisi kwa undani. Wakati kazi katika kipindi cha kupata mwili utakapokwisha, kama utaendelea kupitia jinsi Roho Mtakatifu anafanya kazi, na utafakari ya nyuma, haitakuwa ya kina sana, na kuelewa kwako kutakuwa duni hata hivyo. Wakati huo, Yeye Atakasa tu tabia potovu ya watu, na baada ya kutakasa, watu wanaweza kuelewa ukweli zaidi na kutumia kweli ambazo wamepata kama msingi wa maisha yao na kujibadilisha ndani wenyewe. Bila kujali jinsi umpendavyo Mungu, kumwelewa kwako kumhusu Yeye wakati utakapokuja hutakuwa na maendeleo mengi, ambayo si ya manufaa kama kuelewa Mungu wakati wa kupata mwili. Katika kipindi cha kupata mwili, watu wengi huona, lakini hawaelewi, wao husikia, lakini hawajui; Mungu Anapenda na kustahimili watu sana, lakini wao hawawezi kuihisi; watu wote hawajali; wao watakuwa tu na baadhi ya kuelewa na kuanza kutembea kwenye alama sahihi wakati kazi ya Mungu itakapoisha.

Ni nini kiini cha Kristo? Kiini cha Kristo ni upendo kwa binadamu; kuhusiana na wale wanaomfuata, ni upendo usio na mpaka. Kama Hana upendo au huruma, basi watu wasingekuwa na uwezo wa kumfuata hadi wakati huu. Baadhi ya watu husema: "Basi je, bado Mungu ni mwenye haki?" Ndiyo! Ni sahihi kwamba Yeye bado ni mwenye haki, lakini kwa mtazamo wa tabia Yake, hali Yake ya kuwa mwenye haki ni chuki kwa upotovu na uovu wa binadamu. Je, kama Angekuwa tu mwenye haki bila upendo? Je, kama upendo usingeweza kushinda haki? Basi ingesemekana kuwa binadamu amekwisha. Kwa hiyo, Ninanena wazi na nyinyi, yaani, katika kazi Mungu Anayofanyia binadamu katika kipindi cha kupata mwili Kwake, kiini Chake dhahiri na maarufu zaidi ni upendo; ni stahamala isiyo na kipimo. Kama haikuwa upendo bali Mungu kuwaangamiza watu vile mnavyofikiria; kwa kunena uharibifu, watu waliangamizwa, na kwa kunena chuki kwa watu, watu waliadhibiwa, kulaaniwa, kuhukumiwa, na kkuadibiwa, basi hiyo itakuwa kali sana! Kama Angekuwa na hasira kwa watu, watu wangekuwa na hofu na kutetemeka na wasingewezea kusimama mbele ya macho ya Mungu .... Hii ni njia moja tu ya kuonyesha tabia ya Mungu, na mwishowe, azma Yake bado ni wokovu. Upendo Wake unadhihirika kupitia ufichuzi wote wa tabia Yake. Tafakari juu ya hili, wakati wa kuwa mwili, jambo linalofichuliwa zaidi kwa watu ni upendo. Uvumilivu ni nini? Uvumilivu ni kuwa na huruma kwa sababu kuna upendo ndani, na azma Yake bado ni kuwaokoa watu. Mungu anaweza kuwa na huruma juu ya watu kwa sababu Yeye Ana upendo. Kama vile kuna pendo la kweli kati ya mume na mke, hawaangali upungufu wa yule mwingine na hatia. Kama wangechochewa kiasi cha kuwa na hasira, wao bado wangeweza kuwa na subira. Kila kitu kimeimarishwa juu ya msingi wa upendo. Je, kama Angekuwa wa chuki? Basi mtazamo Yake usingekuwa jinsi ilivyo, kujionyesha Kwake kusingekuwa jinsi ilivyo, na matokeo yasingekuwa jinsi yalivyo.

Kama Mungu tu angekuwa na chuki na hasira, na kungekuwa na hukumu na kurudi tu, na kusingekuwa na upendo ndani yake, basi hali isingekuwa muonavyo sasa na nyinyi watu msingekuwa katika hali nzuri. Je, Angeweza kuwapa ukweli? Mngekuwa mmelaaniwa baada ya kurudi na kuhukumiwa, na kisha mngepitia msiba mkubwa, kama vile kupatwa na ugonjwa, kuendeleza vidonda, kuendeleza upele, kupoteza nywele, kupata kichaa, kuwa kipofu, kuwa ya midomo chakavu, kupoteza masikio na kupoteza visigino, nk mngekuwa mmekwisha kabisa. Hata kama msingekufa mara moja, mngekuwa wagonjwa, vilema, wendawazimu, na vipofu, mngekanyagwa na roho mbovu na mizuka wachafu sana.... Msingekuwa katika hali yenu ya sasa. Kwa hivyo, Nasema kuwa mmefurahia upendo mwingi na mmefurahia stahamala nyingi, huruma na wema; Hata hivyo, watu huchukulia haya kama kawaida, na wanafikiri: Mungu anapaswa kuwa namna hii kwa watu; Mungu pia ni mwenye haki na ghadhabu, na sisi tumeyafurahia kwa wingi!Je kweli umeyafurahia? Kama ungekuwa kweli umeyafurahia, basi ungekuwa umekwisha. Ni vipi binadamu huyu bado angekuwepo sasa? Chuki ya Mungu, ghadhabu, na haki yameonyeshwa yote kwa msingi wa kuokoa kundi hili la watu. Upendo na huruma pamoja na subira kubwa mno pia yako ndani ya tabia hizi.Hii chuki ina hisia ya kutokuwa na chaguo lingine, ni kwa pamoja na shaka isiyokuwa na mpaka na kutazamia kwa binadamu! Chuki ya Mungu imelengwa kwa upotovu wa binadamu, imelengwa ukaidi wa binadamu na dhambi; ni ya upande mmoja, na imeimarishwa juu ya msingi wa upendo. Ni wakati tu kuna upendo ndipo chuki huwepo. Chuki ya Mungu kuelekea kwa binadamu ni tofauti na chuki Yake kuelekea kwa Shetani, kwa sababu Mungu anaokoa watu, na Yeye hamwokoi Shetani. Tabia ya Mungu ya haki imeishi kuwa, Yeye siku zote Amekuwa na ghadhabu, haki na hukumu. Hayakuja tu yalipoonyeshwa kwa binadamu. Kwa kweli, Mungu alikuwa na tabia hii kabla ya binadamu kuiona. Ni wakati tu watu walipoipitia ndipo walipotambua-haki ya Mungu imeishi kuwa namna hii. Kwa kweli, bila kujali kama Yeye ni mwenye haki au Mwenye utukufu, au Yeye Huonyesha hasira kali, Yeye huokoa watu na hutekeleza mpango Wake wa usimamizi wotekwa sababu ya upendo. Baadhi ya watu husema:"Basi ni kiasi kipi cha upendo? "Si kiasi cha upendo Alionao, badala yake Ana asilimia mia moja ya upendo. Kama Angekuwa na upendo wowote chini ya hii, basi binadamu asingeokolewa. Mungu ametoa upendo Wake wote kwa watu. Kwa nini Yeyeanachukua mwili? Imesemekana awali kuwa Mungu hakusita kulipa gharama yote ili kumwokoa binadamu. Kupata mwili ni pamoja na upendo kamili, na hii inawaruhusu nyinyi kuona kuwa binadamu huasi dhidi ya Mungu mno, washafika katika hali ambayo hawawezi kuokolewa; kwa hivyo, Mungu hakuwa na njia nyingine ila kuchukua mwili na kujitoa Mwenyewe kwa binadamu.Mungu ametoa upendo Wake wote.Kama Asingempenda binadamu, kwa hakika Asingechukua mwili. Mungu anaweza kugurumisha radi na moja kwa moja kuonyesha utukufu Wake na ghadhabu na binadamu angeanguka juu ya ardhi; hakungekuwa na haja ya Yeye kuchukua mwili na kutarajia juhudi kubwa sana na kulipa gharama kubwa kama hiyo na kupata fedheha kubwa namna ile. Huu ni mfano ulio wazi. Ni afadhali Yeye Mwenyewe kuteseka, kufedheshwa, kutelekezwa, na kudhulumiwa ili kuokoa binadamu. Yeye bado Angeafadhalishakuja kwa mazingira ya aina hii ili kumwokoa binadamu. Je, huu sio upendo? Kama tu kuna haki na chuki isiyo na kikomo kwa watu, basi Yeye asingechukuwa mwili kufanya kazi, na Mungu angengoja hadi binadamu apotoke kabisa na kumwangamiza, na yote yangekwisha. Ni kwa sababu Mungu anampenda binadamu na kwa sababu Yeye Ana upendo mkubwa kwa binadamu kwamba Yeye Aliuchukua mwili ili kuokoa binadamu aliye mpotovu mno. Wakati wanapitia hukumu ya Mungu na kurudi, watu wengi huja kuelewa asili yao na kusema:"Imekwisha, siwezi kukuokolewa." Ni wakati ambapo unafikiri kwamba huwezi kuokolewa ndipo unaweza kujua kwamba Mungu kwa kweli Ana subira na upendo! Bila upendo wa Mungu, watu wanaweza kufanya nini? Asili ya binadamu ni ya njia hii, lakini Mungu bado Anawanenea nyinyi, na Anajibu bila kuchelewa kila wakati mnauliza swali. Yeye Ana hofu sana kwamba hamwezi kuelewa, Yeye Ana hofu sana kwamba watu watatembea kwenye njia zilizopotoka na kutembea kwa zaidi. Je, bado huelewi jinsi gani Mungu Ana upendo mkubwa kwenu!

Sasa hivi, kuna watu wengi ambao wanaangalia kwa makini. Kwa nini mwili Umechelewa na Hujaondoka baada ya Yeye kumaliza kazi? Je, kuna hatua nyingine katika kazi? Kwa nini Yeye hakimbilii kufanya hatua ifuatayo ya kazi? Bila shaka kuna maana katika hili. Baada ya Yeye kunena mambo mengi, ni matokeo gani halisi yanayopatikana ndani ya watu? Watu husikiliza na kukumbuka tu katika mioyo yao, lakini hawajaingia ndani sana. Mabadiliko yao pia si dhahiri kabisa. Kuhusu hali yenu ya sasa, hamna udhahiri kuhusu kweli nyingi na kuingia katika uhalisikimsingi hakuwezekani. Unieleze: Mungu kuwa mwili Amenena maneno mengi katika kipindi cha kazi Yake, na ni nini azma Yake? Nini matokeo ya mwisho? Kama Yeye sasa Angeanza kufanya hatua ifuatayo ya kazi na kuwatoa watu hawa na wala asingewajali, basi kazi hii ingeachwa bila kumalizika. Kazi katika kipindi cha kupata mwili lazima iwe na hatua mbili kamili. Kwa mfano, Yesu Alikuja katika Enzi ya Neema, na kutoka kuzaliwa Kwake hadi kusulubiwa Kwake na kupaa mbinguni, ilikuwa jumla ya miaka thelathini na tatu na nusu. Kulingana na maisha ya kiumbe ya kawaida, haukuwa muda mrefu; Hata hivyo, kulingana na muda Mungu alikuwa duniani, hakikuwa kipindi kifupi! Miaka hiyo thelathini na tatu na nusu ilikuwa ya mateso makali! Mungu si mtu na Alikuja chini duniani kushirikiana na binadamu wapotovu kwa miaka thelathini na tatu na nusu; hili lilikuwa jambo la kuumiza. Bila kujali kama watu walikuwa wazuri au wabaya Kwake, au kama Alikuwa na mahali pa kuishi-hayo yote pembeni-hata kama mwili Wake hukuteseka uchungu mkubwa, kuishi pamoja na binadamu ni jambo la kuumiza, kwa sababu hawakuwa wa aina moja! Ili kutoa mfano: Kama mtu angeishi na nguruwe siku nzima, basi baada ya muda, bila ya shaka angeudhika sana, kwa kuwa si wa aina moja; watu na nguruwe hawana lugha ya pamoja, hivyo ni jinsi gani hiyo isiwe ya kuumiza! Mume na mke ambao si wa moyo moja na akili watachukiana wanapoishi pamoja. Mungu kupata mwili duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu ni jambo la kuumiza sana Lenyewe, na zaidi ya hayo, hakuna mtu mmoja angemwelewa. Watu hata kufikiri: "Mungu kuwa mwili Anaweza kufanya lolote Atakalo na kusema chochote Anachotaka. Watu wengi sana humfuata. Ni maumivu gani Anayo? Ni kwamba yeye hana mahali pa kuishi, mwili Wake unakabiliwa na baadhi ya maumivu, na Yeye Huchukua baadhi ya maumivu, lakini hii haihesabiki kama kuwa na machungu sana! "Inaweza kusemekana kuwa maumivu haya yanaweza kuchukuliwa na kuvumiliwa na watu. Kupata mwili si jambo la pekee, na Yeye pia Ana uwezo wa kuvumilia, hivyo basi haihesabiki kama mateso makubwa. Cha muhimu zaidi, maumivu yanayomkabili ni kuwa Anaishi na watu wapotovu sana, na Hupitia kila aina ya kejeli, shutuma, hukumu, na lawama. Yeye pia hufuatwa na shetani na Anakataliwa na kupingwa na jamii za kidini. Hakuna mtu anayeweza fidia kwa ajili ya madhara haya katika moyo Wake! Haya ni mambo ya kuumiza. Yeye Huokoa binadamu mpotovu kwa njia ya uvumilivu uliokithiri; Anawapenda watu walio na moyo uliovilia. Hii ni kazi ya kuumiza zaidi. Upinzani mkali wa wanadamu, lawama na masingizio, mashtaka ya uongo, mateso na uwindaji wao na uchinjaji yanasababisha mwili wa Mungu kukumbwa na hatari kubwa katika kufanya kazi hii. Yeye huteseka na maumivu haya, bali nani anaweza kumwelewa na kumfariji? Binadamu ana tu shauku kidogo na malalamiko, au anamshughulikia kwa mwelekeo hasi na kumpuuza. Itakuwaje Asiteseke kwa sababu ya mambo haya? Maumivu yanayokabili moyo Wake ni makubwa mno. Je, faida tu ya nyenzo Anayofurahia yanaweza kufidia madhara binadamu humfanyia? Je, unafikiri kuwa kula vizuri na kuvaa vizuri ni furaha? Mtazamo huu ni wenye mzaha mno! Bwana Yesu alifanya kazi duniani na kuishi kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Ni tu baada ya Yeye kusulubiwa, kufa na kufufuliwa na kuonekana kwa binadamu kwa siku arobaini ndipo Yeye Alifarijika, hivyo basi kumaliza miaka ya kuumia ya kuishi na binadamu. Hata hivyo, moyo wa Mungu daima umepata aina hii ya maumivu kutokana na kuwa nawasiwasi na hatima ya binadamu. Maumivu haya hayawezi kueleweka na mtu yeyote, wala hayawezi kustahimiliwa na mtu yeyote. Bwana Yesu alisulubiwa na Akachukua dhambi za watu wote. Damu Yake yenye thamani huwapa watu msingi wa kuokolewa; Alitumia damu Yake yenye thamani ili kukomboa binadamu kutoka kwa mnaso wa Shetani; ni baada tu ya Yeye kumaliza kazi yote ya ukombozi ndipo maisha Yake ya maumivu duniani yalikamilika. Baada ya kazi yote kukamilika, Hakuchelewa hata siku moja, na Alijitokeza tu kwa watu, kuwaruhusu wote kujua kwamba Mungu kweli Amekamilisha ukombozi, Alimaliza kazi, na kumaliza mpango wa kupata mwili Kwake. Kama kungekuwa na hata kazi kidogo ambayo hakuwa Amekamilisha, basi Asingeondoka. Katika Enzi ya Neema, Yesu mara nyingi alisema: wakati bado haujawadia. "Wakati bado" ina maana kuwa kazi bado hujafika hatima yake; hio ni kusema, kazi ya kupata mwili si kama vile watu hufikiria ambapo Yeye huzunguka Akizungumza na kutazama hali ya maisha katika kanisa, na kisha Hana la kufanya baada ya kusema kila kitu kinachohitajika kusemwa. Baada ya mwili wa kuwa mwili kutimiza kazi Yake, baada ya kusema maneno mengi, Yeye bado lazima Asubiri matokeo ya mwisho, ni lazima Asubiri athari ya wa maneno yake ili kuona ufanano wa binadamu baada ya wao kupokea wokovu. Je, si hii ni ya asili na sahihi? Ameweka juhudi Zake zote katika kazi hii. Je, Yeye Angeweza tu kuacha kila kitu nyuma? Ni lazima Aendelee kutazama hadi mwisho na Asubiri hadi baada ya jambo hilo kuzaa matunda kabla ya kupumzika Kwake na kuendelea mbele kwa hatua ifuatayo ya kazi; ni Mungu Mwenyewe tu ndiye Anaweza kukamilisha mpango wa usimamizi Wake na kazi. Jinsi binadamu atakuwa hatimaye, jinsi watu ambao wameokolewa watakuwa hatimaye, ni watu wangapi watakubaliana na mapenzi Yake, kiasi cha watu wanaompenda kwa kweli, jinsi watu wanaomfuata watakuwa hatimaye, ni watu wangapi wanamjua kwa kweli, watu wangapi wanampenda, watu wangapi wanajiweka wakfu Kwake, ni watu wangapi wanamuabudu kwa kweli—je, mambo haya yote hayafai yawe na matokeo? Si kama watu wanavyodhani: Wakati Mungu Amemaliza kufanya kazi duniani, Anapaswa kupumzika na kungoja na kufurahia! Ni ajabu kiasi gani! Ni kutojali kwa kiasi gani! Nakwambia: Sio kutojali pekee, kusubiri ndiko hakuvumiliki zaidi! Baadhi ya watu hawaelewi; wanafikiri: Kama Mungu alimaliza kazi Yake na Hana mengine ya kusema, basi Roho Wake ameondoka? Baadhi ya watu husema: "Baada ya Mungu kuwa mwili kutimiza kazi na Amemaliza kusema, je, ni sawa kama Yeye hasubiri?” Si sawa. Ana upeo wa kufanya kazi ndani yake katika kipindi cha kupata mwili. Sio kama watu wanavyowaza ambapo hakuna lingine limebaki la kufanya baada ya kazi kukamilika na Roho pekee Anatazama. Sio hivyo. Pia kuna baadhi ya mambo ambayo yanahitaji msaada wa mwili na ambayo mwili lazima ushughulikie. Watu hawawezi jibadili kwa ajili Yake; huu ndio umuhimu ya Mungu kuwa mwili kufanya kazi. Je, unaelewa hii? Hapo awali Nimenena kwa hasira na baadhi ya watu, Nikisema: "Kushirikiana na nyinyikunaumiza sana. " Baadhi ya watu wamesema: "Kama Wewe huko radhi kuwa nasi, basi mbona bado Unasubiri" Huu ni upendo! Bila upendo, Yeye Angekuwa na uwezo wa kusubiri hadi sasa? Wakati mwingine Yeye Ana hasira na Ananena baadhi ya maneno kwa hasira, lakini Hafanyi kazi kwa upungufu wowote wala Hakosi hatua yoyote ya kazi. Hazuili kazi yoyote Anayopaswa kufanya au maneno yoyote Anafaa kusema. Yeye hufanya kile ambacho Anatakiwa kufanya na kusema kile Anapaswa kusema. Baadhi ya watu husema: "Kwa nini Mungu Ananena machache zaidi leo, tofauti na wakati Alinena mengi hapo zamani?” Kwa sababu hatua za kazi tayari zimekamilika, na katika hatua hii ya mwisho ni kusubiri tu. Mimi Nafanya tu baadhi ya kazi ya nyongeza na Nimehangaika ya kutosha. Mbona mwili wangu daima haufanyi vizuri katika kipindi hiki cha mwisho? Inaweza kusemwa kuwa kuna umuhimu katika hili. Ili kuchukua baadhi ya maumivu ya binadamu na magonjwa, mwili wa kuwa mwili unakabiliwa na baadhi ya maumivu. Hii kwa kweli ni sehemu ya hatua. Kazi ambayo haipaswi kufanywa inazuiliwa kupitia magonjwa ya mwili na hairuhusiwi kufanyika. Wakati utakapokuja, mwili lazima uteseke baadhi ya maumivu. Kusingekuwa na vizuizi vingi, basi daima kungekuwa na mengi kiasi ambayo Yeye Angependa kusema kwa binadamu, na Yeye angependa kuwasaidia zaidi kidogo kwa sababu Yeye anafanya kazi ya wokovu. Kama mazingira ya miaka hii miwili ungeruhusu, au kama mwili Wangu ungelikuwa na nguvu zaidi kuliko ilivyo sasa, basi Mimi Ningeenda kila mahali na kutembelea makanisa yote. Hata hivyo, mwili wangu haujiwezi na hauruhusu, basi Naweza kupumzika tu, na wakati jambo kubwa linatokea, yote yanayohitajika kufanywa ni kusema maneno machache na kutoa baadhi ya mwelekeo. Tangu mwanzo, yote ambayo kaziya kupata mwili yamefichua ni upendo, kiini cha kazi Yake ni upendo; Yeye Amejitolea kwa yote, kila kitu Chake kwa binanadamu.

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili yameacha "wakifikiri kwamba."

Iliyotangulia: Sura ya 56. Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Inayofuata: Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki