Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Yaliyomo

Sura ya 50. Yote Yanaamuliwa na Iwapo Mtu Anaumiliki Ukweli

Isipokuwa unapagawa na roho wabaya, bila kujali aina ya roho aliye ndani yako, asili ya kibinadamu daima huwa sawa. Watu wengine daima huhisi kwamba roho yao si sahihi, kwa sababu wanaweza kufanya mambo ambayo ni ya kipekee, wakati watu wengine pia wanahisi kuwa labda roho yao haifai kabisa, kwa sababu hawawezi kamwe kubadilika. Kwa kweli, bila kujali kama kuna kitu chochote kibaya na roho, asili ya mwanadamu daima huwa sawa. Daima humpinga Mungu na kumsaliti Mungu. Kiwango cha upotovu wao pia unafanana kwa karibu sana. Mambo hayo ambayo ni ya kawaida kwa asili ya binadamu yote huwa sawa. Watu wengine daima hushuku kuwa roho zao si sahihi, au wanaweza kufikiri: "Kwa nini nilifanya mambo kama hayo? Singewahi kufikiri kamwe! Je, ni kwa sababu roho yangu si sahihi?" Kwa watu wengine, bila kujali wanachofanya, hawachunguzi roho zao kamwe, na wao huchunguza tu, "Kwa nini nilifanya vitu kwa namna hii? Asili hii yangu ni nini? Napaswa kufanyaje katika siku zijazo ili niushike ukweli?" Mbinu na njia zinazochukuliwa kwa ajili ya uchunguzi ni tofauti; watu wengine wanatafuta ukweli, wakati watu wengine wanaendelea kugharimika juhudi kuelekea hasi. Sasa lazima uelewe kwamba, bila kujali mtu ni wa roho gani, mambo kuhusu roho ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kuona wala kugusa, na jambo la muhimu kuzingatia ni asili yako, kama vile vile kile kilicho katika asili yako. Matendo yako yanafichua thibitisho za kile asili yako ilicho. Thibitisho za nini asili yako ilivyo yanafunua kile ambacho kiini chako kilivyo, lakini hakuna thibitisho la aina ya roho ambayo wewe ulivyo. Asili zote za mwanadamu ni sawa baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani. Zote zilikuja kutoka kwa babu mmoja wa kibinadamu, zikiiishi katika ulimwengu sawa, zikipitia katika upotovu sawa. Mambo ya asili ya binadamu yote ni sawa, mambo yote ya kawaida kwa wanadamu ni sawa, lakini watu wengine wanaweza kufanya mambo fulani kulingana na mazingira hayo, wakati watu wengine wanaweza kufanya mambo mengine kulingana na mazingira yale. Watu wengine wamezaliwa na utamaduni na maarifa fulani, wao ni wasomi; wakati watu wengine hawana utamaduni au ujuzi wowote, bila elimu nyingi. Watu wengine huona mambo kwa mtazamo huu, wakati wengine wanaona mambo kwa mtazamo mwingine. Watu wengine huishi katika mazingira fulani ya kijamii, wakati wengine wanaishi ndani ya mazingira tofauti ya kijamii. Kila mmoja wao ana mila, desturi, na tabia tofauti, lakini yale yanayotoka kwa asili ya wanadamu ni sawa kwa kiasi kikubwa, kwa hivyo si muhimu kujali kuhusu wewe ni wa roho wa aina gani. Hiki ni kitu ambacho hakuna binadamu wanaweza kufikia, hiki ni kitu ambacho Mungu pekee Anajua. Kwa hali yoyote, haina maana kwa mtu kujua mambo kama hayo. Hakuna faida inayoweza kutoka kwa tamaa ya kuchangua na kuisoma roho ya mtu; hiki ni kitu ambacho wale wapumbavu na wajinga sana watajihusisha nacho. Usijishuku kila wakati ukifanya kitu kibaya au ukifanya makosa: "Aa, kuna kitu kibaya na roho yangu? Mimi ni roho mbaya? Je! Roho yangu sio ya haki? Je, mbona mimi hushinda nikifanya mambo kama haya?" Bila kujali matendo ambayo yamefanyika, unapaswa daima kutafuta chanzo kutoka ndani ya asili yako, unapaswa kutafuta ukweli kila siku ambao mwanadamu anapaswa kuingia ndani yake. Ukiichunguza roho yako, hutapata majibu yoyote. Hata ukijua wewe ni wa roho wa ya aina gani, bado huna ufahamu wa asili yako mwenyewe, na bado hutakuwa na uwezo wa kutatua suala lililopo. Kwa hivyo, baadhi yenu huendelea kuzungumza juu ya nyinyi ni wa roho ya aina gani, ni kama nyinyi hasa ni wa kiroho, kama nyinyi ni wenye habari; lakini kwa kweli, wewe hata zaidi sio stadi, mpumbavu hata zaidi. Wengine kati yenu pia hulijadiliana kwa namna hasa ya kiroho, ni kama mambo unayosema ni makubwa sana, ni kama haya ni mambo ambayo watu wa kawaida hawawezi kuelewa, kusema mambo kama "Kitu muhimu kwetu ni kuchunguza sisi ni wa roho ya aina gani. Bila roho ya kibinadamu, huwezi kuokolewa hata kama unamwamini Mungu. Acha kumsumbua Mungu.” Watu wengine hutiwa sumu na hili, wakidhani kwamba hili linaeleweka kwa kina, "Hiyo ni kweli, acha pia nichunguze mimi ni wa roho ya aina gani pia." Anakuwa mwenye kufadhaa kwa sababu analenga sana roho, anachunguza kila kitu anachofanya, hatimaye akigundua suala ni nini: Je, mbona siku zote mimi huenda kinyume na ukweli katika ushughulikiaji wangu wa mambo? Je, mbona mimi sina ubinadamu au akili? Lazima niwe roho mbaya. Kwa kweli, mwanadamu hana asili nzuri na hana ukweli, kwa hivyo mwanadamu anawezaje kufanya tendo lolote zuri? Haijalishi jinsi inavyoonekana vizuri kwa nje haifai ukweli na bado inampinga Mungu. Mwanadamu si mzuri kwa asili, tayari amepotoshwa na kutengenezwa na Shetani kiasi kwamba hana sura yoyote ya sifa muhimu za kibinadamu, daima akiasi dhidi ya na kumpinga Mungu, ameenda mbali sana kutoka kwa Mungu; haiwezekani kwa mtu kufanya chochote ambacho kinapatana na mapenzi ya Mungu, na hakuna kitu chochote katika asili ya mwanadamu kinachoweza kukustahili na Mungu. Hili ni dhahiri. Watu wengine daima ni wenye kufadhaa: "Aa, mbona siku zote ninafanya mambo vibaya, mbona kila mara ninaendelea kufanya mambo ya kipumbavu, na nikijikejeli? Je, ni kwa sababu kuna kitu kibaya na roho yangu?" Akilenga sana masuala ya roho, na kuweka kando mambo ya asili yake mwenyewe, mtu huyu anashikilia mambo madogo na kukosa vitu muhimu. Akiweka kando mambo ya utendaji wakati anashikilia mambo ya mbinguni, si huu ni upumbavu? Je! Umeshikilia jambo hili la roho baada ya uchunguzi wa miaka hii yote? Je! Umeshikilia suala la nafsi? Je! Roho yako inaonekanaje, umewahi kuiona kwa macho yako mwenyewe? Hujishughulishi na kutafuta katika mambo ya asili yako mwenyewe ambayo yamezikwa ndani kwa kina katika nafsi yako, na badala yake kupoteza muda wako kutafuta namna roho yako ni ya aina gani. Je, una ushahidi wa chochote ulichopata? Je, si wewe ni mtu kipofu anayewasha mshumaa, ukipoteza tu nta? Unakataa kupata suluhisho kwa matatizo yako halisi, badala yake unaendelea kujihusisha katika vitendo vibaya na vilivyopotoka, unaendelea kuisoma aina ya roho ambayo wewe ni wake; maswali kama hayo hutatua matatizo gani? Ukiamini katika Mungu, lakini bila kushiriki katika kazi aminifu, daima ukiisoma roho, kama mtu mwenye wazimu. Mtazamo wa mtu mwerevu kweli unafaa kuwa: Sijali kile ambacho Mungu anafanya, au jinsi Mungu ananitendea mimi; sijali nimepotoka kwa kina kiasi gani, au ubinadamu wangu ni wa jinsi gani; sitayumbayumba katika kufuata kwangu kwa ukweli na kufuata kwangu katika kumjua Mungu. Huu ni mwelekeo wa maisha, hili ndilo ambalo mwanadamu anapaswa kutamani kufikia, hii ndiyo njia pekee ya wokovu. Sasa kuufuata ukweli tu ndilo jambo la busara, ni ufahamu tu wa asili yako potovu ndilo jambo la busara, ni uwezo tu wa kumridhisha Mungu ndilo la busara, ilhali uchunguzi wa mambo hayo yote ambayo huwezi kugusa wala kuona ni kupoteza muda. Mradi unaishi katika mwili, lazima uwe na hamu ya kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Kubainisha kama mtu amepagawa na roho mbaya, yote yanategemea na kama akili ya mtu ni ya kawaida katika kufanya mambo; kama si ya kawaida, basi hakuwezi kuwa na wokovu. Sasa hisia zenu ni za kawaida, unazungumza kwa kawaida sana, na hakuna kitu cha kimwujiza na kisicho cha kawaida kimetukia kwako; hata ingawa wakati mwingine hali yako si ya kawaida hasa, hiki tu ni kile ambacho asili ya binadamu hufunua. Matendo yako yanaweza kuwa si sawa wakati wote, lakini hayo pia ndiyo asili ya binadamu inafunua. Ni sawa kwa watu wengine pia, lakini msingi tu na mpangilio wa muda ambao vitu kama vile vinafunuliwa vimekuwa tofauti kwao. Kwako, inaonekana kama kila mtu mwingine anafanya mambo yanayofaa, lakini huu ni utambuzi uliokosea wa wanadamu. Mnahisi kwamba nyinyi sasa mna kimo fulani, mmekabiliwa na maneno na mambo mengine kuhusu roho, na kisha mliyatumia mambo hayo kwa kujichunguza wenyewe, kana kwamba ninyi ni watu muhimu. Hata daktari wa theolojia hawezi kuelewa mambo ya roho, Mungu pekee ndiye Aliye na ufahamu wa jambo hilo, kwa hivyo wanadamu wanawezaje kuona katika hili kwa wazi? Je, si ni rahisi kwa wanadamu kwenda katika njia mbaya? Hii ni kawaida kwa watu siku hizi. Hata ingawa hujakuwa ukifanya majadiliano ya uzito kuhusu mambo kama hayo, ingawa hujawa mdhaifu au kujikwaa kwa sababu ya jambo hili, lakini kwa wakati mmoja, kile ambacho watu wengine walisema kimekuathiri. Hata ingawa huko makini sana na mambo hayo, bado yako ndani yako, na kisha siku inapokuja ambapo umefanya kosa kwa kweli, unapopigwa, unapoanguka, utajishuku: Je, ni kwa sababu pia kuna kitu kibaya na roho yangu? Kwa kawaida, huwa hujishuku, na unawaona wengine kuwa wapumbavu, ukiangalia wanavyokwama wote. Kisha siku inakuja ambapo unashughulikiwa, au wengine wanasema kuwa wewe ni Shetani, roho mbaya. Utaamini hilo pia, utakwama pia na hutaweza kujinasua. Kwa hakika, watuwengi ni wepesi wa kufanya kosa lili hili, wanaona mambo ya roho kama muhimu hasa huku wakiweka kando masuala ya asili yao, ambayo inawafanya kuwa mbali kabisa na ukweli. Huku ni kupotoka katika uzoefu. Ninyi nyote mnapaswa kulenga kujua ni vipengele vipi vya asili yenu bado vinavyowasababisha kwa urahisi kufanya makosa na kwenda katika njia mbaya, na kisha kupata mafunzo kuanzia kwa msingi huu. Hasa katika kumtumikia Mungu, kwa uzoefu wenu wenyewe, kwa kujua asili yenu wenyewe, lazima mfikie ufahamu wa juu hatua kwa hatua, na hivyo basi kuchukua udhibiti kwa hali zenu wenyewe na kuendelea katika njia sahihi. Ikiwa unaweza kuwa na ukweli huu kama maisha yako ya ndani, basi utakuwa imara zaidi sana. Hutakuwa tena mwepesi wa kusema vitu ambavyo huelewi, utakuwa unagonga ndipo unapozungumza, na pia utakuwa unawasiliana mambo ambayo ni ya utendaji. Kadri mtu anavyoelewa asili yake mwenyewe kwa ndani zaidi, na kadri anavyouelewa ukweli zaidi, ndivyo atakachokuwa akisema kitakuwa na kipimo zaidi, na hatazungumza tena upuuzi. Mtu asiye na ukweli daima ni mpumbavu, anathubutu kusema kitu chochote. Wanapohubiri injili, ili kuwapata watu wachache zaidi, wengine wangeweza hata kwenda kwa kiwango cha kulipa gharama ya kufuru; watu hawa hata hawajijui wao ni nani, hawajui asili yao wenyewe, hawamwogopi Mungu. Watu wengine wanafikiri kuwa mambo kama hayo sio ya kutisha vile, lakini je, mambo haya si jambo lolote kubwa kweli? Hadi siku moja wanapotambua uzito wa suala hilo, kisha wanapatwa na hofu kweli; haya si masihara! Ikiwa huwezi kuelewa kiini cha suala hili, basi unaelewa nini? Bado unahisi kuwa wewe ni mwerevu sana, kwamba unaweza kuelewa kila kitu, lakini huna habari kwamba umemkosea Mungu tayari, na huna habari ya jinsi unaenda kuangamia. Hata kama una ufahamu kamili juu ya mambo ya kuzimu na ulimwengu wa kiroho, lakini ikiwa bado huna ufahamu wa asili yako mwenyewe, basi jitihada zako zote zimepotea. Sasa, la muhimu ni kutatua masuala ya asili yako. Lazima uwe na ufahamu kamili kuhusu kila kitu ambacho asili yako inafunua. Ikiwa huwezi kuelewa hili, ufahamu wako wote ni jitihada zilizopotea. Ikiwa huwezi kuelewa hili, hakuna faida katika kuchunguza wewe ni wa roho ya aina gani. Kitu muhimu ni kuwa na ufahamu kamili juu ya mambo yote ambayo kwa kweli huwepo ndani ya asili ya mtu. Bila kujali aina ya roho ndani yako, bado wewe ni mwanadamu, una mawazo, ubongo wako unafanya kazi kwa kawaida, na kwa hivyo unapaswa kujaribu kuuelewa ukweli na kuukubali ukweli. Ikiwa unaweza kuuelewa ukweli, basi unapaswa kutekeleza matendo yako kulingana na ukweli; huu ndio wajibu wa mwanadamu. Masomo yako ya roho hayawezi kukusaidia kwa vyoyote vingine. Kwa mtu ambaye amefunuliwa kuwa roho mbaya anafanya kazi kwake, anapokuwa wa kawaida mara chache, anaweza kuelewa ikiwa unawasiliana ukweli pamoja naye, na anaweza hata kuwa na uzoefu mdogo wakati mwingine, ilhali hii sio kweli kwa wale wenye hisia zisizo ya kawaida, ambao wamepagawa na mapepo kabisa. Isipokuwa kwa watu hawa, kwa wale walio na hisia ya kawaida, bila kujali aina ya roho ndani yao, bila kujali kiwango chao cha elimu, mtu yeyote aliye na ufahamu wa roho hata mdogo anaweza kuelewa ukweli fulani, na hiyo inatosha. Mtu hana kiungo ambacho kinaweza kupokea ukweli, lakini mtu anaweza kuusikiliza ukweli, mawazo ya mwanadamu bado ni muhimu kwa mujibu wa mafundisho ya ukweli, na hili ndilo mwanadamu anaweza kufanikisha. Kwa hivyo, hakuna haja tena kwako kujifunza wewe ni wa roho wa aina gani. Sasa suala si kujaribu kuelewa wewe ni wa roho ya aina gani; ikiwa hii roho yako ina uwezo wa kuukubali ukweli, ikiwa hii roho yako ni roho inayomwamini Mungu, haya si muhimu. La muhimu ni kama wewe, kama mwanadamu, unaweza kuukubali ukweli, kama wewe ni mtu anayeutafuta ukweli, kama wewe ni mtu anayeweza kuwa na ufahamu thabiti wa hali zako mwenyewe, kama wewe ni mtu ambaye anaelewa asili yako mwenyewe, na haya ni muhimu. Masomo yako ya aina ya roho uliyo nayo si ya maana, na zaidi ya hayo, hayana thamani. Ikiwa utaendelea kuchunguza roho yako ni ya aina gani, kuendelea kuchunguza kinachofanyika katika nafsi yako, kile roho yako inafanya, matokeo ya roho yako ni nini, jinsi itakavyokuwa wakati ujao, basi utachelewesha mambo yaliyo muhimu kweli. Hata kama una uchunguzi wa kina wa mambo kama hayo, siku moja ambapo wengine wamekwisha kuuelewa ukweli na kuingia ndani ya uhalisi, utakuwa umechelewesha mambo muhimu badala yake, utakuwa tayari umejichimbia ndani ya shimo. Huku kutakuwa kwenda katika njia mbaya, kukitapanya imani yako kwa Mungu, bila kitu chochote cha kuonyeshea. Unaenda kumlaumu nani iwapo siku hiyo itakuja?