Sura ya 34. Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu. Je wewe hutenda vipi wakati watu walio chini yako wanakurai na kukupa sifa kwa matokeo unayozalisha katika kazi yako? Je wewe hutenda vipi wakati watu wanakupa mapendekezo? Je, wewe huomba mbele ya Mungu? Mnasali wakati mna mambo na matatizo, lakini je, mnasali wakati hali zenu ni nzuri, au wakati mnahisi mmekuwa na mkutano wa mafanikio? Kwa hivyo wengi wenu huwa hamsali! Kama umekuwa na mkutano wenye mafanikio, unapaswa kutoa sala; unapaswa kutoa sala ya sifa. Mtu akikusifu, na wewe unakuwa na kiburi, ukihisi kama uliye na ukweli, basi utaanguka katika hali isiyo sawa, lakini moyo wako bado utakuwa na furaha, na hutakuwa na sala ya sifa, na hata zaidi hutakuwa na sala ya shukrani. Matokeo ya wewe kuanguka katika hali hii ni kwamba mkutano wako unaofuata utakuwa wa kuchosha, hutakuwa na maneno ya kusema, na Roho Mtakatifu hatafanya kazi. Watu hawawezi kufahamu hali zao wenyewe, wao hufanya kazi kidogo na kisha kufurahia matunda ya kazi zao. Katika hali mbaya, ni vigumu kujua ni siku ngapi watahitaji ili wapate afueni. Hali ya aina hii ndiyo hatari zaidi. Nyote huomba wakati mna jambo au wakati hamuoni mambo kwa uwazi, mnaomba wakati mna mashaka na wasiwasi juu ya kitu au tabia zenu potovu zimefichuliwa. Nyinyi huomba tu mnapokuwa mnahitaji kitu. Lazima pia uombe wakati una mafanikio katika kazi yako. Wakati unapata matokeo fulani katika kazi yako, unapata msisimko, na mara umepata msisimko, wewe huombi; wewe daima huwa na furaha na daima umenaswa kwa ndani. Baadhi yenu wakati huu mnapokea nidhamu: Unapoenda nje kufanya ununuzi, unagonga mwamba na kitu kinakuendea vibaya; muuza kwenye duka anasema maneno mengi makali ambayo yanakufanya uhisi usiye mtulivu na uliye na mkazo, na bado hujui kwa njia ipi umekosea Mungu. Kwa kweli, mara nyinyi, Mungu anatumia mazingira ya nje kukufundisha nidhamu; kwa mfano, Anatumia mambo kama mtu asiyeamini kukugombeza wewe, au kufanya pesa zako kuibiwa ili kukufanya asiye mtulivu. Mwishowe, utakuja katika uwepo wa Mungu kuomba na wakati unaomba, baadhi ya maneno yatatoka nje. Wewe utakuja kutambua kuwa hali yako haikuwa sahihi, kwa mfano, ulikuwa umeridhika na kupendezwa na wewe mwenyewe..., basi utahisi kuchukizwa na kuridhika kwako mwenyewe. Pamoja na maneno katika sala yako, hali isiyo sahihi ndani yako itageuka. Mara tu baada ya kuomba, Roho Mtakatifu atafanya kazi kwako; Atakupa aina ya hisia na kukufanya utoke kwenye hali isiyo sahihi. Maombi siyo tu kuhusu kuuliza na kuuliza, wala si kuhusu kumtafuta Mungu wakati wewe una njaa; kama huna njaa, je hauhitaji kuomba? Ukiwa umeshiba, lazima pia uombe.

Je, mmegundua kwamba mkienda muda mrefu bila kuomba, hata kama mna nguvu na hamko hasi, au mhahisi kama mna hali mahususi ya kawaida ndani , mtahisi kama mnafanya mambo wenyewe na hakuna matokeo katika mnalofanya? Mimi Nimesema awali: "Watu wanajihusisha na mambo yao wenyewe na kufanya jambo lao wenyewe.” Siku hizi, watu hawaombi wanapofanya kazi; Mungu hayuko katika mioyo yao hata kidogo, na wanafikiri: "Mimi nitafanya tu kwa mujibu wa mipango ya kazi na katika hali yoyote sitafanya jambo lolote baya au kuvuruga chochote....” Hukuomba na zaidi ya hayo hukutoa shukrani. Hali hii ni mbaya! Mara nyingi, unajua kwamba hali hii si sahihi, lakini huna njia sahihi ya kurekebisha, na kwa sababu hii, huwezi kugeuka. Hata kama ungeelewa ukweli, hungeweza kuuweka katika vitendo; hata kama ungeelewa hali yako mbaya ya ndani (kuwa na kiburi, mpotovu, na muasi), hungeweza kuirekebisha au kuikomesha. Watu wanajishughulisha na mambo yao wenyewe na hawako makini na kazi au shughuli ya Roho Mtakatifu. Wao wanajali tu kuhusu masuala yao wenyewe na kwa sababu hiyo, Roho Mtakatifu anawatelekeza. Baada ya Roho Mtakatifu kuwatelekeza, watahisi wenye giza na wakavu; hawatapokea chakula au furaha hata kidogo. Watu wengi tu huomba mara moja kila nusu mwaka. Wao hutunza mambo yao na kufanya kazi yao, lakini wanahisi goigoi, wakati mwingine wakifikiri: "Ninafanya nini, na hili litafika mwisho lini?” Hata mawazo haya yatajitokeza. Kutoomba kwa muda mrefu ni hatari sana! Maombi ni muhimu sana! Maisha ya kanisa bila kuomba kamwe hufanya mikutano ya kuchosha na isiyosisimua. Kwa hivyo, wakati mko pamoja, lazima msali daima na kutoa sifa, na Roho Mtakatifu atafanya kazi hasa vizuri. Nguvu ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu ni isiyo na kikomo; watu wanaweza kuitumia wakati wote bila kuimaliza—daima inapatikana. Wakati wanajitegemea wenyewe, watu wanaweza kuwa na kipawa cha porojo, lakini kama Roho Mtakatifu hafanyi kazi katika hili, basi ni nini wanachoweza kukamilisha? Mara nyingi, watu huomba mara tatu hadi tano na neno moja tu au mawili, "Ee Mungu, nakushukuru , nakupa Wewe sifa," kisha hawana kitu kingine cha kusema, hawawezi kufungua midomo yao. Nieleze hiki ni kiwango gani cha imani; ni hatari sana! Sivyo? Watu wanaamini katika Mungu, lakini hawana hata maneno ya kumsifu au kumshukuru, na wao hawana maneno kumtukuza Mungu. Hata hawathubutu kutamka maneno "muulize Mungu," wanaona aibu sana kusema hayo. Wao ni wapotovu sana! Licha ya ukweli kwamba unazungumza kuhusu Mungu na wewe unamkubali Mungu katika moyo wako, kama huji katika uwepo wa Mungu, na moyo wako uko mbali na Mungu, basi Roho Mtakatifu hatafanya kazi. Hasa nyinyi viongozi—hatutawataja watu walio chini—kila asubuhi mnapoamka, lazima muombe. Baada ya kuomba, siku yako itakuwa hasa nzuri na yenye kustawisha, na utahisi Roho Mtakatifu upande wako Akikulinda wewe wakati wote. Usipoomba kwa siku moja, au ukienda siku tatu hadi tano bila kuomba, utahijihisi hasa mpweke na mwenye ukiwa. Utawakumbuka wapendwa wako na msukumo wako na hamu yatakuwa kubwa hasa.

Sasa Nimepata kuwa watu wote wana tatizo: Wakiwa na jambo, wao huja katika uwepo wa Mungu, lakini sala ni sala na masuala ni masuala, na watu wanadhani kwamba hawapaswi kuzungumzia masuala wanapoomba. Ni nadra sana muwe na sala ya kweli, na baadhi yenu hata hamjui jinsi ya kuomba; kwa hakika, sala hasa huwa inahusu kusema yaliyo katika moyo wako, kama tu mazungumzo ya kawaida. Hata hivyo, baadhi ya watu huchukua nafasi zisizofaa wakati wanaomba, na bila kujali kama inakubaliana na mapenzi ya Mungu au la, wao hudai Mungu awape walichoomba. Kwa sababu hiyo, zaidi wanavyoomba ndivyo inavyozidi kukosa uchangamfu. Unaposali, chochote ambacho moyo wako unauliza, tamaa, na maombi, au wakati unataka kushughulikia baadhi ya mambo ambayo huelewi kikamilifu unamuuliza Mungu hekima, nguvu, au kukupa nuru, ni lazima uwe mwenye busara katika njia unaongea. Kama huna busara, na unapiga magoti na kusema: "Mungu, nipe nguvu na uniruhusu nione asili yangu; Nakuomba ufanye hivyo. Au, nakuomba unipe hiki au kile, nakuomba uniruhusu niwe hivi au vile..., "neno hili "kuuliza” hubeba kipengele cha nguvu, na ni kama kuweka shinikizo kwa Mungu kumfanya Afanye kile. Zaidi ya hayo, wewe unajiamulia awali mambo yako mwenyewe. Hata kama wewe huomba kwa njia hii, Roho Mtakatifu anaona ni kama: Kwa kuwa tayari umeshajiamulia awali mwenyewe, na wewe unataka kulifanya kwa njia hiyo, matokeo ya aina hii ya maombi yatakuwa nini? Unapaswa kutafuta na kutii katika maombi yako; kwa mfano, kama jambo lingekujia ambalo hujui namna ya kulishughulikia, kisha unasema: “Ee Mungu! Jambo hili limekujia , na mimi sijui jinsi ya kulishughulikia. Niko tayari kukuridhisha Wewe katika suala hili, niko tayari kukutafuta Wewe, nina hamu ya mapenzi Yako kutimika, ninatamani kufanya kulingana na mapenzi Yako, na si kulingana na mapenzi yangu mwenyewe. Unajua kwamba nia za mwanadamu ni ukiukaji wa mapenzi Yako; wao hupinga Wewe na hawafanyi kulingana na ukweli. Nina hamu tu ya kufanya kulingana na nia Zako. Nakuaomba unipe nuru na kuniongoza katika jambo hili, ili kwamba mimi nisikukosee Wewe....” Aina hii ya toni ya sauti katika sala inafaa. Kama wewe husema tu: "Ee Mungu, nakuaomba ufanye hili au lile; nisaidie na kuniongoza; niandalie mazingira ya kufaa na watu wa kufaa kwangu, ili kwamba niweze kufanya vizuri katika kazi yangu...,” wakati aina hii ya sala imeisha, bado hujui mapenzi ya Mungu ni nini, kwa sababu unajaribu kufanya Mungu afanye mambo kulingana na nia yako.

Sasa mnahitaji kufahamu kama mambo mnayosema katika maombi yenu ni ya maana au la. Bila kujali kama nyinyi ni wajinga au kama nyinyi mnaomba kwa makusudi kwa njia hii, ikiwa maombi yenu si ya busara, basi Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yenu. Kwa hivyo, mnapoomba, maneno mnayosema lazima yawe na busara, na toni yenu lazima iwe sahihi: “Ee Mungu! Unajua udhaifu wangu na Unajua ukaidi wangu. Mimi tu nakuomba tu Uweze kunipa nguvu, hivyo niweze kuhimili majaribu ya mazingira haya. Hata hivyo, wacha iwe kulingana na mapenzi Yako. Mimi nauliza hili tu na sijui ni nini mapenzi Yako, lakini natamani mapenzi Yako yafanyike; bila kujali kama Wewe hunitumia mimi katika huduma au unifanye kutumika kama foili[a], niko tayari kwa vyovyote. Hata hivyo, nakuomba nguvu na hekima ili viniwezeshe kukuridhisha Wewe katika jambo hili. Mimi nina nia tu ya kutii mipango Yako....” Baada ya wewe kuomba kwa njia hii, wewe utahisi ukiwa hasa imara. Kama unasisitiza tu kwa kuuliza na kuuliza, basi wakati umemaliza kuomba hakitakuwa kitu zaidi ya rundo la maneno matupu, kwa sababu tayari umeshajiamulia awali nia zako. Wakati unapiga magoti kuomba, unapaswa kusema kitu kama: “Ee Mungu! Unajua udhaifu wangu na Unajua hali zangu. Ninakuomba unipe nuru katika suala hili na uniruhusu nielewe mapenzi Yako. Ninatamani tu kutii mipango Yako na moyo wangu unatamani kukutii ....” Ukiomba hivi, basi Roho Mtakatifu atakuendesha na kama mwelekeo wa sala yako si sahihi, basi itakuwa isiyo changamfu na kavu, na Roho Mtakatifu hatakuendesha wewe; wewe unanong’ona tu, unaomba kimya kimya, au kufunga macho yako na kusema maneno machache unavyopenda, ambao ni uzembe tu. Kama wewe ni mzembe, Roho Mtakatifu atafanya kazi? Watu wanaokuja katika uwepo wa Mwenyezi Mungu lazima wote watende vizuri na kuonyesha uchaji. Tazama dhabihu za makuhani wakati wa Enzi ya Sheria, wote walikuwa wanapiga magoti. Maombi si jambo rahisi vile. Watu huja mbele ya Mungu, lakini bado ni wafidhuli na wasiokuwa na mipaka, na wanataka kulala kitandani mwao na kufumba macho yao. Hili halikubaliki! Sisemi mambo haya kuwahitaji watu wafuate baadhi ya sheria mahususi; katika kiwango cha chini zaidi, mioyo yao lazima imgeukie Mungu na ni lazima wawe na mtazamo wa uchaji mbele ya Mungu.

Sala zenu hukosa mantiki mara nyingi mno; zote zina toni hii ya sauti: “Ee Mungu! Kwa kuwa Wewe umenifanya kuwa kiongozi, lazima Ufanye kila kitu ninachofanya kiwe cha kufaa ili kazi Yako isikatizwe na maslahi ya familia ya Mungu yasipate hasara. Lazima Unifanye nifanye mambo kwa njia hii....” Je, hili ni muhimu? Sala hii si ya busara! Je Mungu anaweza kufanya kazi ndani yako unapokuja katika uwepo wa Mungu na kuomba bila busara hivi? Kama ungekuja mbele ya Kristo na uniongeleshe bila mantiki, je, Mimi ningekuzikiliza? Wewe ungetupwa nje! Je, si ni sawa na kuwa katika uwepo wa Roho na kuwa mbele za Kristo? Unapokuja katika uwepo wa Mungu kuomba, lazima ufikirie kuhusu jinsi ya kuzungumza kwa busara na kufikiri kuhusu kitu cha kusema ili uweze kuigeuza hali yako ya ndani kuwa uchaji, udhalilisho na unyenyekevu, kisha useme sala na utapakwa mafuta. Mara nyingi wakati watu wanaomba, wao hupiga magoti na kufumba macho yao na hawasemi lolote; wao husema tu, "Ee Mungu, ee Mungu!” Wao husema tu maneno haya mawili, wakiita kwa muda bila kusema kitu kingine chochote. Kwa nini iko hivi? Hali yako si sawa! Je, mna nyakati kama hii? Kulingana na hali yenu ya sasa ilivyo, mnajua mnachoweza kufanya na ni kwa kiasi gani mnaweza kukifanya, na mnajua nyinyi ni nani. Hata hivyo, mara nyingi hali yako si ya kawaida. Wakati mwingine, hali yako hurekebishwa, lakini hujui jinsi ilivyobadilishwa, na mara nyingi unaomba bila maneno yoyote, ukidhani kwamba ni kwa sababu huna elimu. Je, unahitaji elimu ndio uombe? Maombi si kuandika insha, ni kuzungumza tu kwa mujibu wa akili ya mtu wa kawaida. Tazama maombi ya Yesu (kutaja sala ya Yesu si ya kufanya watu kuchukua mwelekeo sawa na nafasi kama Wake), Aliomba katika Bustani ya Gethsemane: "Kama inawezekana....” Hiyo ni, "kama inawezekana.” Inafanyika kwa njia ya kushauriana na si kwa njia ya kusema "Mimi nakuuliza Wewe.” Alikuwa anaweka moyo mtiifu katika sala Yake, na katika hali Yake ya utiifu, Alisali hivi: "Kama inawezekana, acha kikombe hiki cha mateso kinipite: Walakini si kama nitakavyo Mimi, bali kama utakavyo Wewe” Bado aliomba hivi mara ya pili, na mara ya tatu Alisali hivi: "Naomba mapenzi ya Mungu yafanyike.” Yeye alielewa mapenzi ya Mungu Baba, akisema: "Naomba mapenzi Yako yafanyike.” Aliweza kuwatii kikamilifu bila kujichagua mwenyewe kwa kiwango hata kidogo. Alisema, "Kama inawezekana, acha kikombe hiki cha mateso kinipite.” Je, hiyo inamaanisha nini? Ni kwa sababu ya wazo kuhusu kuvuja damu msalabani mpaka pumzi Yake ya mwisho ya kufa na maumivu makubwa! Hii ilihusisha kifo na yalisema katika kigezo cha kwamba Yeye alikuwa bado hajaelewa kabisa mapenzi ya Mungu Baba. Kwa hiyo, Alikuwa mtiifu sana kwa kuwa Yeye aliweza kuomba kwa njia hiyo katika fikira ya maumivu. Sala Yake ilikuwa ya kawaida, Yeye hakuomba kubishana wala kusema kilikuwa lazima kiondolewe, bali ilikuwa ni kutafuta nia ya Mungu katika hali ambayo Hakuilewa. Mara ya kwanza Alipoomba, Hakuelewa na kusema: "Kama inawezekana ... lakini kama utakavyo Wewe.” Alimwomba Mungu katika hali ya unyenyekevu. Mara ya pili, Akaomba vile vile. Kwa ujumla, Aliomba mara tatu (bila shaka sala hizi tatu hazikufanyika tu katika muda wa siku tatu), na katika sala Yake ya mwisho, Alielewa kabisa nia za Mungu. Baada ya hapo, Hakuuliza chochote. Katika maombi yake mawili ya kwanza, Alitafuta, na katika kutafuta, Alikuwa bado katika hali ya unyenyekevu. Hata hivyo, watu hawaombi kwa njia hiyo. Wanasema, "Mungu, nakuomba ufanye hiki na kile na nakuomba Uniongoze katika hili na lile, na nakuomba Uniandalie mazingira....” Labda Hatakuandalia mazingira yanayokufaa na Atakuwacha upitie katika mateso. Kama watu kila mara wangesema, "Mungu, nakuaomba unifanyie maandalizi na unipe nguvu...," sala hiyo ingekuwa isiyo na busara! Lazima uwe na busara wakati unaomba, na lazima uombe katika kigezo cha unyenyekevu. Usitoe uamuzi. Kabla hujaomba, wewe unaamua: Lazima nimuulize Mungu na kumwambia Mungu kile cha kufanya. Aina hii ya maombi ni yasiyo na busara. Mara nyingi, Roho hasikilizi maombi ya watu hata kidogo, kwa hiyo, maombi yao ni ya kuchosha sana.

Hata kama watu hupiga magoti kuomba katika ulimwengu usiogusika, wanazungumza na kuomba, lazima uelewe kwamba sala za watu pia ni mkondo wa Roho Mtakatifu kufanya kazi. Watu wanapoomba na kutafuta katika hali sahihi, Roho Mtakatifu pia Atafanya kazi kwa wakati uo huo. Hizi ni vipengele viwili ambavyo Mungu na wanadamu wanaweza kwa mafanikio kuratibu pamoja, au kwa maneno mengine, ni Mungu anawasaidia watu kushughulikia masuala. Hii ni aina ya ushirikiano wa mwanadamu mbele ya Mungu; pia ni mbinu ya Mungu ya kufanya watu wakamilifu. Ni zaidi njia ya kuingia kwa kawaida kwa watu katika maisha—sio sherehe. Maombi si tu kuhusu kuamsha nguvu ya mtu au kutaja baadhi ya misemo; hayako hivi. Iwapo hayo ndiyo yote yaliyokuwa, basi ingetosha tu kufuata mkondo na kutoa baadhi ya misemo; hakungekuwa na haja ya kuuliza chochote, hakungekuwa na haja ya ibada na hakungekuwa na haja ya uchaji. Umuhimu wa sala ni wa kina sana! Kama wewe huomba mara kwa mara na kama unajua jinsi ya kuomba, mara kwa mara ukiomba kwa unyenyekevu na kwa busara, basi mara kwa mara utahisi hasa ukawaida ndani. Ikiwa mara kwa mara unaomba na misemo michache na huna mzigo, au kutafakari jinsi unaongea na busara au bila busara katika sala yako, na ni aina gani ya njia ya kuzungumza si ibada ya kweli, na kama wewe kila mara hauko makini kuhusu mambo haya , basi maombi yako hayawezi kuwa na mafanikio na hali ndani yako siku zote haitakuwa ya kawaida; hutaweza kwa undani kuingia katika masomo ya ni nini busara ya kawaida, utiifu wa kweli ni nini, ni nini ibada ya kweli, na wapi pa kusimama. Haya yote ni masuala ngumu kueleza. Kwa kuwa watu wengi wana mawasiliano kidogo nami, wanaweza tu kuja katika uwepo wa Roho na kuomba. Unaposali, inahusisha kama maneno yako ni ya busara, kama maneno yako ni kuhusu ibada ya kweli, kama Mungu anakusifu kwa mambo unayoomba, kama maneno yako ni kuhusu shughuli, kama kuna uchafu wa binadamu katika maneno yako, yawe maneno yako, matendo na maamuzi ni kulingana ukweli; kama una uchaji, heshima na utii kwa Mungu, na kama kweli unamtendea Mungu kama Mungu. Lazima uwe wa kweli na mwenye ari na maneno unayoomba wakati hauko mbele ya Kristo. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kuwa wa kawaida mbele ya Kristo. Kama wewe si wa kweli mbele ya Roho, unapokuja mbele ya mtu (Kristo), utakuwa daima katika upinzani, au hutakuwa na mantiki katika maneno yako, au hutakuwa mwaminifu katika maneno yako, au daima utakuwa unakatiza kwa maneno na matendo yako. Baada ya jambo hilo kuisha, wewe daima utajishutumu mwenyewe. Mbona siku zote unajishutumu mwenyewe? Kwa sababu kwa kawaida huna uelewa wa kweli katika ibada yako kwa Mungu na katika jinsi unamtendea Mungu. Kwa hiyo, wakati mambo yanakujia, unachanganyikiwa na hujui jinsi ya kutenda, na wewe daima utafanya mambo vibaya. Je, watu wanaoamini katika Mungu huja vipi katika uwepo wa Mungu? Kwa njia ya maombi. Unaposali, chunguza jinsi ya kuzungumza na busara, namna ya kuzungumza katika mahali sahihi kwa ajili ya watu, jinsi ya kuzungumza katika hali ya unyenyekevu, na ni aina gani ya njia ya kuzungumza inafanya moyo wako uwe na wasiwasi (isipokuwa sala ambazo hazisemwi kwa dhati). Itakuwa bora zaidi kama ungefanya mazoezi kwa kipindi cha muda na kisha uje mbele ya Mungu. Kwa kawaida, maombi yako mbele ya Roho si ya busara na kamwe hulengi hili. Unaamini kuwa Mungu hakuoni, hivyo unaweza kusema chochote utakacho, na ukisema kitu kibaya si neno. Wewe ni usiyejali na mpumbavu siku nzima, na matokeo yake, unapokuja katika uwepo wa Kristo, wewe una hofu ya kusema kitu kibaya na kufanya kitu kibaya. Hata ingawa una hofu ya kusema kitu kibaya, utasema kitu kibaya; hata ingawa una hofu ya kufanya kitu kibaya, kuna uwezekano wa wewe kufanya makosa; ingawa unaogopa kuwa mdeni, kwa hakika utakuwa mdeni, na hutaweza kulipa madeni yako. Kwa sababu huwezi mara kwa mara kuwasiliana na Kristo au kumsikia Kristo akisema na wewe ana kwa ana. Unaweza tu kuja mara nyingi kwa uwepo wa Roho kuomba, kutafuta na kutii, kwa sababu hata kama Mimi ningeongea na wewe ana kwa ana, ingebidi ujitegemee mwenyewe kutembea katika njia hii. Kuanzia sasa kuendelea, lazima muwe makini zaidi kuhusu mnachosema wakati mnaomba. Unapoomba, tafakari, na kuhisi, na Roho Mtakatifu anakupa nuru, utafanya maendeleo katika nyanja hii. Hisia ya kupata nuru ya Roho Mtakatifu ni hasa ngumu kueleza. Kama una hisia hizi zisizoelezeka na utambuzi usioelezeka, kama baadaye utafanya baadhi ya mambo na kushughulikia baadhi ya mambo, au kuwa na mawasiliano na Kristo na kushughulikia baadhi ya mambo, basi utakuwa na uwezo wa kutambua maneno ambayo yana mantiki, maneno ambayo hayana mantiki, mambo ambayo yana mantiki, na mambo ambayo hayana mantiki. Hili linatimiza malengo ya maombi.

Lazima uipe uzito njia unayochukulia maombi. Ukilala kitandani na kuomba, ukiamini kwamba Mungu anaweza kukusikia wewe, wewe huonyeshi uchaji! Angalia watu wengi katika Biblia ambao waliomba na ambao hawakuwa wanakimbilia uamuzi baada ya kujadili jambo. Kila kitu hatimaye kiliamuliwa na Roho Mtakatifu kwa njia ya maombi. Mji wa Jericho ulishambuliwa kupitia maombi; Watu wa Ninawi walitubu na kumwomba Mungu awasamehe pia kwa maombi. Maombi si sherehe, kuna umuhimu mkubwa ndani yake. Tunaweza kuona nini kutoka katika maombi ya watu? Watu wanamtumikia Mungu moja kwa moja. Ukilitazama hili kama sherehe, basi bila shaka hutamtumikia Mungu vizuri. Inaweza kusemwa kwamba ikiwa maombi yako si ya bidii au ya dhati, basi Mungu hatakuhesabu, Yeye atakupuuza, na kama utapuuzwa, huwezi kuwa na Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani mwako. Kwa hiyo, unakatizwa tamaa katika kufanya kazi yako. Kuanzia sasa, bila maombi, huwezi kufanya kazi. Ni sala ndiyo huleta kazi na sala ndiyo huleta huduma. Unasema wewe ni kiongozi na mtu anayemtumikia Mungu, lakini hujawahi kujitoa mwenyewe kwa sala na hatujapata kamwe kuwa wa kwelii katika maombi yako. Katika kuhudumu kwa njia hii, utashindwa. Mwanadamu ana sifa gani ndiyo asiombe? Kwa sababu Mungu alikuwa mwili? Hiyo siyo sababu. Wakati mwingine Mimi pia huomba. Angalia wakati ambapo Yesu alikuwa katika mwili na kuomba wakati mambo muhimu yalikuja juu Yake. Aliomba juu ya mlima, akiwa kwenye mashua, na katika bustani, na Aliwaongoza wanafunzi wake kuomba. Ukija katika uwepo wa Mungu mara nyingi na kusali mara nyingi, basi inathibitisha kwamba wewe unamchukua Mungu kwa makini. Ikiwa mara kwa mara unfanya kazi mwenyewe na mara kwa mara huombi, mara kwa mara unafanya hiki na kile nyuma Yake, basi humtumikii Mungu, bali unafanya tu biashara yako mwenyewe. Je hauhukumiwi katika kufanya biashara yako mwenyewe? Kutoka nje kuangalia ndani, haionekani kama umefanya kitu chochote cha kusumbua, na inaonekana ni kama hujakufuru, lakini unafanya jambo lako mwenyewe. Je, hukatizi? Sivyo? Hata kama inaonekana kama hukatizi kutoka nje, wewe ni unampinga Mungu katika asili.

Watu wote wamepitia hili; mambo ambayo hukujia kwa njia ambayo hutaki ni hasa magumu kuvumilia; unapokuwa na wasiwasi, utazungumza na mtu na baada ya muda, hutajisikia mwenye wasiwasi. Kuepuka usumbufu hakutatui hali yako. Wakati mwingine wakati matatizo yanakujia kazini, unahisi shinikizo, na wakati upogoaji na ushughulikiaji unakujia, unahisi hasa kushinikizwa.... Wakati wa kero hizi ni mara ngapi gani ulikuja mbele ya Mungu kuomba? Kila wakati ulifanya marekebisho wewe mwenyewe na kugeuka kwa njia ya kipumbavu. Kwa hivyo, watu wanaamini katika Mungu lakini Mungu hayuko katika mioyo yao. Wote kwa upofu wanafanya mambo bila thamani, kama ombaomba anayechukua kidogo hapa na kidogo pale kutoka katika biwi la takataka, na kujaza mfuko wake; lakini haina thamani na inafanywa kwa upofu kabisa. Unaona kwamba watu mara nyingi wanaondoka katika njia sahihi, wanatoka kwayo mara kwa mara. Tunaweza kuona asili ya watu kutokana na hili. Je, unaona nini kutokana na hili? Asili ya watu ni kusaliti. Hawana Mungu wanapofanya kazi. Hata wanafikiri: "Naamini katika Mungu, ni jinsi gani sina Mungu? Je, mimi sifanyi kazi kwa ajili ya Mungu? “ Moyo wako hauna Mungu, unaenda mbali kutoka kwa Mungu na kumsaliti kwa yoyote yale unayofanya. Maombi ni kitu kikubwa zaidi; ukienda katika kumtumikia Mungu bila hata kuomba, basi wewe unahudumu bure. Hali yako itakuwa isiyo ya kawaida zaidi na utakuwa na matokeo kidogo. Maombi si kuhusu jinsi maneno yako yalivyo mazuri wakati unaomba, unahitaji tu kusema maneno ya moyo wako na kuzungumza kwa uaminifu kulingana na matatizo yako. Ongea kutoka katika mtazamo wa kuwa sehemu ya uumbaji na kutoka katika mtazamo wa kutii: "Ee Mungu, Unajua kwamba moyo wangu ni mgumu sana. Ee Mungu, niongoze katika jambo hili; Unajua kuwa nina udhaifu, Mimi nimepungukiwa na sifai kutumiwa na Wewe. Mimi ni muasi na hukatiza kazi yako ninapofanya mambo; vitendo vyangu haviambatani na na mapenzi Yako. Nakuomba Ufanye kazi Yako mwenyewe na sisi tutashirikiana tu.... “ Kama huwezi kusema maneno haya, basi wewe umemalizika. Baadhi ya watu hudhani: "Wakati ninaomba ni lazima nitambue kama sala ni ya busara au la; haiwezekani kuomba. “ Hili si tatizo. Fanya mazoezi kwa muda na utafahamu. Omba na wewe utajua kama kuna maneno ambayo si sahihi. Uhusiano wa moja kwa moja zaidi na Mungu ni kupitia katika maombi, na wakati wa maombi ndio uhusiano wa watu na Mungu ni wa karibu sana. Kwa kawaida, wakati unafanya hili, je, unaweza kwa wakati uo huo kuanguka kwenye magoti yako na kusali? La, huwezi. Kwenda chini kwenye magoti yako na kusali ndio wakati ambao uhusiano wako na Mungu ni wa karibu sana. Unaposoma neno la Mungu, utakuwa na hisia ya aina tofauti ukilisoma baada ya maombi. Ukilisoma neno wakati ambao hujasali kwa muda fulani hutalielewa; ukishalisoma hutajua linamaanisha nini.

Kuomba na kutafuta katika uwepo wa Mungu si kuhusu kumlazimisha Mungu kufanya hili na lile. Sala yenye busara ni nini? Sala lisilo na busara ni nini?? Utajua baada ya kupata uzoefu kwa muda fulani. Kwa mfano, baada ya kuomba wakati huu, wewe unajisikia kwamba Roho Mtakatifu hafanyi hivyo na Hakuelekezi kule. Unapoomba wakati ufuatao, hutaomba kwa njia hiyo, hutamlazimisha Mungu kama ulivyojaribu mara ya mwisho, na hutamuuliza Mungu mambo kulingana na mapenzi yako mwenyewe. Wakati unaomba tena, utasema: “Ee Mungu! Kila kitu hufanywa kufuatana na mapenzi yako.” Mradi tu unalenga mbinu hii, na kupapasa huku na kule kwa muda, basi utajua "kukosa busara" ni nini. Pia kuna aina ya hali ambapo watu huhisi katika roho zao kwamba wakati wanaomba kulingana na nia zao wenyewe, wao wanakosa uchangamfu, kosa la kusema,ni wenye kufedhehesha, na kuzungumza bila maneno. Zaidi wanavyosema, zaidi inavyokuwa ya kufedhehesha zaidi. Hii inathibitisha kwamba unapoomba hivi, ni kufuata mwili kikamilifu, na Roho Mtakatifu hafanyi kazi au kukuongoza hivyo. Hili ni suala la kupapasa huku na kule na suala la uzoefu. Hata kama Mimi ningekuwa nimekwishamaliza kusema na wewe sasa hivi, unapopitia hili, unaweza kuwa na baadhi ya hali maalum. Maombi ni hasa kuhusu kuzungumza kwa uaminifu: “Ee Mungu! Unajua upotovu wangu, na leo Nimefanya jambo jingine lisilo la busara. Nilikuwa na nia ndani, lakini mimi ni mdanganyifu. Wakati huo sikufanya hilo kulingana na mapenzi Yako au kilingana na ukweli, bali nilifanya kulingana na nia yangu mwenyewe, na nilijitetea mwenyewe. Sasa natambua upotovu wangu na nakuomba Unipe nuru zaidi na uniruhusu kuelewa ukweli na kuuweka katika vitendo hivyo niweze kutupa mbali mambo haya....” Sema hivi; kiri na kusema kwa kweli kuhusu masuala halisi: “Ee Mungu! Niko tayari kutupa mbali upotovu wangu, niko tayari kubadili tabia yangu na kuuweka ukweli katika vitendo....” Mara nyingi watu hawaombi kwa kweli, wao hufikiri na kutafakari tu, wao huwa na ufahamu wa akili na toba. Hata hivyo, hawana uelewa wa ukweli kabisa, ambao lazima ufanyike kupitia sala. Baada ya kuomba, kiasi cha uelewa wako kitakuwa na kina zaidi kuliko kama ungekuwa unatafakari tu. Roho Mtakatifu hufanya kazi kukugusa, na hali, hisia, na kuendelea Anaokupa kunakuruhusu kuwa na uelewa wa kina wa jambo hili, na kiwango chako cha majuto kitakuwa hasa na kina. Utajuta jambo hili kwa ndani na hivyo utalielewa kabisa. Kama unajichunguza tu kwa uzembe, na baada ya hayo, huna njia zinazofaa kufanya mazoezi, na huna maendeleo yoyote katika ukweli, basi hutaweza kubadilika. Kuchukua mfano, wakati mwingine watu wanaweka azimio, wanafikiri: "Lazima nijitumie kwa bidii kwa Mungu na kwa bidii niulipize upendo wa Mungu.” Wakati una nia hii ikihamasisha matumizi yako, shauku yako haitakuwa lazima iwe kubwa, na moyo wako hautakuwa hakika kabisa umewekezwa katika kipengele hiki. Hata hivyo, ukiguswa wakati unaomba na kisha kuweka azimio: "Niko tayari kupitia ugumu, niko tayari kupokea majaribio kutoka Kwako, niko tayari kabisa kukutii. Bila kujali ni matatizo mangapi yatakuwepo, niko tayari kuulipiza upendo Wako. Nafurahia upendo Wako mkuu na furaha hii kubwa. Ninakushukuru kutoka ndani ya moyo na nakupa Wewe utukufu.” Na aina hii ya maombi, utakuwa umejawa nguvu; haya ni matokeo yanayopatikana kutoka kwa maombi. Baada ya kuomba, Roho Mtakatifu atawapa nuru na kuwaangazia watu, na kuwaongoza watu, na kuwapa watu imani na ujasiri wa kuuweka ukweli katika vitendo. Unaona kwamba baadhi ya watu wanasoma neno la Mungu kila siku na hawatoi matokeo haya. Baada kusoma maneno ya Mungu, na wanafanya ushirika na kuwasiliana, mioyo yao itakuwa yenye kung’aa, nao watakuwa na njia. Kama Roho Mtakatifu pia anakupa uelekezaji, mizigo na uelekezi, basi itakuwa tofauti sana. Kama unaguswa kidogo baada tu ya kusoma maneno ya Mungu, na kumwaga machozi wakati uo huo, kuguswa huko kutatoweka haraka baada ya kufanya kazi kwa muda. Kama una maombi ya machozi, maombi ya bidii au sala za dhati, nguvu zako hazitashuka chini siku tatu baada ya sala kwisha. Je si kila mtu huwa na aina hii ya uzoefu? Haya ni matokeo yanayopatikana kutoka kwa maombi. Kusudi la maombi ni ili watu waje mbele ya Mungu na kukubali kile Anachotaka kuwapa. Unaposali mara kwa mara, unapokuja kwa Mungu mara kwa mara, basi mara kwa mara uko na uhusiano na Mungu. Kila mara unasisimuliwa Naye moyoni mwako na kila mara unakubali kile ambacho Anakuletea. Kwa kuwa wewe kila mara hukubali Anachokutolea utabadilika, na hali yako itakuwa bora zaidi na zaidi na hutahisi tena kama asiye na furaha. Hasa baada ya ndugu na dada wameomba pamoja, kuna kiwango kikubwa cha nguvu, nyuso zimejawa na jasho na unahisi kwamba umenufaika pakubwa mno. Kwa hakika hujashiriki kitu chochote spesheli kwenye ushirika kwa kwa siku kadhaa, na ni sala la kutia nguvu sana kiasi kwamba unahisi uko tayari kuitupilia kando familia yako na dunia, yenye kutia nguvu sana kiasi kwamba hutamani chochote—Mungu pekee Anatosha. Hivyo ndivyo nguvu hii ilivyo kuu. Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwapa watu nguvu hii na watu kamwe hawatapata kuifurahia kikamilifu! Kama hutegemei uwezo huu, imarisha moyo wako na kaza shingo lako; au kama unategemea utashi wako mwenyewe na matarajio, basi unaweza kuenda wapi? Huwezi kufika mbali kabla ya kujikwaa na kuanguka, na hutakuwa na nguvu hizo unapokwenda. Watu lazima wadumishe mawasiliano na Mungu tangu mwanzo hadi mwisho, lakini watu hujikwamua kutoka kwa Mungu wanapokwenda. Mungu ni Mungu, watu ni watu, na wao huenda njia zao tofauti. Mungu huongea neno Lake na watu wanatembea njia zao wenyewe, ni njia mbili tofauti. Watu wakiwa hawana nguvu, wanaweza kuja kwa Mungu na kusema maneno machache ili kuomba nguvu kiasi. Baada ya kukopa nguvu kidogo, wao hukimbia. Baada ya kukimbia kwa muda, wao huishiwa na nguvu, na kumrudia Mungu na kumwomba nguvu zaidi kidogo. Watu wako namna hii na hawawezi kusimama imara kwa muda mrefu sana. Watu wanapomwacha Mungu, basi hawana njia.

Nimebaini kuwa uwezo wa watu wengi kujizuia wenyewe ni hasa zenye upungufu. Kwa nini iko hivi? Watu hawaombi kamwe, na wakati hawaombi, wanakuwa waasherati; mara wanapokuwa waasherati, hawana uchaji au unyenyekevu; wao wako makini na ubinadamu tu, uadilifu, na kujua asili yao potovu, ni hayo tu. Watu hupuuza jinsi Roho Mtakatifu kwa kweli hufanya kazi na huwagusa watu, na jinsi wanapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika maisha yao ya kila siku. Imani ya watu kwa Mungu ni imani tu, na hakuna kitu cha kiroho kulihusu. Haya ni mambo mawili tofauti. Ni ulimwengu wa uyakinifu tu, na unakana roho. Kwa hiyo, wakati watu wanatembea, wapotea na kuanguka shimoni kichwa mbele. Bila maombi, utendaji wao wa ukweli unaweza tu kuzingatia kanuni moja ndani ya wigo fulani; wao hutekeleza tu masharti. Hata kama humkosei Mungu kwa kutimiza mipango kutoka juu, wewe unatii tu masharti. Hisia za kiroho ya watu siku hizi ni zisizojali na yenye mwendo wa pole. Kuna mambo mengi yasiyoeleweka katika uhusiano wa watu na Mungu, kama vile kuhisi wakiguswa kiroho au kupata nuru; lakini watu hawahisi haya, ni wasiojali. Ni kama kuimba, wakati watu hawaimbi mara nyingi, basi hawana uhakika na tuni. Watu hawasomi neno la Mungu na kamwe hawaungani na mambo ya maisha ya kiroho. Hawana ufahamu juu ya hali zao wenyewe. Bila kuomba na bila maisha ya kanisa, ni vigumu kufahamu hali ya maisha ya kiroho. Je, mnahisi hivi? Kuamini katika Mungu, ni muhimu kuomba hivi. Bila kuomba, basi huwezi kuwa na sura ya kuamini katika Mungu. Sasa tunasema, hakuna haja ya kanuni, mwanadamu anaweza kuomba wakati wowote na mahali popote. Kwa hivyo, baadhi ya watu huomba kwa nadra sana; wao wanaamka asubuhi na hawaombi. Wanaamka na kuchana nywele zao, kuosha nyuso zao, na kisha kusoma na kuimba. Usiku wanajilaza na kwenda kulala bila kuomba. Je, mnahisi hivi? Kama unasoma tu neno la Mungu bila kuomba, basi utakuwa kama mtu asiyeamini anayesoma neno la Mungu na halielewi. Bila maombi, moyo wako huwezi kuwa umejitolea kabisa na huwezi kuwa na hisia pambanuzi katika roho yako au kuguswa ndani ya roho yako. Utakuwa ni usiyejali na wa mwendo wa polepole, na utasema tu baadhi ya mambo nje kuhusu kubadilisha tabia yako. Inaonekana kana kwamba unaamini katika Mungu, lakini kwa kweli, kina cha hisia zako si kirefu vile. Inaonekana kana kwamba huamini katika Mungu, na huwezi kuomba bila kujali jinsi unavyojaribu. Hili tayari ni hatari sana na yenye upungufu. Kurudi kwa roho kuomba haikatizi kazi nyingi za nje; haisababishi tu usumbufu, lakini pia ni yenye faida kwa kazi.

Tanbihi:

a. Foili - mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kivilinganisha

Iliyotangulia: Sura ya 33. Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Inayofuata: Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki