Sura ya 31. Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu

Kitu hiki kinachoitwa mwanadamu kina uwezo wa kumsaliti Mungu, kwa hivyo unaweza kujua nini kutoka kwa hili? Baadhi ya watu huuliza: "Mungu alimuumba mwanadamu kwa hivyo Mungu hawezi kumzuia mwanadamu kumsaliti Yeye? Ni kwa nini mwanadamu bado ana uwezo wa kumsaliti Mungu? Je, Mungu si mwenyezi?" Hili ni tatizo, sio? Ni tatizo gani unaloweza kuona hapa katika suala hili? Mungu ana upande wa vitendo, lakini pia Ana upande wa uenyezi. Mwanadamu asingekuwa amepotoshwa na Shetani, bado tu angeweza kumsaliti Mungu. Kitu hiki kinachoitwa mwanadamu hakina hiari ya nafsi yake mwenyewe: Jinsi wanatakiwa kumwabudu Mungu, jinsi wanapaswa kumkana Shetani, kutoshirikiana na uovu wake. Wanapaswa kumtii Mungu, Mungu ana ukweli, uzima na njia, na Mungu hakosewi. Mambo haya hayako ndani ya wanadamu, wala wanadamu hawamiliki mambo hayo ambayo yangefahamu asili ya Shetani. Hapo mwanzo, wanadamu hawakuwa na chochote ndani yao, hivyo aliweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote. Hata zaidi watu wa siku hizi, ambao wamepotoshwa na Shetani na ambao sasa wana mambo ya kishetani ndani yao. Wao wanaweza kwa urahisi sana kumsaliti Mungu. Hili ndilo tatizo. Ni nini unachoweza kuona kuhusiana na tatizo hili? Mungu ana upande Wake wa uenyezi, na pia upande Wake wa vitendo. Ikiwa utaona tu upande wa Mungu wa vitendo, na usiweze kuona uenyezi Wake, basi itakuwa rahisi kwako kumsaliti Mungu, na kumchukulia Yeye kama tu mtu wa kawaida; ikiwa unaangalia upande wa Mungu ambao ni uenyezi, lakini huwezi kuona upande Wake wa vitendo, basi utamuasi Mungu kwa urahisi. Ikiwa huwezi kuona sehemu zote mbili za upande wa Mungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi sana kwako kumuasi Yeye. Kwa hivyo, inasemekana: "Je, kumfahamu Mungu sio jambo gumu zaidi ulimwenguni kulifanya?" Kadri mtu anavyomfahamu Mungu, ndivyo atakavyofahamu mapenzi ya Mungu na umuhimu wa kila kitu Anachofanya. Lakini uhalisi wa kumtaka mwanadamu amfahamu Mungu ni huu: Mwanadamu hawezi kumfahamu Mungu kikamilifu. Ingawa Mungu ana upande Wake wa vitendo, bado haiwezekani kamwe kwa mwanadamu kumfahamu Yeye kikamilifu. Mungu ni mkuu sana, wa ajabu sana na vigumu sana kumwelewa, kwa kuwa mawazo ya wanadamu ni finyu sana. Kwa nini inasemekana kwamba wanadamu daima watakuwa kama watoto wachanga mbele ya Mungu? Ni kwa sababu hii.

Mungu huonyesha maneno mengine au Hufanya matendo mengine na watu kila mara hukosa kufahamu na kufikiri, "Ni jinsi gani Mungu anaweza kutenda hivyo? Mungu ni mwenyezi!" Kuna vita vya daima ndani ya mwanadamu. Kuhusiana na Mungu kupitia mateso ya ulimwengu huu, watu wengine hufikiria: "Kwa nini Mungu anahitaji kupitia mateso ya ulimwengu huu ikiwa Yeye ni mwenyezi? Je, Yeye tayari hajui mateso ya ulimwengu huu yako vipi? Je, Mungu si mwenyezi? Bado Anahitaji kuyapitia?" Hili linahusiana na upande wa vitendo wa kazi ya Mungu. Usulubisho ulivumiliwa ili wanadamu waweze kukombolewa, ilhali mwanadamu hamfahamu Mungu na kila mara anahodhi dhana zengine kuhusu Mungu, akisema: "Kuwakomboa wanadamu wote Mungu alitakiwa tu kumwambia Shetani, 'Mimi ni mwenyezi. Unathubutu kuwazuia wanadamu wasije Kwangu? Ni lazima unipe wanadamu.' Kwa maneno haya machache kila kitu kingetatuliwa—je, Mungu hakuwa na mamlaka? Yote yaliyohitajika ilikuwa kwa Mungu kusema kwamba wanadamu wamekombolewa na kwamba dhambi za mwanadamu zimesamehewa, kisha mwanadamu hangekuwa na dhambi. Je, mambo haya hayakuamuliwa kwa maneno ya Mungu? Ikiwa mbingu na nchi na vitu vyote viliumbwa kwa maneno kutoka kwa Mungu, kwa nini basi Mungu hangetatua suala hili? Kwa nini Yeye Mwenyewe alihitajika kusulubiwa?" Upande wa Mungu wa uenyezi na upande Wake wa vitendo zote zinafanya kazi hapa. Kuhusiana na upande Wake wa vitendo, Mungu mwenye mwili alivumilia mateso mengi katika miaka Yake thelathini na mitatu na nusu hapa duniani, mwishowe Alisulubiwa mpaka damu Yake ikaisha. Alivumilia mateso ya kuogofya kabisa lakini kisha alifufuliwa kutoka kifoni. Kufufuka Kwake kulikuwa hali ya Mungu ya uenyezi ikifanya kazi. Hakufanya ishara yoyote, au kumwaga damu yoyote au kusababisha mvua kunyesha na kusema hii ilikuwa sadaka ya dhambi. Hakufanya kitu chochote kama hicho, lakini badala yake Yeye binafsi alipata mwili ili kukutana na wanadamu wote na alipigwa misumari juu ya msalaba, ili wanadamu waweze kujua kuhusu kitendo hiki. Kupitia kitendo hiki, wanadamu walikuja kujua kwamba Mungu alikuwa amewakomboa na hili lilikuwa thibitisho kwamba Mungu alikuwa kweli Amewaokoa wanadamu. Haijalishi kupata mwili gani kunatekeleza kazi au iwapo Roho Mwenyewe anafanya kazi hiyo moja kwa moja, ni kitu cha lazima. Hii inamaanisha kwamba, kwa kufanya mambo hivi, kazi hiyo inafanywa kuwa ya thamani zaidi na muhimu zaidi, na ni kwa kufanya tu vitu kwa njia hii ndipo wanadamu wanaweza kupata faida za kazi hiyo. Hii ni kwa sababu wanadamu wote ni kitu cha usimamizi wa Mungu. Ilisemwa hapo awali kwamba wanadamu walisimamiwa ili kupigana vita na Shetani na kumuaibisha. Na kwa kweli, hili sio zuri kwa mwanadamu mwishowe? Kwa mwanadamu, hili ni jambo la kukumbuka na ni jambo ambalo ni la thamani sana na muhimu. Kwa sababu wale ambao wamefanywa kuwa wakamilifu ni kikundi cha watu ambao wameibuka kutoka kwa dhiki kuu wakiwa na ufahamu wa Mungu, ambao wamekamilishwa na Mungu na ambao wameokoka upotovu wa Shetani; hivyo kazi hii lazima kweli ifanywe hivi. Uamuzi kuhusu ni mbinu gani ya kutumiwa katika kila hatua ya kazi Yake unategemea mahitaji ya wanadamu. Kazi ya Mungu bila shaka haifanywi kwa njia yoyote ya zamani. Lakini watu wana chaguo na wana dhana zao wenyewe. Kwa mfano, kuhusu usulubisho, watu hufikiria: "Kusulubiwa kwa Mungu kunahusiana na sisi vipi?” Wanafikiri hakuna uhusiano, lakini Mungu alihitajika kusulubiwa ili kuwaokoa wanadamu. Kusulubiwa kulikuwa mateso mabaya zaidi wakati huo, sivyo? Je, Roho angeweza kusulubiwa? Kama Roho angesulubiwa Hangehisi uchungu wowote, Hangekuwa mfano wa Mungu na hangeweza kuwa ishara ya Mungu, bila kutaja kwamba Hangeweza kutoa damu. Roho hawezi kutoa damu; ni mwili tu unaweza kutoa damu na damu Yake ya thamani ilikuwa thibitisho la sadaka ya dhambi. Mwili wake ulichukua mfano wa mwili wa dhambi na Akavumilia uchungu kwa niaba ya wanadamu. Roho hangeweza kupigwa misumari juu ya msalaba, hivyo Roho hawezi kuvumilia uchungu kwa niaba ya wanadamu na hawezi kuzikomboa dhambi za mwanadamu. Hili lilifanywa kwa ajili ya wanadamu na huu ni upande wa vitendo wa Mungu. Lakini kwamba Mungu angefanya hili, kwamba Angempenda mwanadamu, kilikuwa kitu ambacho hakingetimizwa na mwanadamu mwenyewe, hivyo huu ulikuwa uenyezi wa Mungu kazini. Kwa nini husemwa kwamba Yeye ni Mungu na kwamba Yeye ana hali ya uenyezi? Kila kitendo ambacho Mungu hufanya kina hali Yake ya uenyezi ndani yake, na pia kina hali Yake ya utendaji. Uenyezi wa Mungu ni kiini Chake, lakini utendaji Wake pia unajumuisha upande mmoja wa kiini Chake; hali hizi mbili hazitenganishwi. Mungu kufanya matendo katika uhalisi ni hali Yake ya vitendo ikitekeleza kazi, na kwamba Anaweza kufanya kazi kwa njia hii ni hali Yake ya uenyezi. Huwezi kusema kwamba Mungu hufanya kazi katika uhalisi, kwamba Mungu ni wa vitendo, na kwamba ni upande Wake wa vitendo unaotekeleza kazi bila hali ya uenyezi Wake. Kulingana na ufafanuzi wako, hii huwa sheria. Inajumuisha hali Yake ya uenyezi na hali Yake ya utendaji. Kitu chochote ambacho Mungu hufanya kina hali hizo mbili za uenyezi Wake na utendaji Wake, na yote hutekelezwa kulingana na kiini Chake; ni maonyesho ya tabia Yake, na ni ufunuo wa kiini Chake na kile Alicho. Watu hufikiri kwamba, katika Enzi ya Neema, Mungu ni rehema na upendo; lakini bado Ana ghadhabu Yake. Hukumu Yake, kulaani Kwake Mafarisayo na Wayahudi wote—je, hii si ghadhabu na haki Yake? Huwezi kusema kwamba Mungu ni rehema na upendo wakati wa Enzi ya Neema, kwamba kimsingi Hana ghadhabu, hukumu au laana—huku ni kutofahamu kwa watu kuhusu kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu katika enzi hiyo yote ilikuwa ni maonyesho ya tabia Yake. Kila kitu Alichofanya ambacho mwanadamu angeona kilikuwa ni kuthibitisha kwamba Yeye Mwenyewe ni Mungu na kwamba Yeye ni mwenyezi, kuthibitisha kwamba Yeye Mwenyewe ana kiini cha Mungu. Je, hukumu na kuadibu kwa Mungu wakati wa hatua hii humaanisha kwamba Yeye hana rehema au upendo? Yeye bado ana rehema na upendo. Ikiwa utatumia tu aina moja ya maneno, au kutumia sentensi moja au mbili kujumuisha kiini na tabia ya Mungu, basi wewe ni mjinga sana—humfahamu Mungu! Wengina watasema: "Tafadhali zungumza nasi juu ya ukweli kuhusu kumfahamu Mungu. Tafadhali tufafanulie waziwazi." Ni nini ambacho mtu anayemfahamu Mungu angesema? "Kumfahamu Mungu ni kwa kina sana. Hakuwezi kuonyeshwa kwa sentensi moja au mbili, au kuzungumziwa kwa siku moja au mbili kisha kufahamike." Kujua hili kunaweza kufikiriwa kama kuwa na ufahamu fulani—mwanadamu hawezi kamwe kumfahamu Mungu kikamilifu. Wenye kiburi na waisomfahamu Mungu watasema: "Bila shaka ninajua Yeye ni Mungu wa aina gani; ninamjua Mungu na ninamfahamu Yeye." Kuna mambo mengine ambayo wanadamu hawajapitia, ukweli mwingine ambao hawajaona na hivyo hawawezi kuwa na ufahamu halisi wa hayo na hawawezi kuwa na utambuzi wa kweli wa hayo, kumaanisha vitu hivyo vitaonekana kuwa vya dhahania sana kwao. Kitu kimoja tu ambacho wale wasiofahamu husikia ni aina ya ufafanuzi; huenda wakawa na ufahamu wa mafundisho ya kidini, lakini sio ufahamu halisi. Kwa vile tu hufahamu, haimaanishi kwamba hayo si ukweli. Kwa wale ambao hawajapata uzoefu, ni kama kwamba mambo hayo ni ya dhahania na magumu kufahamu, ilhali kwa kweli si ya dhahania katu. Ikiwa una uzoefu halisi, basi utajua neno lolote la Mungu liko katika muktadha gani, na utajua ni katika hali gani kitu chochote, ufahamu wowote na hali yoyote ambayo Mungu huzungumzia iko na kinahusu, na unaweza kutaja baadhi ya ufahamu kutoka kwa kumbukumbu yako. Ikiwa wewe husikia tu maneno, ikiwa huna ufahamu wa utendaji kamwe, ikiwa huna ufahamu katika kumbukumbu yako, basi utaona vigumu kuyakubali na, ukishayakubali, bado utahisi kwamba hayo ni aina fulani ya ufafanuzi tu. Hili kabisa ni jambo linalotakiwa kupitiwa na sio ujuzi au maarifa yanayoweza kusomwa. Kuwakomboa wanadamu wote, kuzikomboa dhambi zote za wanadamu—hii ni hali ya Mungu ya uenyezi. Sio kwamba Mungu huketi tu kivivu na kusema kwamba Yeye ni mwenyezi. Uenyezi wake unahusisha vitendo vinavyofanywa katika uhalisi. Katika kufanya kazi, Mungu huwashinda wanadamu, wao huanguka mbele Zake na wanakuwa wale wanaoweza kumtii Yeye. Ikiwa hali moja ya Mungu ingezungumziwa kwa kipekee bila nyengine, ama uenyezi Wake au utendaji Wake, basi mwanadamu hangeweza kuzifahamu: Hali hizi mbili lazima zifahamike sawia. Mungu hufanya kazi katika uhalisi, Yeye huonyesha tabia Yake mwenyewe na kile Alicho. Kazi yoyote asiyoweza kuifanya mwanadamu, Yeye anaweza kuifanya, na hili linahusu hali Yake ya uenyezi. Mungu kuifanya kazi hii Mwenyewe ni hali yake ya vitendo, na hali hizi mbili hufanya kazi kwa maafikiano. Maneno anayonena Mungu yana hali Yake ya uenyezi na Yeye hushika mamlaka Yake, akikamilisha Anachosema Atakamlisha. Ni wazi kwamba matokeo ya mwisho yatakuwa nini; Anaponena maneno haya, uenyezi Wake hufichuliwa. Usisahau hili: Kiini cha Mungu Mwenyewe ni uenyezi pamoja na vitendo, na hali hizi mbili hutimizana. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni maonyesho ya tabia Yake na ni ufunuo wa kile Alicho. Kile Alicho kinahusisha uenyezi Wake, haki Yake na adhama Yake. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, Mungu alimwambia Yona aende Ninawi, na hili lilithibitisha kwamba Mungu ana upande wa vitendo. Lakini Yona hakusikia na, mwishowe, kuendelea kuishi kwake ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu ilikuwa kazi ya uenyezi wa Mungu. Kile ambacho Mungu alimtendea Yona kinafichua kwamba Mungu ni mwenyezi. Kazi ya Mungu kuanzia mwanzo hadi mwisho ni ufunuo wa kiini Chake mwenyewe na onyesho la kile Alicho. Kiini Chake kina hali mbili: Moja ni hali ya uenyezi Wake, na nyengine ni hali ya utendaji Wake. Hizi hali mbili unaweza kuziona katika kila hatua ya kazi ya Mungu, na unaweza kuona kwamba hali hizi mbili ziko katika kila kitu anachofanya Mungu. Hii ni njia moja ya kumfahamu Mungu.

Iliyotangulia: Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro

Inayofuata: Sura ya 32. Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki