Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Je, mnaona kwa dhahiri njia ya imani yenu kwa Mungu na njia yenu ya kufuata ukweli? Imani katika Mungu kweli ni nini? Je, mmetosheka baada ya kupitia shida kidogo? Watu wengine hufikiri kwamba baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na ushughulikiwaji au baada ya kufichua hali yao ya kweli, wamemaliza na matokeo yao yameonekana. Wengi wa watu hawawezi kuona suala hili kwa dhahiri, na wao wote husimamishwa hapo, bila kujua jinsi ya kuitembea njia iliyo mbele. Kwa ujumla, wasipopitia ushughulikiwaji na upogolewaji au hawana vikwazo vyovyote, watahisi kama kutafuta ukweli wakati wakiamini katika Mungu, na watahisi kwamba wanapaswa kuyatosheleza mapenzi ya Mungu. Lakini mara tu wanapokuwa na shida kidogo na matatizo fulani yanajitokeza, asili zao za kusaliti zinafunuliwa, na kuwafanya waonekane wenye karaha hasa, na baadaye, watazihisi pia asili zao hasa ni zenye karaha. Mwishowe, wanajiamulia matokeo wenyewe: Imefika kikomo, mimi nimekwisha, si nimemalizwa kwa kufanya jambo hili? Hakika Mungu hataniokoa. Kuna watu wengi ambao wako katika hali ya aina hii; hata mnaweza kusema kuwa kila mtu yuko jinsi hii. Kwa nini watu wanaweza kujieleza wenyewe kwa njia hii? Inathibitisha kwamba watu hawaelewi nia ya Mungu kuwaokoa. Kuwa ukishughulikiwa mara moja tu husababisha uende muda mrefu bila kufuata ukweli; kufanya kosa moja dogo husababisha usitimize majukumu yako; mazingira yasiyo ya thamani husababisha utuame. Yaelekea kuwa watu huhisi kwamba wanapaswa kutokuwa na dosari ili wawe na nguvu ya kutafuta. Wakigundua kwamba ni wapotovu sana, basi hawatakuwa na mwelekeo wa kutafuta. Watu wengi wamesema mambo ya kuvunja moyo na hasi kama haya: “Aa! Nimekwisha, ni wazi kuwa nimeangamia. Hakuna jinsi ninavyoweza kuokolewa. Hata kama Mungu angenisamehe, singeweza kujisamehe mwenyewe. Mimi sitabadilika kamwe.” Watu kuelewa visivyo mapenzi ya Mungu kunaonyesha kwamba watu hawaelewi kazi ya Mungu. Kwa kweli, wanadamu mara kwa mara watafunua baadhi ya tabia zao potovu wanapoingia ndani kikawaida. Wao ni wachafu katika mambo ambayo wao hufanya, huwa hawachukui majukumu, hawajitolei, na wao hufanya kazi kwa uzembe. Hii ni jambo la kawaida sana na lisiloepukika. Kama vitu hivi havingefunuliwa, basi mtu angewezaje kusema kwamba wanadamu ni wapotovu? Kama watu hawangekuwa wapotovu, basi kazi ya Mungu ya wokovu haingekuwa na umuhimu. Hali ya sasa ni kwamba watu hawana ukweli, na kwa hakika hawajielewi wenyewe na kuona hali zao kwa dhahiri. Kwa hiyo, hali zao zinahitaji kufunuliwa na kufafanuliwa. Ni kwa kufichua mambo haya tu ndipo watakapoweza kuona mwanga. Watu wote ni wenye ganzi na wapumbavu. Kama Mungu hawezi kufanya kazi kwa njia hii, basi hamtabadilika. Matatizo huwatokea katika kila hatua. Mimi Najadili hili na nyinyi ili kuwasahihisha na kuchukua usukani ili muweze kufuata njia iliyo sahihi. Vinginevyo mtakuwa daima mkifanya mambo kwa kupita mipaka, daima mataelekea kwenye miisho ya barabara, mtaendelea bila njia, na kujieleza wenyewe. Watu wanaanza kupitia mambo, huwa hawajielewi wenyewe, lakini mwisho, kila mtu hujielewa wenyewe, akisema: "Aa, mimi ni ibilisi Shetani! Watu ni ibilisi, mashetani. Wakati huu mimi nimekwisha, siwezi kuokolewa; hakuna nafasi tena na hakuna uwezekano wa kuokolewa. "Kwa kweli watu ni wadhaifu sana na ni vigumu kuwashughulikia, na wao wanapenda kupita mipaka. Kama siku moja watu kweli wangeyaelewa mapenzi ya Mungu, wangesema: "Aa, upotovu wangu ulikuwa na kina kikubwa hivi kwa muda huu wote na mimi hatimaye ninautambua. Kwa bahati nzuri, Mungu huniokoa, na sasa ninaweza kuona maisha ya kung'aa na ninaweza kutembea kwenye njia sahihi ya maisha. Sijui ni jinsi gani ninaweza kumshukuru Mungu. "Ni kama kuinuka kutoka kwa ndoto na kuuona mwanga. Je, si huku ni kupokea wokovu mkuu? Je, hawapaswi kumsifu Mungu? Watu wengine huwa hawajielewi wenyewe hata wakati kifo kimekaribia; bado ni wenye kiburi na hawawezi kukubali ukweli uliofichuliwa. Wanahisi kuwa ni wazuri sana: Mimi ni mtu mzuri, ningewezaje kufanya hivyo? Inaonekana kama wamelaumiwa kimakosa. Baadhi ya watu hupitia miaka ya kazi ya Mungu na mwishowe bado huwa hawaelewi asili zao. Wao daima hudhani kuwa ni watu wema na kwamba walifanya makosa katika muda wa kutojali, na hata leo, wangependelea kuondolewa kuliko kutii. Mtu wa aina hii ni mwenye kiburi na mjinga sana na hasa hawezi kukubali ukweli. Hawawezi kamwe kubadilisha na kuwa wanadamu. Kutokana na haya mnaweza kugundua kwamba hata kama asili za watu ziko katika upinzani na usaliti kwa Mungu, kuna tofauti katika asili zao. Hii huhitaji uelewa wa ndani wa asili za watu.

Kuna sifa ya kawaida katika asili za watu ambazo ni lazima zieleweke. Ni tabia ya kawaida kwamba watu wote wanaweza kumsaliti Mungu, lakini kila mtu ana udhaifu wake. Watu fulani hupenda hiki, na wengine hupenda kile, watu fulani huheshimu hiki na watu wengine huheshimu kile. Hizi ni tofauti katika asili za watu. Baadhi ya watu wana uwezo wa kuhimili mateso kidogo, baadhi ya watu huwa na matatizo kuhimili mateso kidogo. Hii ni kutokana na matamanio katika hali zao kuwa tofauti. Ni vipi kuwa wanakabiliwa na tukio la aina moja, lakini wengine wanaweza kulihimili na wengine hawawezi? Ni kwa sababu mambo ya asili zao ni tofauti. Tabia potovu za baadhi ya watu hudhihirika kwa uzito, na tabia potovu za watu wengine hudhihirika kwa wepesi; hata hivyo, viini vya asili zao ni sawa. Hii ni tabia ya kawaida. Jinsi asili za watu zilivyo huamua watu ni wa aina gani. Ingawa wana sifa za kawaida na watu wengine, huenda wasiwe watu wa aina moja. Kwa nini si watu aina moja? Kwa sababu mambo ya asili zao siyo wazi na hazina nguvu vile. Kwa mfano, si tamaa ni tabia ya kawaida ambayo watu huwa nayo? Kila mtu anayo. Aidha, eneo hili ni gumu sana kulishinda. Hata hivyo, ni kali sana hasa kwa watu wengine. Wakati wanapolikabili suala hili, hawawezi kulishinda na wanaweza kutoroka na watu wengine au kuwaongoza wengine kutoroka. Inaweza kusemwa kwamba asili za watu hawa ni mbovu. Baadhi ya watu ni wadhaifu kidogo katika kukabiliana na suala hili, au kidogo wana shauku na tamaa, lakini hawafanyi mambo ya aibu, wanaweza kujidhibiti wenyewe na kuepuka vitu hivi. Basi hamuwezi kusema kwamba watu hawa wana asili mbaya. Daima kuna shauku na tamaa kwa mwili. Watu wengine hutenda kwa pupa na hujiendekeza katika tamaa zao na kufanya chochote wanachotaka. Lakini watu wengine hawako hivi kabisa. Wanaweza kufuata ukweli na hutegemea ukweli kutenda, na wanaweza kutelekeza mwili. Ingawa wana tamaa za mwili, wao hujionyesha wenyewe kwa njia tofauti. Hapa ndipo ambapo watu hutofautiana. Watu wengine hutamani fedha; wanapoona fedha na mambo mazuri, hutamani kuwa nayo kwa ajili yao wenyewe, na hamu yao ya kuwa nayo ni ya nguvu ya kipekee. Hali ya watu hawa ni uroho na tamaa ya pesa. Wanapoona kitu fulani, wanakuwa waroho; wao hata huthubutu kutumia na kuiba fedha za kanisa, hata dola 20,000 au 30,000; pesa zinavyokuwa nyingi, ndivyo wanavyozidi kudhubutu kufanya hivyo; hawamwogopi Mungu kabisa. Hii ni asili ya tamaa. Watu wengine hutumia dola 10 au 20 na huhisi wasiwasi katika dhamiri zao. Wao huharakisha na kupiga magoti mbele ya Mungu kuomba, na kwa machozi ya majuto, wao huuliza Mungu kuwasamehe. Watu wote wana udhaifu; wewe huwezi kusema kwamba huyu ni mtu ambaye huona tamaa ya fedha, ni tabia ya upotovu tu inayofunuliwa. Watu wengine hupenda kuwahukumu wengine. Wao husema: "Jamaa huyu alitumia dola 3 au 5, na hakusali mbele ya Mungu. Wakati ujao, atatumia dola 20 au 30; huyu mtu ni mroho. "Kuzungumza kwa njia hii si sahihi. Watu huwa na tabia potovu lakini kwa hakika wana udhaifu wa kawaida. Udhaifu mwingine pia ni tabia potovu ya watu, lakini kuna tofauti kati ya tabia potovu na asili ya aina hiyo. Huwezi kuirundika pamoja na kuwahukumu watu kiholela. Kuwahukumu wengine ni jambo la hatari zaidi kwa watu. Kama hamuwezi kutofautisha au kuona mambo kwa dhahiri, basi msifanye madai yasiyo na msingi ili kuepuka kuwaumiza watu. Kuzungumza na kufanya mambo bila kuelewa ukweli ni kupotovu na hakuwafaidi wengine au nyinyi wenyewe.

Mnaamini katika Mungu lakini hamna uhakika kususu ni lengo gani mnalopaswa kufikia. Hakuna yeyote anayeamini au hutafuta kwa mujibu kamili wa mahitaji ya Mungu. Kuna masuala mengi mno yaliyo ndani yenu; labda hamna uhakika kwa sasa juu yayo na hamjachunguza ndani ya mawazo yenu na tabia zenu za asili au labda hamkuzichambua mapema. Siku moja, utayaelewa maneno haya, na wakati huo, utaweza kujielewa mwenyewe.

Pia kuna mambo mengi yasiyofaa katika asili za watu. Wakati watu wanavaa nguo nzuri au kupata simu ya mkononi, toni ya sauti zao hubadilika; wakati wanawake wengine wanavaa viatu vya mchuchumio, wao hutembea na mkao tofauti. Ni vitu gani vilivyo katika nyoyo za watu na ni asili gani huwafanya wafunue vitu hivi viovu na vibaya? Hivyo ni vitu vya asili ya kibinadamu ambavyo watu wanahitaji kuvielewa. Watu siku hizi bado hutegemea utashi kudhibiti vitu hivi katika asili ya binadamu, hali ambayo husababisha wasifunue chochote. Hata hivyo, pamoja na uzoefu wa watu, na pamoja na uelewa wa watu kuongeza uketo katika kila nyanja ya ukweli, na kuelewa kwa asili zao, wataingia ndani hatua kwa hatua kulingana na matakwa ya Mungu, na hayo yote yataanza kubadilika hatua kwa hatua. Watu wanapoanza kuingia ndani, ni lazima wafanye mazoezi ya kuutelekeza mwili. Baadaye, wanapofahamu na kuuelewa ukweli kwa hakika hawatahitaji nguvu maalum za kuutelekeza mwili. Wakati huo, watu wataweza kwa utambuzi kuishi kulingana na ukweli. Watakuwa na kanuni na upeo kwa kile wanachokifanya, na watakaa ndani ya mipaka. Kuna matatizo wakati watu wanapitia maneno ya Mungu mara ya kwanza. Kwa sababu hawaelewi ukweli, wao daima huuliza jinsi ya kufanya hili na lile. Aidha, hali ya hasi ya watu daima huwasumbua, na wao huhisi kwamba hawana njia ya kufuata. Msihangaike kuhusu hali hasi; Baadhi yazo zinaweza kutatuliwa. Ikiwa unaweza kuwasiliana nao, basi wasiliana nao; usihangaike kuhusu wale usioweza kuwasiliana nao, fanya mazoezi tu na kuingia ndani kwa kawaida na kuwasilisha ukweli zaidi. Hatimaye, siku moja wakati una uhakika juu ya ukweli, na unaona mambo mengi kwa dhahiri, basi hali hasi kwa kawaida zitatoweka. Sasa hamko katika hali mliyokuwa hapo awali, sivyo? Angalau ni chache kuliko hapo awali. Mkizingatia kufuata ukweli kwa bidii, basi suala lolote linaweza kutatuliwa. Kuwa na uwezo wa kutatua matatizo yenu wenyewe ni maendeleo na ukuaji. Baada ya kupitia kwa kiwango fulani, maoni ya maisha ya mtu, umuhimu wa kuwepo, na msingi wa kuwepo utabadilika kabisa. Hiyo ni kwamba mtazaliwa tena, na kuwa watu tofauti kabisa. Hili ni la kushangaza! Haya ni mabadiliko makubwa; ni mabadiliko ambayo hugeuza kila kitu pindu. Utahisi kwamba umaarufu, faida, msimamo, mali, anasa, na utukufu wa dunia havina maana na kwamba una uwezo wa kuviachilia kwa urahisi. Huyu ni mtu katika mfano wa mwanadamu. Wale ambao hatimaye wamekamilishwa watakuwa kikundi kama hiki. Wao wataishi kwa ajili ya ukweli, kwa ajili ya Mungu, na kwa ajili haki. Huu ni mfano wa mtu. Baadhi ya watu watauliza: "Mtu ni nini?" Watu siku hizi sio watu. Ikiwa wao sio watu, basi wao ni nini? Unaweza kusema wao ni wanyama, ng'ombe, mashetani, na pepo. Kwa kifupi, wako tu katika mfano wa watu, lakini si hawastahili kuitwa watu, kwa sababu hawana ubinadamu wa kawaida. Unasema kuwa watu ni wanyama, lakini wana lugha, mawazo, na fikira, na wana uwezo wa kubuni teknolojia, hivyo wanapaswa kuainishwa kama wanyama walioendelea. Wasioamini husema kwamba mababu zao walikuwa sokwe; walikuwa wanyama, sio watu, na ni sahihi kwa kusema kwamba watu ni mashetani na pepo. Kwa sababu hii ndivyo asili za watu zilivyo, hili ndilo wao hufichua na kuonyesha; kwa hiyo, ni sahihi zaidi kusema kuwa watu ni pepo na mashetani, wao si samaki wala ndege, wao hawafanani na watu. Waamini wengine wa muda mrefu wamepitia miaka mingi, na kuwa na ufahamu wa ndani kiasi; kasi fulani wanaweza kumwelewa Mungu kidogo, kwa kiasi fulani wana wasiwasi juu ya mambo ambayo Mungu huyajali, na kufikiri juu ya kile Mungu anachofikiria. Wana nia hizi. Huu kwa kiasi fulani u katika mfano wa mtu, na u karibu kufika. Waumini wapya hawana uzoefu wa kuadibiwa au kuhukumiwa na hawajapitia kupogolewa kwingi au kushughulikiwa. Hawasikilizi ukweli mwingi, na husoma tu neno la Mungu, lakini kwa kweli hawajalipitia. Hata wako mbali zaidi. Kina cha uzoefu ambacho watu wanacho kitaamua ni kiasi gani watakachobadilika. Jinsi unavyopata uzoefu kidogo, na jinsi unavyopata ufahamu kidogo wa ukweli, ndivyo utakavyokuwa na mchanganyiko mchache wa binadamu ndani yako. Kama huna uzoefu wowote, basi wewe ni Shetani hai asiyebadilika, na wewe ni ibilisi tu. Je, unaamini jambo hili? Utayaelewa maneno haya siku moja. Watu wazuri wako wapi siku hizi? Bila mfano wa kibinadamu, unawezaje kuitwa mtu? Watu wema hawapo. Watu wana magamba ya kibinadamu tu kwa nje na hawana kiini cha binadamu. Kusema kuwa watu ni wanyama kwa mavazi ya binadamu si kutia chumvi. Katika kupitia kazi ya Mungu, ukitaka kuwa katika mfano wa mtu, lazima upitie ufunuo, kuadibiwa, na hukumu ya maneno haya, na hatimaye utaweza kubadilika. Hii ni njia, na watu wasipoifanya kwa njia hii, hawawezi kubadilika. Wanapaswa kufanya hivyo kidogo kidogo na ni lazima wapitie hukumu na uadibiwaji; na kupogolewa kwa mfululizo na kushughulikiwa. Vitu vilivyofunuliwa katika asili za watu ni lazima vifichuliwe. Baada ya kufichuliwa na watu kuvielewa vizuri, wataweza kutembea kwenye njia sahihi. Ni baada tu ya kupata uzoefu kwa muda na kuelewa ukweli fulani ndipo watakapokuwa na uhakika wa kusimama kiasi. Hali zenu za sasa zimepunguka. Licha ya ukweli kwamba mmekuwa mkiruka kwa furaha, huu kweli ni wakati hatari zaidi kwenu. Kila mtu yuko karibu kufikwa na hatari. Mimi Nimesema hili mara nyingi, lakini watu wengi hawaelewi maana ya maneno haya. Baadhi ya watu watafikiri: "Hatari? Hatari gani? Hali yangu ya sasa ni nzuri, nitawezaje kuwa katika hatari? Ni vigumu kuwa nitaanguka au kupoteza njia yangu. Mungu ni mwenye neema kwangu. "Je, ni nani mnayesema hapati neema? Kila mtu hupokea neema, lakini kila mtu yuko hatarini; ni baraka maalum kwako kuwa katika hatari na kupata neema. Watu sasa wanahisi kwamba wako karibu kufika wanakopaswa kuwa, lakini ukweli kwamba wanasema hivi inathibitisha kwamba wako mbali sana.

Iliyotangulia:Sura ya 52. Dalili za Udanganyifu Ndani ya Mwanadamu na Asili ya Mwanadamu Ambazo Humsaliti Mungu

Inayofuata:Sura ya 54. Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja