Sura ya 49. Unapaswa Kuutumia Ukweli Kumaliza Hali Yako Hasi

Watu wengi wana hali hizi ambazo tumejadiliana hapo awali, hata ingawa si wazi kama hapo awali. Hii ni kwa sababu watu hawakuwa na ufahamu wowote wa ukweli wakati huo, na hawakuelewa chochote. Siku hizi, unasikiliza zaidi, na kwa kiwango cha chini kabisa, nyote mnaelewa baadhi ya mafundisho. Hata hivyo, una hali fulani zilizojikita ndani ambazo hazijafunuliwa. Una uwezo wa kuuona upotovu kwa wazi ambao mara nyingi hufunuliwa na kuwa na ufahamu mara tu unapofunuliwa; unajua asili ya malengo yako yaliyofunuliwa, maneno, na vitendo. Lakini sasa hivi, hujui mambo yaliyo ndani yako, mambo yaliyofichwa zaidi na vitu vinavyowasilisha asili ya kibinadamu. Wakati mwingine, hata kama una ufahamu fulani, huhisi kwamba mambo hayo si sahihi; wakati mwingine unatambua tu kama kufanya jambo hili ni sawa au sio sahihi, lakini bado huwezi kulitofautisha wazi. Hii ni kwa sababu huko wazi kuhusu ukweli. Kuna mchakato unaohusika ili kufikia ufahamu wa kweli. Bila kujali kama watu ni wazee au wapya, kwa hakika hawaulewi ukweli sasa, na hawajafikia kiwango cha ufahamu wa wazi. Wanajua tu maneno machache ya mafundisho, au kufuata sheria chache tu na kisha kuachia hapo. Hii ni kwa sababu watu wana hali ndani mwao ambazo zinawazuia kuingia ndani, wote wanadhibitiwa na hali zao ndani, na hawana kiini cha neno la Mungu kama maisha yao. Watu wenyewe hawana uwezo wa kugundua vitu vinavyobuniwa kutoka katika asili zao, na kwa kutoweza kugundua hili, huwafanya wafikirie kuwa wamebadilishwa kwa kiasi fulani na kuwa na kimo fulani kwa kufuata sheria tu, kuzungumza juu ya mafundisho fulani na kuonyesha tabia chache nzuri, na wanadhani kwamba hayo yanapaswa kutosha kumridhisha Mungu. Mawazo haya yanathibitisha kuwa wao ni wa kina kifupi na hawana kimo cha kweli.

Hata ingawa hali fulani ambazo watu wanazo ndani sio mawazo dhidi ya Mungu, sio hasi, na watu wanadhani kuwa ni sahihi hasa na zinazofaa, kwa kweli ni matokeo ya asili ya kibinadamu. Katika hatua fulani, ingawa watu wana kimo fulani, mambo hayo bado yako ndani yao. Hili haliepukiki, na labda kwa wakati fulani, mambo haya yatatoka kwa nguvu. Hayawezi kuepukika. Watu wana ufahamu fulani, lakini hawazitofautishi hali hizi wazi, na hawajui ikiwa hali hizi ni sawa au sio sahihi; hata wao hujiuliza kwa mioyo yao kwa nini hawakuzitambua. Inaonekana kama jambo lisilowezekana hasa. Hili ndilo linalowafanya watu wawe wagumu zaidi kushughulika nao. Majeraha ya nje ya ngozi yanaweza kutibiwa kwa urahisi, lakini magonjwa katika damu ambayo watu hawawezi kuyaona si rahisi kuponya. Lazima watoe damu na kuipima ili kujua. Mambo ambayo yamekita mizizi ndani ya watu na vitu vinavyobuniwa kutoka kwa asili ya kibinadamu ni mambo ambayo watu hutegemea ili kuishi. Kwa hivyo, watu wanahisi kwamba vitu vinavyoubuniwa kutoka kwa asili ya kibinadamu ni sahihi. Ni kana kwamba watu wanapaswa kuwa namna hii na kuwa na hiki au nia, mahitaji na matamanio ya aina hiyo. Hakuna hata mtu mmoja anayeelewa kwamba ukweli ni ukweli, kila kitu kinachobuniwa kutoka kwa asili ya binadamu ni kipotovu, na yote ni kinyume na ukweli. Watu hawawezi kuelewa hili na hawana ufahamu kulihusu. Hasa watu siku hizi ​​wanaweza kuzungumza kwa uwazi kwa kiasi fulani juu ya mafundisho fulani rahisi, na kuwa na kimo kidogo na uzoefu, na wanaonekana kuwa wasiojali ikiwa ni wachafu kidogo, na wanafikiri kwamba huu ndio msingi ambao wanapaswa kuamini kwa Mungu na kumfuata Mungu. Kweli, hili ni kosa kubwa mno. Watu hawapaswi kuchanganya kile wanachofikiri kuwa sawa na ukweli au kuufuata ukweli kwenye msingi wa kosa. Ukweli sio mchafu. Kwa sasa kuna watu wengi ambao wanajitia moyo, na wanautafuta ukweli kwa msingi wa kutarajia siku ya Mungu na kubadilika kwa Mungu. Wanahisi kuwa kutafuta kwa njia hii ni sawa na njia ya hatua ni sahihi, lakini hatua yao ya kuanzia ni mbaya kimsingi na kila kitu kinachozaliwa kutoka kwa hatua ya kuanzia isiyo sahihi kitakuwa daima kisicho sahihi. Bila kujali ni hatua gani ambayo watu wapo, ikiwa hawawezi kuelewa hali ya aina hii ndani yao na hawawezi kuibadilisha, basi ni kama mradi wa uhandisi usio wa maana bila kujali jinsi wanavyotafuta. Ikiwa mwanzo wa mtu si sahihi na msingi wake si sahihi, basi karibuni au baadaye mradi wake utaanguka na hautaweza kusimama. Mtu wa aina hii karibuni au baadaye atakuwa katika hatari. Je, mnayaelewa maneno haya? Kwa nini kuna watu wengi waadilifu ambao hawawezi kuikubali njia ya kweli?Kwa sababu imani yao kwa Mungu ina dosari kimsingi; hawaukubali ukweli na wanaondolewa na Mungu. Katika familia ya Mungu, kuna baadhi ya viongozi ambao hali zao ni mbaya na wana uchafu mwingi ambao hawajautatua. Kuwapogoa na kuwashughulikia hakuna maana, na hatimaye, magonjwa yao ya kale yanajitokeza tena, yanafunua kabisa asili zao za kweli na yanaondolewa. Hali fulani ambazo watu wanazo ni kama saratani:Ikiwa haitatibiwa mapema, basi karibuni au baadaye lipuka na watu watapoteza maisha yao.

Katika kila hatua, hali za watu zinalingana moja kwa moja na kiwango ambacho wameingia na kiasi ambacho wamepata. Wakati hali za watu ni ya kawaida kwa ulinganisho, basi wanaweza kuelewa na kuingia katika ukweli fulani na kuelewa mambo fulani halisi ya kweli kulingana na maneno ya Mungu, na wanaweza kuwatolea na kuwatumikia wengine. Hali za watu wengine si sahihi, na hata ingawa wanawafuata wengine katika kutafuta, na pia wanasoma, kusikiliza, na kuwasiliana, wanaishia kupata kiasi kidogo zaidi kuliko watu wenye hali ya kawaida. Ikiwa daima kutakuwa na uchafu wa kibinadamu, ufunuo wa hali potovu, na uchafuzi wa mawazo na fikira za watu, basi watu lazima wamefunikwa kabisa na ukosefu wa uwazi ndani yao. Je! Hili linakosaje kuathiri kuingia kwa mtu katika ukweli? Ni watu wenye akili timamu pekee ndio wanaoweza kuuelewa ukweli, ni watu wenye mioyo safi pekee ndio wanaoweza kumwona Mungu; ni kwa kuyaondoa mambo yaliyo ndani yako tu ndipo unaweza kuupata ukweli kwa urahisi. Wakati mioyo ya watu iko katika msukosuko, si rahisi kuuelewa ukweli. Ni watu ambao wanaelewa ukweli pekee ndio wanaoweza kuona ndani ya hali zao wenyewe kwa kiasi fulani, na ni kwa kuona ndani ya kiini cha matatizo yake tu ndipo mtu anaweza kuielewa asili yake wenyewe. Ikiwa hali za watu ndani ni sahihi na za kawaida kabisa, basi wana hali ya kweli; hawana uwezekano wa kuteleza au kulalamika wakati mambo yanapowajia. Namna unavyotafuta katika kila hatua na hali ambayo unatafuta ni mambo ambayo huwezi kutojali. Kutojali hatimaye kutaleta shida. Wakati hali yako ni ya kawaida, utatembea katika njia sahihi na kufanya mambo kwa usahihi na utaingia kwa haraka katika maneno ya Mungu. Ni kwa kutafuta maisha kwa njia hii tu ndipo unaweza kukua.

Kuna hali nyingine ambayo watu wanayo ndani ambapo wanasoma maneno ya Mungu kwa miaka michache na kupitia ushughulikiaji na kupogoa; wanaweza kuachilia kidogo nia zao za kupokea baraka; mioyo yao inalegea zaidi, na hawatafuti kupata baraka; mioyo yao ni ya kukubali, na wanamtii tu mipango ya Mungu, vichwa vyao vimeinama kidogo, na chochote ambacho Mungu anafanya ni sawa kwao. Hali hii pia si sahihi. "Chochote ambacho Mungu anafanya ni sawa, kwa hali yoyote, sitaomba baraka. "Watu wenye hali ya aina hii wanaonekana kuhisi kwamba kufuata mipango ya Mungu ndiyo yote wanayohitaji kufanya. Nakuuliza:"Je! Kweli unatii mipango ya Mungu?Je! Kweli unamiliki ukweli wa kipengele hiki? "Je! Kweli utajiwasilishaje bilakimo cha kweli? Bado unafikiri kuwa unatii mipango ya Mungu! Siku hizi mtazamo wa watu wengine ni: Sijali kuhusu kupata baraka au kupata maafa. Mungu anaweza kufanya vyovyote Atakavyo! Hii ni hali mbaya kabisa na isiyojihusisha; hawautilii ukweli maanani, wakisema, "Kwa hali yoyote ni mipango ya Mungu, na hatimaye, Mungu ataamua hatima yetu. Hatuwezi kuamua chochote, hivyo njia yoyote tunayotafuta ni sawa. "Huku ni kulegea bila kutenda, na kwa kidhahania hakuna jitihada zilizowekwa. Je! Watu ambao wana hali ya aina hii wanaweza kuendelea? Wanaweza kutosheleza mahitaji ya Mungu?

Kuwa na mabadiliko ya mawazo ni muhimu katika kufuata kuingia; hali yako ikibadilika, na hakuna kitu kinachokuzuia, basi unaweza kutafuta kwa ufanisi. Ikiwa watu wanaweza kuingia katika ukweli kwa kutafuta kwao au la au kiasi gani cha nguvu walicho nacho katika kutafuta kwao kunategemea kabisa jinsi hali yao ilivyo. Ikiwa hali ya watu ni ya kawaida, basi watakuwa na nguvu katika kutafuta kwao. Ikiwa watu kamwe hawana nguvu, ikiwa hawana joto wala baridi katika kufuata, basi bila shaka hali yao ndani haitakuwa ya kawaida, lazima kuwe na matatizo ndani, na hakika wamezuiwa na kitu: Wanamwamini Mungu lakini hawana maono na hawajui jinsi ya kutafuta; au wamepoteza Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani yao na hawana mwanga wa ukweli; au wana mtazamo mbaya na wamepoteza imani ya kweli. Haya yote ni uwezekano. Najua kwamba kuna watu fulani ambao daima wanafadhaika; daima wanahisi kuwa kuna matatizo na roho zao: "Kwa nini mimi daima hufanya mambo mabaya? Kwa nini mimi daima hufanya makosa? Je, ni kwa sababu nina roho mbaya ndani? Ikiwa kuna roho mbaya anayefanya kazi ndani yangu, basi sijamalizwa mimi? "Watu ambao wamekuwa na kazi isiyo ya kawaida ya pepo wachafu ndani yao hasa ni rahisi sana kuzuiwa katika mambo haya. Ni hatari sana kwa moyo daima kuwa na wasiwasi, na ni rahisi zaidi kwa Shetani kuwatumia na kufanya hofu zao ziwe kweli. Hii ndiyo hali ngumu zaidi kukabiliana nayo. "Kama roho za watu si sahihi, basi wameangamia. Roho huamua kila kitu. "Kuna baadhi kati yenu ambao wako katika hatari ya kufikiri kwa njia hii. Jambo hili linakuwa kizuizi chao, na hali hii inaweza kusababishakuharibikiwa akili na hawatakuwa na uwezo wa kuendelea kuamini. Hali ya aina hii ni ya hatari zaidi, na inapaswa kutatuliwa haraka iwezekanavyo. Pia kuna baadhi ya watu ambao wana mawazo ya kipumbavu katika mioyo yao; wao daima huwaza: Kwa kuwa ni Mungu ambayehuwajaalia na kuwachagua watu, na Mungu ndiye Anayeamua kila kitu, basi tunatafuta nini? Wao watazama ndani ya hali hii na hawataweza kutoka, na hawatawasikiliza watu wengine wakati wanaposhirikiana nao; watasema, "Ninaelewa haya yote, siwezi tu kuikwepa. "Katika siku hiyo wanapofahamu kweli, watajionea majuto, "Niliwezaje kuwa mjinga wakati huo? Mimi ni mpumbavu kweli! "kwa kweli, kila mtu ana hali isiyo ya kawaida ndani; asili ya kila mtu hubuni kitu tofauti kulingana na mazingira na asili tofauti. Asili za watu ni sawa, lakini kwa sababu mazingira na asili zao ni tofauti, au kwa sababu kazi wanayofanya ni tofauti na nafasi zao ni tofauti, wanazalisha hali tofauti. Hata hivyo, tabia za jumla za asili za watu ni sawa. Wakati mazingira yanapokuja juu yake, hali ya aina hii inazalishwa; wakati mazingira yanakujia, basi hali ya aina hiyo inazalishwa. Watu wengine hujikwaa juu ya suala hili, watu wengine hujikwaa juu ya suala lile, watu wengine huwa hasi katika suala hili, watu wengine ni wadhaifu katika jambo lile. Mwishowe, wanapomwomba Mungu, inaonekana ni kama Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao, na hali nyingine hujitokeza ndani:"Ikiwa Roho Mtakatifu hafanyi kazi na Mungu ameniacha, basi mimi sijaangamia? Basi ni heri nisiamini; ninaamini, lakini sipokei kitu chochote. Mungu hafanyi kazi ndani yangu, kwa hivyo sijaondolewa? "Hali nyingine kama hii inatokea, na ugonjwa wa zamani unabaki wakati mpya unakuja. Wakati watu wanapaswa kufa, hakuna kitu cha kuwaokoa. Watu ambao wana uwezo wa kurudi kwenye njia sahihi ni wa maana sana, yaani, yeyote asiyepaswa kufa ataokolewa daima. Wakati watu wamepotea katika njia yao, wanaweza kuamka na kutambua kwamba hali zao si za kawaida, wanaweza kuhisi kwamba wako katika hali za hatari; na wanaweza kufanya kila kitu katika uwezo wao kujiondoa na kurudi katika hali ya kawaida. Watu wenye kimo cha aina hii ni wachache sana. Kwa nini nasema kuwa watu hawana kimo? Kwa sababu huoni wazi, hujui, au hata hutambui ni hali ipi itasababisha matokeo yapi. Kwa hivyo, watu daima wanakuwa wadhaifu na hasi wakati mambo fulani yanawajia, na inakuwa rahisi kwao kuanguka. Kuwa na kimo kunamaanisha nini? Ikiwa huwezi kudhibiti hisia zako, ikiwa huwezi kuishi katika hali ya kawaida mara kwa mara, na huwezi kuona wazi hali yako isiyo ya kawaida, basi huna kimo. Kuwa na kimo ina maana kwamba unaelewa ukweli fulani na ukweli umekuwa maisha yako na msaada wako na msingi wa kuwepo kwako. Bila kujali kinachokujia, unaweza kuishi kulingana na ukweli, utakuwa na uwezekano mdogo zaidi wa kuwa mdhaifu na kuanguka, na uwezekano mdogo zaidi wa kuzama katika hali zote za hatari. Huku ni kuwa na kimo. Je, watu wanaweza kupata hali hii kwa sasa? La, hawawezi! Watu wengi huwa hasi na wadhaifu, wote wamezama katika hali ambayo hawawezi kutoka ndani kwa urahisi. Hata kama wangeweza kutoka ndani yake baadaye, hawangejua ni nini kilichokuwa kikiendelea, na hawangejua ni hali gani yao haikuwa sahihi. Wakati jambo hilo linajitokeza tena kwao, watateleza tena na kupotea, na ugonjwa wa zamani unarudi. Wao ni wadhaifu na wamekwama katika kila jambo linalowajia. Ikiwa watu wanawasiliana nao na watafakari, wanaweza kuamka, lakini bado hawawezi kuelewa hali zao kikamilifu au kufahamu ufunuo wa asili zao. Hatimaye, hawataweza kubadilika almradi uzoefu walio nao; wanaanguka wakati jambo hili linawajia, nao huwa wadhaifu wakati jambo hilo linawajia. Ikiwa wanakabiliwa na matatizo yoyote, basi wanataka kuziacha kazi zao; wao wako hasi mara nyingi zaidi kuliko walivyo kawaida na mara nyingi hupoteza Roho Mtakatifu Anayefanya kazi ndani yao. Hii ni hali halisi ambayo kila mtu anayo. Bila kujali kama watu wanaweza kudhibiti hali zao au la, bila kujali kama wanaweza kuthibitisha kwamba wanaishi katika hali ya kawaida au la kunategemea kabisa kiwango cha ukweli ambacho wameingia ndani yake. Kutoka kwa hili tunaweza kabisa kuona kimo cha kweli cha watu. Watu wengine husema: "Ninahisi kuwa niko na kimo kidogo kuhusiana na kujiwasilisha kwa Mungu. "Unahisi kuwa una kimo kidogo, lakini kwa hakika, hali yako ya sasa si duni sana, au haina tishio kwako, au sio hali ya uchungu sana, na unaweza kujiwasilisha kwa mipango ya Mungu. Je, ingekuwa chungu kwa kiwango fulani? Bado ungeweza kujiwasilisha kabisa? Ikiwa maumivu yangekuwa yasiyostahimilika kama yale ya Ayubu, basi ungeweza kujiwasilisha kwa mipango ya Mungu? Hili ndilo suala na kimo. Kwa hivyo, wakati mazingira ni mazuri, unahisi: Ninaweza kujiwasilisha kwa mipango ya Mungu, naweza kujiwasilisha kwa mipangilio ya Mungu, nina nia na azimio la kufuata hadi mwisho na kuyatosheleza mapenzi ya Mungu na kushuhudia kwa ajili ya Mungu kama Ayubu. Unahisi kwamba una dhamira hii, lakini wakati kitu kikubwa zaidi kuliko mazingira haya kinakujia, wakati majaribio makubwa yanapokujia, na wakati mateso makubwa yanapokujia, utaweza kusimama imara? Je, unajua? Je, unaweza kutabiri hili? Si watu wengi wanaojua kwa hakika wao ni nani, kwa sababu hakuna yeyote aliye na ukweli, na hawawezi kujijua wenyewe kwa kweli.

Iliyotangulia: Sura ya 48. Ni kwa Kuzielewa Hali Zako tu Ndipo Utakapoweza Kutembea Katika Njia Sawa

Inayofuata: Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki