Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 55. Usieleze Kile Mungu Alicho Nacho na Kile Alicho

Kazi na matamshi ya Mungu ya miaka michache iliyopita yote yamerekodiwa kimsingi katika kitabu, Neno Laonekana katika Mwili. Baadhi ya maneno katika kitabu hiki ni ya kinabii na yanatabiri vile enzi za baadaye zitakavyokuwa. Unabii kwa kweli ni mfumo wa jumla, na zaidi ya nusu ya kitabu kinajadili kuingia kwa mwanadamu kwa maisha, kinaweka wazi utu, na kinazungumzia kuhusu kumwelewa Mungu na tabia Yake. Na kuhusu enzi gani, enzi ngapi na ufalme wa aina gani mwanadamu ataingia baadaye, je, hakuna mipango makini, hakuna marejeleo maalum na zaidi hakuna vipindi vya muda? Yaani, enzi za baadaye hazikuhusu. Sasa hivi sio wakati na tuko mbali sana nayo. Hutaweza kuelewa hata Nikikuambia. Aidha, watu hawahitaji kuelewa mambo haya sasa. Wanahitaji tu kuelewa maneno ambayo yanafichua utu sasa hivi. Kitu kikitokea ambacho kitawafanya watu waulize tena kuhusu mafumbo, unaweza kujibu kama ifuatavyo: “Mambo haya hayahusiani sana na kubadilisha tabia ya maisha ya mwanadamu. Elewa mengi yake kama uwezavyo, lakini kama kweli huyaelewi, yafikirie jinsi yoyote utakavyo!”

Zamani, kulikuwa na unabii uliosemwa, kama vile Ufalme wa Milenia, Mungu na mwanadamu wakiingia katika pumziko pamoja, na pia kuhusu Enzi ya Neno. Maneno ya unabii yote yanahusu wakati ujao karibuni; yale ambayo hayajatajwa ni mambo ambayo yako mbali sana. Hamhitaji kusoma mambo ambayo yako mbali; yale ambayo hamfai kuyajua hamtaambiwa; yale ambayo mnafaa kuyajua ni ukweli mzima utokao kwa Mungu—kwa mfano, tabia ya Mungu inayoonyeshwa kwa ajili ya mwanadamu, kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho ambayo yanafichuliwa na maneno ya Mungu, hukumu, kuadibu, na ufunuo wa utu, na pia mwelekeo kwa maisha unaopewa watu, kwa sababu kazi ya kuwaokoa wanadamu inajumuisha vitu hivi kama kiini wake. Sababu ya Mungu kusema mambo haya Anapofanya kazi ya kusimamia ubinadamu ni hasa kuwashinda na kuwaokoa watu, na kubadilisha tabia ya watu. Kwa sasa Enzi ya Neno ni enzi ya ukweli, ni enzi ya ukweli kumshinda na kumwokoa mwanadamu; kutakuwa na maneno zaidi baadaye—kuna mengi ambayo bado hayajasemwa. Watu wengine wanafikiri kuwa maneno haya ni maneno yote ambayo yameonyeshwa na Mungu—huu ni ufafanuzi uliopotoka sana, kwa sababu kazi ya Enzi ya Neno imepata tu mwanzo wake katika Uchina, lakini kutakuwa na maneno zaidi baada ya Mungu kuonekana hadharani na kufanya kazi baadaye. Jinsi Enzi ya Ufalme itakavyokuwa, namna ya hatima watakayoingia binadamu, kitakachofanyika wanapoingia katika hatima hiyo, jinsi maisha yatakavyokuwa kwa binadamu wakati huo, kiwango ambacho silika ya binadamu inaweza kufika, aina ya uongozi na aina ya utoaji wa vitu kwa siku za mbele utakaohitajika, na kadhalika, haya yote yamejumuishwa katika kazi ya Enzi ya Neno. Ujumulishaji wote wa Mungu sio jinsi unavyofikiria katika kitabu cha Neno Laonekana katika Mwili. Je, maonyesho ya tabia ya Mungu, na kazi ya Mungu, vinaweza kuwa rahisi jinsi unavyoifikiria kuwa? Ujumulishaji wote wa Mungu, kuwa kila mahali, kudura, na ukuu sio maneno matupu—kama maneno katika kitabu hiki yanawakilisha kila kitu cha Mungu, na kama maneno haya yanakomesha usimamizi wote wa Mungu, basi umemtazama Mungu kwa njia ndogo sana; je, huku si kumweleza Mungu tena? Unapaswa kujua kuwa maneno haya ni sehemu ndogo sana ya Mungu mjumuisha yote. Jamii yote ya kidini imemweleza Mungu katika Biblia. Na leo mnamueleza Yeye pia? Je, hamjui kuwa kumweleza Mungu ni kumdharau Mungu? Kuwa huku ni kumhukumu na kumkufuru Mungu?

Sasa hivi, watu wengi wanafikiria kwa jinsi hii: Kile ambacho Mungu Amesema katika siku za mwisho yote yako kwenye kitabu, Neno Laonekana katika Mwili, hakuna maneno zaidi kutoka kwa Mungu; hayo ni yote ambayo Mungu Amesema. Ni makosa makubwa kufikiria hivi! Kitabu, Neno Laonekana katika Mwili, kinaonyesha tu kuwa kazi ya ushindi katika Uchina imefika mwisho, na kuletwa katika kikomo, lakini hii haimaanishi kuwa usimamizi wote wa Mungu umeisha. Wakati kazi ya ulimwengu mzima itakapoisha, tunaweza tu kusema kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita umeisha; wakati mpango wa usimamizi utakapofika mwisho, je, si Mungu bado Atakuwepo, na watu bado, watakuwepo katika ulimwengu huu? Bora tu maisha yapo, bora tu ubinadamu upo, basi usimamizi wa Mungu utakuwa unaendelea. Kama tu katika kiwanda, kwa sababu tu bidhaa moja imemaliza kipindi chake cha uzalishaji haimaanishi kuwa kiwanda kitafungwa; ili mradi kiwanda kinahitajika kuwepo, shughuli za kiwanda zitakuwepo bado; kiwanda kitahitaji kutoa bidhaa mpya, lakini kwa njia nyingine. Wakati ambapo mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita utakapokamilika, almradi ubinadamu bado upo, kuishi, maisha, na ulimwengu huu, basi Mungu atakuwa bado Anasimamia yote, lakini hautaitwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita tena. Kile tunachoita kwa sasa usimamizi wa Mungu pengine kitajulikana kwa jina lingine baadaye; hayo yatakuwa maisha mengine kwa binadamu na Mungu; Mungu hawezi bado kutumia maneno ya sasa kuwaongoza watu, kwani maneno haya yanafaa tu kwa kipindi hiki cha wakati. Kwa hivyo, usieleze kazi ya Mungu katika wakati wowote. Wengine wanasema kuwa Mungu anawapa watu maneno haya tu, na sio kitu kingine; kuwa Mungu anaweza kusema tu maneno haya—huku pia ni kumfungia Mungu katika kiwango fulani. Hii ni sawa tu na, sasa hivi, katika Enzi ya Ufalme, kutumia maneno kutoka kwa enzi ya Yesu—je, hiyo itafaa? Baadhi ya maneno yatatumika, na mengine yanafaa kuondolewa, kwa hivyo huwezi kusema kuwa maneno ya Mungu hayawezi kamwe kuharibiwa. Je, watu hueleza vitu bila kusita? Katika baadhi ya maeneo, wanafanya hivyo. Pengine siku moja utasoma Neno Laonekana katika Mwili kama watu wanavyosoma Biblia leo, bila kuenda kwa mwendo sawa na nyayo ya Mungu. Sasa ndio wakati mzuri wa kusoma Neno Laonekana katika Mwili; kusoma baadaye itakuwa kama kuangalia kalenda nzee, kwa sababu kutakuwa na kitu kipya cha kuchukua nafasi ya kilicho kizee katika wakati huo. Mahitaji ya watu yanatolewa na kuendelezwa kulingana na kazi ya Mungu. Katika wakati huo, utu, na silika na sifa ambazo watu wanafaa kuwa nazo vitakuwa vimebadilika kwa kiasi fulani; baada ya dunia hii kubadilika, mahitaji ya binadamu yatakuwa tofauti. Wengine wanauliza: “Mungu ataongea baadaye?” Wengine watafikia hitimisho kuwa “Mungu hatazungumza, kwa sababu kazi Yake imeisha, na wakati kazi ya Enzi ya Neno imekapokamilika, hakuna kitu kingine kitakachosemwa, na maneno mengine yoyote yatakuwa uongo. Je, hili pia sio kosa? Ni rahisi kwa binadamu kufanya kosa la kumweleza Mungu; watu ni wepesi wa kushikilia yaliyopita, na kumwekea Mungu mipaka. Kwa dhahiri hawamjui Mungu, na bado kwa utukutu wanaieleza kazi ya Mungu. Asili yao ni yenye kiburi sana! Kila wakati watu wanapenda kushikilia dhana za zamani, wanaweka vitu vya siku zilizopita mioyoni yao, na kuvitumia kama mtaji wao, wakiwa na kiburi na wenye makuu, na kufikiri kuwa wanaelewa kila kitu, na kuwa na uchungu wa kuieleza kazi ya Mungu. Katika hili, je, hawatimilizi hukumu kwa Mungu? Kwa kuongeza, watu hawaijali kazi mpya ya Mungu, ambayo inaonyesha kuwa ni vigumu kwao kukubali mambo mapya, ilhali bado kwa upofu wanamweleza Mungu; watu wamejawa na kiburi hata hawana busara, hawamsikilizi yeyote, na hata hawayakubali maneno ya Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo asili ya mwanadamu: wenye kiburi kabisa na wa kujidai, na bila utii hata kidogo. Walipomhukumu Yesu, Mafarisayo walikuwa hivi: Hata kama Ulikuwa sahihi, bado singekufuata Wewe—Yehova tu ndiye Mungu wa kweli. Leo, je, hakuna watu wanaosema hivi: “Ni Kristo? Singemfuata Yeye hata kama Angekuwa kweli ni Kristo!” Je, watu kama hao wapo? Ndio, kuna watu wengi wa kidini kama hawa. Hii inaonyesha kuwa tabia ya mwanadamu imepotoka sana, kuwa amepita kiwango cha wokovu.

Kati ya watakatifu tangu mwanzo hadi mwisho wa enzi, Musa na Petro tu ndio waliomjua Mungu kwa kweli, na walisifiwa na Mungu; hata hivyo, wangeweza kumwelewa Mungu? Walichoshika ni kidogo sana. Wao wenyewe hawakuthubutu kusema kuwa walimjua Mungu. Wale wanaomjua Mungu kwa kweli hawamwelezi, kwa sababu wanagundua kuwa Mungu hapimiki na ni wa kupita kisai. Wale wasiomjua Mungu ni wale ambao ni wepesi wa kumweleza na kile Alicho nacho na kile Alicho, wamejawa na fikira juu ya Mungu, wanatoa dhana kwa urahisi kuhusu kila kitu ambacho Mungu Amefanya. Hivyo, wale wanaoamini kuwa wanamjua Mungu ni wale wanaopinga Mungu zaidi, na ndio watu walio wenye hatari kubwa zaidi.

Iliyotangulia:Sura ya 54. Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja

Inayofuata:Sura ya 56. Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?