Sura ya 52. Dalili za Udanganyifu Ndani ya Mwanadamu na Asili ya Mwanadamu Ambazo Humsaliti Mungu

Ugumu ambao watu wanaweza kuukabili kwa urahisi katika uzoefu wao, vitu ambavyo vinawasababisha watu kuanguka kwa urahisi, na pahali ambapo udhaifu wa jaala wa kila mtu upo yote ni masuala ambayo lazima mtu awe na ujuzi nayo. Kwa nini unaanguka, unamwacha Mungu na kupoteza imani ya kuendelea na ukimbiziaji wako wa ukweli unapokabiliana na mambo fulani? Kwa sasa, kila mtu yumo hatarini mwa mambo haya. Bila kujali kiwango cha imani uliyo nayo kwa kawaida, shauku yako ni kubwa kiasi gani, wewe ni shupavu na asiyekubali kushindwa jinsi gani, ni kitu cha aina moja pekee kinaweza kufanyika ambacho kinaweza kufanya kila mmoja kushtuka na kuanguka kwa urahisi. Hicho ni kitu cha aina gani? Inapoonekana kuwa wale wanaomwamini Mungu huteseka dhuluma na kutengwa duniani ilhali wasioamini wanafanikiwa duniani nao ni matajiri na wenye mamlaka, na wakati waumini wanaonekana kudhulumiwa na kuonewa, wengi wa watu hawawezi kuelewa jambo hili. Baadhi hata hulalamika: “Hata hivyo hakuna Mungu? Mbona Mungu hatusaidii? Mbona Mungu hafanyi lolote kuhusu watu hawa?” Ni nini shida wakati hali ya aina hii linatokea mara kwa mara? Hasa unapoona kuwa majeshi ya wasioamini ni yenye nguvu zaidi unafikiria: “Mbona familia ya Mungu haina majeshi yake binafsi? Mbona familia ya Mungu siku zote inateseka kuonewa na kudhulumiwa na wengine?” Wengi wa watu watakuwa dhaifu namna hii wakati jambo la aina hili hutokea. Kila mtu atafikiria jinsi namna ya afisa duniani ni ya kuvutia, jinsi filosofia zao za maisha zilivyo za kiburi, fiche ama zisizo wazi, jinsi walivyo hodari, jinsi walivyovalia vizuri, jinsi walivyo na uwepo…. Wengi wa watu wanaonea wivu vitu hivi ndani ya mioyo yao. Sivyo? Watu wote wana vitu hivi ndani yao na wanaweza kushindwa na kujaribiwa na vitu hivi, hadi hata kiwango ambacho vitu hivi vinaweza kuwafanya kuwa dhaifu kwa muda. Jambo hili linadhibitisha kwamba watu bado hawana shauku sana katika Mungu, katika neno Lake ama katika ukweli. Haijalishi jinsi usivyokubali kushindwa ama kiwango cha imani uliyo nayo kwa kawaida, unapokumbana na jambo kama hili unakuwa dhaifu kwa muda; unapokumbana na ugumu mkuu, inakuchukua siku nyingi kupata ahueni. Watu wengine hawawezi kustahimili wanapomwona mtu mwengine akiingia katika chuo cha elimu, ama akiwa afisa. Hata iwapo mtu mwengine atapata nyongeza ya mshahara kazini ama awe na maisha mazuri ya familia, ama iwapo ana kitu ambacho anafurahia, hawawezi tu kustahimili hayo! Watu wengine wanapenda magari, na wanafikiri: “Mbona wengine wanaweza kuwa na magari mazuri, lakini hatuwezi kuwa na magari mazuri? Tunamwamini Mungu kwa hivyo tunapaswa kupewa kipaumbele. Mungu anapaswa kuturuhusu kufurahia vitu hivi kwanza. Mbona tusivifurahie sasa?” Kwamba watu wanayo majibizo haya na kufikiri vitu hivi ndani ya mioyo yao, kwamba wanavichukulia vitu hivi kuwa muhimu sana hufichua asili ya mwanadamu ilivyo. Watu wanacho kitu kimoja ndani ya asili zao na kinawaruhusu kuwa na shauku katika vitu hivi. Aidha, ni kana kwamba hawawezi kujiondoa kwa vitu kama hivi. Wanahisi kwamba, bila vitu hivi, maisha yanachosha. Sasa kuna watu wengi wanaofikiri kwa kawaida: “Je, ningeendelea kuishi iwapo singekuwa na ukweli? Ningeendelea kuishi bila Mungu?” Wanatafakari hili na mwishowe kufikiri: “Ndiyo, bado ningeishi, na singehisi vibaya sana kulihusu. Iwapo sasa hakungekuwa na jamii, wala mataifa, wala wasioamini, ningehisi kwamba pengine dunia ni tupu sana, bila chochote cha kusisimua kikitendeka.” Asili za watu zina vitu hivi ndani zake, na hawamtamani Mungu sana, wala hawatamani sana vitu ambavyo ni vyema, changamfu, vya urembo ama vizuri. Kwa hivyo watu bado wanamwamini Mungu kwa ajili ya nini? Wanamwamini Mungu tu kwa sababu wana tamanio na wanahitaji kitu kutoka Kwake. Wakiongozwa na tamanio hili, watu wanautafuta ukweli, wanamwamini Mungu, wanateseka ugumu na ni shupavu. Lakini kwamba mtu humwamini Mungu na huteseka kidogo haimaanishi kwamba wameviacha vitu hivyo. Kwa ukweli halisi, bado wanavitamani sana. Mbona watu wengine hufichua nyuso zao ibilisi punde wanapokuwa viongozi ama wako katika nafasi ya jukumu? Hii inaonyesha kwamba mioyo yao inatamani sana vitu hivyo. Hii ni asili ya aina gani? Asili hii ndani ya mwanadamu ni kama ya Shetani. Yote ambayo Shetani anaabudu ni vitu hivi na Shetani anavifurahia vyote. Asili ndani ya mwanadamu ni sawa na ile ya Shetani, kwa hivyo wana mtazamo sawa na Shetani, wakiungana naye bila hiari. Unaona kwamba kila mtu ana baadhi ya vitu ndani yake ambavyo vinaenda dhidi ya ukweli, ambavyo havikubaliani na ukweli. Vitu hivi havilingani kabisa na ukweli na havina uhusuano nao, lakini watu hawana uwezo wa kutambua hili. Watu wanahisi wakati mwingine: “Kuna sababu mbona nafanya hili kwa njia hii; ni sahihi. Inapaswa kusemwa kwamba linakubaliana na ukweli na ninalifanya kulingana na mahitaji ya Mungu.” Kwa kweli kile unachofanya ni kitu ambacho kimeibuka kutoka kwa makusudi mema ya mwanadamu na kutoka kwa asili yako ya kishetani. Unaweza kuhisi kwamba ni kizuri sana, lakini kwa kweli hakikubaliani na ukweli. Mbona watu wengine wanaogopa wanapoona majeshi makubwa ya wasioamini? Zaidi, wanawaonea wivu ndani ya mioyo yao, wakisema: “Iwapo ningemwamini Mungu na pia kuwa na mamlaka kama haya, kuwa na pesa nyingi sana na kuwa na watu wengi wanaonisaidia, basi hiyo ingekuwa vizuri sana.” Hivi ndivyo vitu ambavyo watu wana wivu navyo. Iwapo watu hawangekuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, hawangekuwa na mazingira dhalimu, wala mtu wa kuwaongoza, mtu wa kuwashurutisha, basi kila mtu angefuata mitindo ya dunia na hakuna ambaye angemwamini Mungu. Kwa wale miongoni mwenu ambao sasa ni viongozi, mnaweza kuwa mmejaa nguvu, na mnafikiri: “Lazima nifanye kazi yangu vizuri, na kuwaongoza watu hawa vizuri.” Lakini ungekuwa mtu aliye chini anayefuata na aliye na mtu mwengine wa kumwongoza, pengine hungekuwa na nguvu uliyo nayo sasa, na pengine mara nyingi utakuwa mnyonge na kuvunjika moyo kama watu wengine. Wakati uko katika nafasi ya jukumu unahisi kwamba lazima uwafanye walio chini yako wafuate imani yao kwa makini, na kutowaacha wapotoke kwa sababu ya uongozi wako. Kazi yako kama kiongozi ni kuwaruhusu wale walio chini yako kufuata. Na hadhi hii unaweza kufanya kazi hiyo vyema. Lakini iwapo hungekuwa na hadhi hii, basi pengine hungekuwa na nguvu kama ulivyo sasa. Kwa kuchunguza vitu hivi ndani ya watu tutagundua kwamba vitu ambavyo wanatamani sana si vya haki, si vya mwanga, si vya ukweli na havikubaliani na ukweli. Badala yake, wanatamani sana vile vitu ambavyo ni vya dunia, vitu vilivyo vya Shetani, na vitu ambavyo watu wanavidhania kuwa vizuri. Katika kueneza injili watu wengi huwa hasi wanapoona kwamba kazi yao inakuwa ngumu au watu wachache sana wanaingia kanisani. Wanafikiri: “Majeshi ya madhehebu na makundi yote ni ya nguvu sana na watu ambao wanawabadili ni wanafuzi wa chuo cha elimu, wasomi wa aina zote na pia baadhi ya afisa.” Ni kana kwamba wanahisi kutolewa heshima kubwa kwa sababu ya hawa maafisa na wanafunzi wengi wa chuo cha elimu, bila kutambua mwanafunzi wa chuo cha elimu anafikia kiwango kipi. Wanafanya wanaloweza kuwaabudu wale walio na maarifa kidogo ama elimu kidogo, na pia wanawaona maafisa na majeshi haya kuwa hasa muhimu. Lakini imani yako iko kwa Mungu, sio kwao, wala siyo imani katika nguvu zao. Watu wanamwamini Mungu lakini wanatafuta usalama katika majeshi haya na kuwaabudu wale walio na kiwango kikubwa cha maarifa. Hili linaamua asili ya mwanadamu kuwa ipi? Mwanadamu anamsaliti Mungu. Ndani ya vitu hivi ambavyo watu wanaabudu, ni vipi humletea Mungu furaha? Hakuna chochote! Maarifa, hadhi, umaarufu na faida, utajiri, mamlaka—ni vipi kati ya hivi ambavyo Mungu hupenda? Ni vipi viliyo vitu vizuri? Ni vipi vinakubaliana na ukweli? Hakuna chochote! Lakini vitu hivi vipo katika kila mtu na vinapendwa na kila mtu. Kutoka kwa uhusiano wa watu wawili na kutoka kwa mielekeo yao kwa wengine inaweza kuonekana kuwa watu wanatilia maanani sana hadhi, mamlaka na utajiri. Mtu anapoenda katika nyumba ya mwengine na kuona kwamba ni tajiri, na kwamba familia yake huishi katika hali ya kufaa, anataka kubaki hapo na asiondoke, akisahau hata baba na mama yake mwenyewe. Wazazi waliomzaa na kumlea, waliochukua miaka mingi kumuelimisha wanasahaulika kabisa, hadi kiwango anapoweza kuwatupa wazazi wake mara moja, kwa hivyo kumsahau Mungu si rahisi sana kwake kufanya? Asili ya usaliti ndani ya mwanadamu ni kali sana na imekita mizizi sana. Mbona inasemwa kwamba asili ya mwanadamu ni kusaliti? Usaliti huu una vitu vingapi ndani yake? Ni pamoja na vitu vyote ambavyo watu hupenda, kutamani sana, kutafuta, kulinda na vitu vyote ambavyo watu wanaweza kufikiria. Kwa ujumla, inaweza kusemwa kwamba asili ya mwanadamu ni kusaliti. Tunawezaje kuona kwamba hivi ndivyo yalivyo mambo? Inawezekana kabisa kuona wakati wa kulinganisha mwelekeo wa watu kwa Mungu, kumtafuta Yeye kwao na vitu ambavyo wanavifikiri ndani ya mioyo yao na ambavyo Mungu anahitaji kutoka kwao, haijalishi iwapo anachofikiria mtu siku nzima kinakubaliana na mapenzi ya Mungu au la. Kwa hivyo watu hufikiria nini masaa ishirini na manne ya siku? Kando na wanapolala ama wakati wa mlo, watu hufikiria nini? Wanakaa hapo bila chakufanya na kutafakari: “Eh, tazama familia hiyo inayoishi kwa furaha sana, kwa raha sana. Ningeishi kama wao ilhali pia kumwamini Mungu, hilo lingekuwa vyema zaidi! Ningekuwa na mema kutoka pande zote ziwezekanazo!” Kisha kuna wale ambao hutafakari siku nzima: “Ningekuwa na maisha kamili ya familia kama walivyo nayo na ningepata mwenzi mzuri, mtu ambaye hatanitesa, basi hilo lingekuwa vyema sana!” Kisha kuna baadhi amabo huwaona wengine na kazi nzuri, na kufikiri: “Eh, Ningekuwa na hali sawa na wao, na kazi nzuri na kutengeneza pesa nyingi, nikivaa nguo nzuri na kula vyema, ningekuwa na hayo na pia kumwamini Mungu, basi hiyo ingekuwa vyema kiasi gani!” Daima huweka kumwamini Mungu mwisho kabisa na kwa kutajwa kwa kumwamini Mungu, watahisi: “Sasa kumwamini Mungu kwa njia hii inamaanisha kwamba nakosa kufanya mambo fulani. Iwapo ninaweza kufurahia maisha zaidikidogo, kula vyema kidogo, na kutokuwa na anayenitesa, hilo si bora? Mbona basi Mungu hanisaidii kutimiza lengo langu kwa njia hiyo? Mbona basi Mungu haniridhishi kwa njia hiyo?” Mbona imesemwa awali kwamba kila kitu kilicho moyoni mwa mwanadamu ni kibovu, na hakikubaliani na mapenzi ya Mungu? Moyo wa mwanadamu umejawa na kula kwa chakula, kuvaa kwa nguo, kujiburudisha na kujifurahisha. Lakini vitu hivi ni vya nini? Ni vya dunia; ni vya ibilisi. Mapenzi ya Mungu si kuwaruhusu wanadamu kufurahia vitu hivi tu; kama ilivyosema Biblia awali: “Mtu hataishi kwa mkate pekee yake, ila kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.” Lakini sasa mwanadamu haishi kumwamini Mungu pekee, wala haishi kupata neno la Mungu pekee. Anayo malengo mengine mengi, vitu vingine vingi anavyotamani sana. Mtazamo wake kuhusu maisha si kuishi kwa ajili ya Mungu au kuishi kwa ajili ya neno la Mungu, au kuishi kwa ajili ya haki, au kumkidhi Mungu, au kuyatimiza mapenzi ya Mungu, au kuokolewa. Mwanadamu halengi mambo haya, na yuko mbali kuyafikia. Wengi wa watu huishi ili kupata baraka. Kisha kuna baadhi ambao huishi ili kupata sifa njema, na hili ni kosa zaidi! “Joka kuu jekundu hunitesa kwa kiwango kama hiki. Si lazima niishi vizuri? Joka kuu jekundu hunidhuru sana, huwadhuru ndugu zangu na huidhuru familia ya Mungu. Lazima nijaribu kuishi vyema na mwishowe niupokee wokovu wangu. Hilo litakuwa funzo kwake, na hii itakuwa njia ya nguvu yangu kurudisha pigo.” Na kisha kuna wale wanaosema ndani ya mioyo yao: “Eh, kama sisi, kundi hili la watu, hatumwamini Mungu kwa makini, na kazi ya Mungu inatumiwa vibaya nasi, basi tunapaswa kulaaniwa na hatutaweza kuonyesha nyuso zetu kwa watu wa dunia! Hata zaidi hatutaweza kuonyesha nyuso zetu kwa wale ambao tayari walitudhihaki na kututukana!” Maana iliyodokezwa ni: “Mungu, lazima Wewe unifanye mkamilifu. Usipofanya hivyo, basi ni wapi ningeuonyesha uso wangu? Singeweza tena kumwona yeyote.” Huu ni mtazamo ambao watu wanao ndani yao. Mbona watu huishi, malengo ya maisha yao ni yapi, mtizamo wao kuhusu maisha ni upi, msingi wao wa kuishi ni upi—vitu hivi vyote vinaweza kuonekana kabisa. Watu wengine hufikiri sasa kwamba wana baadhi ya nia ya kuishi kwa ajili ya Mungu na kwamba kuna baadhi ya maonyesho maalum ya haya. Wanaweza kuacha familia zao na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kutoa kwa ajili ya Mungu. Hawawataki tena watoto wao, waume zao ama wake zao. Wanaweza kuhisi kwamba ni vijana lakini hawataoa au kuolewa, na hili linaweza kudhaniwa kama kuishi kwa ajili ya Mungu. Juujuu umeiacha familia yako, na unatenda kwa njia hii kidogo na kutenda kwa njia hii kidogo—hiki ni kipengele cha mwanadamu cha ushirikiano. Lakini malengo ambayo mwanadamu anatamani sana ndani ya moyo wake si vitu hivi. Kile wanachofikiria watu masaa ishirini na manne ya siku ni chakula kipi kizuri cha kula, nguo gani nzuri za kununua, viatu vipi vizuri vya kununua, ama kujadili jinsi walivyo watu wengine, ama kutafakari yale yatakayowafanyikia siku za baadaye, ama jinsi ya kuishi maisha mazuri. Hivi ndivyo vitu wanavyofikiria pekee. Kisha kuna wale ambao hutafakari: “Wakati mimi ni mzee, sitakuwa na familia na sitakuwa na makazi. Ni wakati upi basi nitaweza kuishi kwa furaha? Ni wakati upi sitateseka namna hii?” Daima wanahisi wasiwasi ndani yao kuhusu vitu hivi na kuhisi kubanwa navyo kiwango cha kutoweza kupumua. Unaona kwamba mnapokaa pamoja katika ushirika, hali ya aina hii inaibuka mara nyingi: Dada anashiriki na mwengine na anasema, “Umeshindaje hivi karibuni?” Mwengine anasema: “Hali yangu haikuwa nzuri awali, lakini nimepata afueni.” Dada anasema: “Haya niambie jinsi ulivyopata afueni.” Huyo mwengine basi anashiriki naye, akipiga gumzo na kutoka nje ya mada, akikengeuka kutoka kwa mada. Iwapo hamna mtu hapo wa kusimamia, mkutano unageuka kuwa porojo, na hakuna kinachopatwa hata kidogo. Katika mwanadamu hakuna mwanga mwingi wa ukweli, hamna uzoefu ama uelewa mwingi wa ukweli. Hivyo basi hata wakati wa kushiriki hawawezi kufikia mada sahihi—hiki ndicho kimo cha mwanadamu sasa hivi. Kuna watu wengi sasa ambao hawapitii majaribu au kuteseka mazingira mabaya na wanafikiri: “Natafuta ukweli vyema sana hivi sasa. Angalau najua jinsi ya kupata uzoefu nami niko karibu kidogo na uhalisi. Ninaweza kuelewa kile anachosema Mungu na pia naweza kukipokea. Haijalishi linaloweza kunifikia, nahisi kwamba sitakuwa msaliti wala kumwacha Mungu.” Hivi ndivyo wengi wa watu wanaoishi kwa raha huhisi. Lakini kwa kweli hujatambua kwamba, ingawa huwezi kumwacha Mungu, moyo wako u mbali na kuwa sawa na awali. Iwapo kwa kweli unaweza kuhakikisha kwamba utaendelea licha ya mazingira, licha ya kile kinachoweza kukufikia, licha ya taabu, majaribu au mateso unayoweza kupitia, au ugonjwa unaoweza kukuumiza, iwapo unaweza kuendelea bila kujali yatakayotokea, bila kubadili azimio lako la asili au malengo utafutayo, basi unahitajika kuangusha vizuizi vyote katika njia yako na kutakasa kabisa vitu vyote vilivyobaki ndani ya moyo wako ambavyo havikubaliani na ukweli. Hapo tu ndipo utakapoweza kutatua shida zako kabisa.

Watu wachache sasa husema: “Natoa maisha yangu yote kwa Mungu. Haijalishi maisha yangu yatadumu kwa muda gani, nitafuata hadi mwsho kabisa. Haijalishi afanyacho Mungu, haijalishi jinsi Mungu atakavyonitendea, nitayashika imara maneno ya Mungu.” Umefikiria namna hii? Pengine umefikiria namna hii mara chache, lakini bado unahisi kwamba huna azimio la aina hiyo, kwamba huna nguvu ya kutosha kulifikia. Hali hizi zote ziko katika mioyo ya watu. Iwapo baadaye kitu kiabadilika ghafla, unaweza basi kuwa katika hatari ya kuanguka, unaweza kuiacha njia ya kweli, na unaweza kuwa mtu anayekufuru dhidi ya Mungu. Je, hili si hatari? Iwapo hakuna mabadiliko katika mitazamo na fikira za asili ndani yako, na hakuna badiliko katika malengo ya maisha yako na katika msingi wako wa kuishi, basi hutakuwa salama na unaweza kukumbana na hali ya hatari. Kwa sababu kila siku watu wana fikira hai na kwa sababu mbongo na mioyo yao iko hai kwa kiwango kwamba, wakati wowote, watafuata baada ya mabadiliko katika mazingira yao na hali zao. Sasa hivi unakaa hapa lakini pengine wakati ujao utakuwa umetorokea kwingine na kupotea kabisa. Mabadiliko yanaweza kutokea haraka sana! Ndani ya kanisa kuna baadhi ambao leo wataimba nyimbo za kidini na kucheza ngoma, na wataomba kwa machozi wakiwa na hisia kali. Lakini kesho watakuwa wamepotea, wakiwa wameenda pasipojulikana na yeyote, pengine kwa sinema, ukumbi wa kucheza ngoma, nyumba ya kamari, wakiwa wamepotea katika bahari za dunia. Wale miongoni mwenu leo ambao ni viongozi ama wamekuwa wafanyikazi mnahisi kwamba mko salama na haiwezekani kwenu kuanguka chini. Baadhi hata hufikiri: “Nimepitia hatari na kukaa gerezani kwa muda. Nimestahimili mateso na kupitia majaribu na sijajiondoa.” Vitu hivi si hakikisho la majaliwa yako. Kwa ukweli wa hakika, kila mtu yumo hatarini kila siku. Wengine ghafla watakutana na kitu fulani siku moja ambacho kitawafanya kuhisi kwamba hawawezi kuendelea kuishi, hadi watakapotaka kufa. Kama wakati ambapo mtu ni mgonjwa sana naye anapumua hewa yake ya mwisho. Anahisi kana kwamba maisha ni machungu sana, kwamba hayana haja na afadhali tu afe. Kifo pia ni njia ya kujiondoa. Hili si wazo lao? Iwapo hakuna jambo baya limemfikia mtu, wao hufikiri, “La, siwezi! Siwezi!” Haijalishi jinsi gani unaweza kufikiri, huwezi kugundua hisia hiyo, na haijalishi unaitafakari kiasi gani, huwezi kutambua akili hiyo ilikuwaje wakati huo. Wakati mtu anaugua naye ana maumivu makali, anahisi kwamba hawezi kuyastahimili. Lakini afikiriapo kuhusu wakati huo baadaye, hawezi kuyakumbuka, kana kwamba hakuhisi maumivu hata kidogo; baada ya kufika pwani, mtu haombi tena. Watu ni viumbe hai walio na fikira hai na wanabadilika na mazingira yao. Hiyo ni kusema kwamba kila mtu yu katika hatari kubwa, na yuko ukingoni mwa hatari; huko salama na huna uhakika, bila kujua wakati badiliko litafanyika. Baadaye, kutakuwa na baadhi ya watu watakaokabiliwa na mateso makubwa ama majaribu makubwa. Bila shaka wakati majaribu yatawafikia baadaye hayatakuwa ya kiwango cha Ayubu; jinsi gani yeyote anaweza kuwa na kimo kinacholingana na cha Ayubu? Watu siku hizi hawawezi kuitwa watu wazuri, sembuse kuitwa watu wenye haki. Kwa hivyo wale waliokuja baadaye hawakustahili kufurahia majaribu ya aina moja kama Ayubu. Aina ya majaribu aliyopitia Ayubu yalikuwa kuwa na ushuhuda kwa Yehova na hiki ni kitu ambacho hakitafanyika tena. Ayubu hasa alikuwa amependelewa kufurahia majaribu haya na kuwa na kushuhudia kwake kulikuwa kumekamilika. Watu siku hizi kimsingi hawamiliki imani na ubinadamu wa Ayubu, hawana ukweli wanaopaswa kuwa nao, na asili yao potovu karibu isiweze kurekebishwa, kwa hivyo wangewezaje kubaki wamesimama wakati wa majaribu yoyote? Unapaswa kujiandaa na ukweli iwapo unapaswa kujua jinsi ya kubaki umesimama wakati wa majaribu ya baadaye, na iwapo unapaswa kujua aina gani ya mtazamo unapaswa kuweka. Usipojiandaa vizuri na ukweli sasa, wakati majaribu yanakufikia utakuwa katika dhiki kubwa sana, na utakuwa umechelewa kujuta.

Iliyotangulia: Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?

Inayofuata: Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki