Sura ya 27. Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu”

Ukilibadilisha au kulikanganya neno la Mungu Mwenyewe, basi hiyo ni sawa na uasi wa Mungu, kukufuru dhidi Yake na usaliti. Hii ni sawa tu na malaika mkuu kusema:"Mungu, Unaweza kuumba mbingu na ardhi na vitu vyote na Unaweza kufanya miujiza, lakini pia mimi ninaweza. Unapanda juu kwenye kiti cha enzi, na hivyo hivyo mimi pia napanda. Unatawala mataifa yote, Ninatawala mataifa yote pia. Wewe ulimuumba mwanadamu ilhali mimi ninawatawala!" Je, hii si ya hali sawa? Wengine wana mtazamo fidhuli kuhusu mipangilio ya kazi kutoka juu. Wanafikiri: "Aliye juu hufanya mipangilio ya kazi na sisi tunafanya kazi kwenye viwango vya chini. Kuna baadhi ya maneno na mambo ambayo tunaweza kufanya kwa urahisi, ambayo yanaweza kubadilishwa mara yanapofika viwango vya chini, kwa sababu aliye juu husema mambo tu, na sisi tulio chini tunayatenda. Tunaelewa hali katika viwango vya chini, ambayo aliye juu haelewi, hivyo tunaweza kufanya kazi kwa njia yoyote inayotufaa. Kwa vile wale walio katika ngazi za chini wamekabidhiwa kwetu, tunaweza kuwaongoza vyovyote tunavyotaka. Haijalishi jinsi tunavyowaongoza, na hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kuingilia kati. "Wanaendeleza kanuni hii katika utumishi wao wa Mungu: "Nitasikiliza chochote ambacho nadhani ni sahihi lakini sitasikiliza chochote ninachofikiri hakifai. Naweza kukupinga na kuasi dhidi Yako. Sitatekeleza kitu chochote au kuweka kitu chochote katika matendo kwa ajili Yako. Ukisema chochote kisichostahili basi nitakibadilisha kwa ajili Yako, na nitakipitisha tu baada yake kupitia kwangu. Ikiwa hakijaidhinishwa na mimi, basi hakitachapishwa. "Mahali pengine, mipangilio kutoka kwa aliye juu inapitishwa katika hali yao ya asili. Lakini watu hawa kwanza hubadilisha mipango ya kazi kabla ya kuipeleka kwenye mikoa wanayoongoza. Mtu wa aina hii daima hutaka kumweka Mungu kwa upande mmoja na yuko na hamu sana kwa wengine kumfuata, kumwamini. Machoni pake, Mungu hafanani kabisa naye katika maeneo fulani, na anadhani kuwa ana kitu ambacho Mungu hana, kwamba kila mtu anapaswa kumwamini na kwamba yeye ni Mungu. Matendo yao ni ya asili hii. Je, mnaelewa? Ikiwa mmeelewa, mnaweza bado kulia? Je! bado mnaweza kuwahurumia watu hawa? Je! Bado mnaweza kufikiri kwamba aliye juu amefanya vibaya au hajafanya kwa haki, na kwamba wale ambao wanaweza kuteseka sana waondolewe? Wanateseka kwa ajili ya nani? Wanateseka kwa ajili ya hali yao wenyewe. Je! Wanamtumikia Mungu? Je! Wanafanya wajibu wao? Je, ni waaminifu kwa Mungu? Je, wao ni watiifu? Wao ni vikaragosi wa Shetani, bila shaka. Kazi yao ni shetani akichukua nguvu, kuuharibu mpango wa usimamizi wa Mungu na kuvuruga kazi ya Mungu. Imani yao ni nini? Wao ni ibilisi na wapinga Kristo, vila shaka. Watu wengine husema: "Tazama jinsi wanavyoteseka, wakijitahidi sana kuandika vitabu hivyo. "Kuandika nini? Vitabu gani? Wanateseka kwa ajili ya nani? Nyinyi daima huona jinsi wanavyoteseka, na kusema: ", Ee wanateseka sana! Kwa hivyo ni sawa kwamba walimuasi Mungu kidogo. Mungu anapaswa kuwasamehe. "La hasha! Wangeruhusiwa kufanya watakavyo, kila mtu angeruhusiwa kumuasi Mungu! Je! Mateso kidogo yanamaanisha kuwa wao wamehitimu kumuasi Mungu? Je, ina maana kwamba wanapaswa kumuasi Mungu? Je! Ina maana kwamba wanapaswa kuasi dhidi ya Mungu? Je! Ina maana kwamba wanapaswa kuchukua sheria katika mikono yao wenyewe na kutomtii Mungu? Ina maana kwamba wanaweza kufanya chochote wanachotaka? Ikiwa kila kitu ambacho mtu alifanya kingekuwa sahihi na kila mtu angekuwa na wa ukweli, basi hakungekuwa na haja ya hatua hii ya kazi ili kumwokoa mwanadamu. Ingeonyesha kwamba mwanadamu hana upotovu na kwamba mwanadamu si wa Shetani. Mwanadamu hana ukweli, bado hatii na bado anataka kutenda bila kufikiri. Mungu huongea ukweli, lakini bado wanataka kuubadilisha, nao wanafikiri kwamba wanachokifanya kina ukweli, kwamba wanachokifanya ni sawa. Wao ni kitu tu kilichotumwa na ibilisi na kutumwa na Shetani! Ikiwa bado mnaweza kuhisi huruma kwa mtu wa aina hii, bado mnalia machozi kwa ajili yao na bado mnaweza kuwatetea kwa haki kwa ajili yake, basi nyinyi pia ni bure. Pia mnafikiri kuwa aliye juu ametenda kwa njia isiyo ya upole, na kwamba watu hawa waliteseka sana na jinsi walivyoweza kuondolewa kwa ghafla. Kwa kusema hili, nyinyi pia ni vikaragosi wa Shetani na nyinyi ni mapepo. Je! Kuna yeyote kati yenu ambaye bado anataka kuwatetea kwa haki kwa ajili yao? Mnasema: "Mtu mmoja aliwashtaki na Mungu akawaondoa. Mungu hajui chochote, na aliye juu ambaye anatuongoza hajui chochote pia. "Maoni yako yamekosea sana, ya kipumbavu sana! Watu wengine wanaropokaropoka na husema chochote wanachotaka kusema. Wanaona kwamba Mungu sasa ni mtu wa kawaida, hivyo humkashifu Mungu mara nyingi wanavyotaka. Mtu wa aina hii huzaa matunda yaliyooza tu! Mnamdharau Mungu sana na kwenda kinyume na Mungu; mnamdharau Mungu hadharani, mnakufuru dhidi ya Mungu, mnamkashifu, kumhukumu na kumpaka Mungu matope. Mtu wa aina hii baadaye atakuwa mlengwa wa adhabu kali. Kwa mfano, kuna baadhi ya watu ambao wana chuki kwa Mungu ambayo daima wao hueneza. Maneno yoyote ambayo ni machafu na yanatoa chuki yao zaidi, wanayasema. Je, watu wa aina hii sio mashetani? Baada ya muda, wanahisi majuto, na wengine husema: "Wao ni wa kusikitisha sana. Wanatubu na kusema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu, kwamba hawaemlewi Mungu. Wanasema mambo kama haya na inaonekana kama wameacha kufanya upumbavu. Je! Hawawezi kusamehewa? "Wanawezaje kusamehewa kwa urahisi vile? Ikiwa kuna hadhi katika mtu mmoja, basi tunaweza kusema nini kumhusu Mungu? Walimkufuru na kumkashifu Mungu, kisha wakatubu, na wanapaswa kusamehewa? Inasemekana walikuwa wapumbavu kwa muda. Ulikuwa ujinga wa muda mfupi? Watu wengine huongea kwa makusudi, bila shaka. Wakiona kwamba aliye juu amewaondoa, hawangefurahia tena hali yao na wanaogopa kuwa hawatakuwa na uwezo wa kuishi, kwa hivyo wanasema mengi kuhusu kutoridhika kwao. Kisha baadaye, wanatubu na kulia sana. Lakini maneno yako yamezidi kiasi, na maji yaliyomwagika chini hawezi kuzoleka tena. Je! Mungu anaweza kuwaruhusu watu kumdharau kwa kawaida, kumhukumu na kukufuru dhidi Yake na kulipuuza? Huko si kuwa na adabu! Wengine wamepita hisia zote za aibu, na husema: "Mungu, damu yako ya thamani ilinikomboa. Unatuuliza kuwasamehe wengine sabini mara saba, hivyo Unapaswa kunisamehe! "Hata baada ya kumaliza uasi wao, bado wananena kwa njia hii. Kwa kweli wamepita hisia zote za aibu! Wengine huanza uvumi na kumkashifu Mungu katika viwango vya chini. Baada yao kumaliza kumtukana Mungu, wao huwa na hofu, wakiogopa kuadhibiwa, nao huanguka kwa magoti yao na kuomba: "Ee Mungu! Tafadhali Usiniache! Tafadhali Usiniadhibu! Ninakubali dhambi yangu na mimi ninatubu. Mimi ni mdeni Wako. Nimefanya makosa. "Je, unadhani mtu wa aina hii anaweza kusamehewa? Hawezi! Kwa nini hawezi? Kwa sababu hili ni kosa dhidi ya Roho Mtakatifu, na dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu haiwezi kusamehewa katika maisha haya au katika maisha yajayo. Mungu Anamaanisha Anachosema; Mungu ni mwenye heshima na mwenye ghadhabu. Ana tabia yenye haki na Hawezi kuwa "mtu mzuri" ambaye watu hufikiri, wakidhani kwamba hataangalia tena makosa ya zamani ya yeyote ambaye ni mzuri Kwake. Hili halitafanyika. Je! Ni jambo gani zuri linaloweza kutokea katika kumuasi Mungu? Ukifanya jambo baya kwa sababu ya ujinga wa muda mfupi, basi hili linaweza kusamehewa. Pia inasemeheka kama hali yako ya upotovu inajionyesha wakati mwingine. Lakini ikiwa unamuasi Mungu moja kwa moja, unaasi dhidi ya Mungu moja kwa moja, unaenda dhidi Yake moja kwa moja, unakufuru dhidi Yake, unamkashifu, unaanzisha uvumi kumhusu, basi hutakuwa na umuhimu wowote na lazima usubiri adhabu. Mtu wa aina hii haifai kuomba tena. Anafaa tu kwenda na kusubiri kuadhibiwa. Msamaha hauwezekani. Wakati unapokuja, usiseme bila haya: "Ee Mungu! Tafadhali nisamehe!" Ikiwa, baada ya mtu kuwa na ufahamu fulani, anaenda na kufanya mambo haya mabaya tena, basi anafanya ukiukaji huu kwa kujua, na hivyo haiwezekani kumsamehe. Wakati ilivyotajwa hapo awali kwamba Mungu hangeyakumbuka makosa ya mwanadamu, ilikuwa inasemwa kuhusiana na makosa madogo ambayo hayajumuishi makosa dhidi ya amri za utawala wa Mungu, au makosa dhidi ya tabia ya Mungu; makosa haya madogo hayachukuliwi kuwa kukufuru. Ukimkufuru Mungu, kumhukumu Mungu au kumkashifu Mungu hata mara moja, basi hii ni dosari ya milele ambayo haiwezekani kuifuta iwe safi. Ilhali bado watu wanafikiri kukurufu kwa kawaida dhidi ya Mungu, kumtupia Mungu matusi na kumtumia Mungu. Kitu kama hicho kinawezekanaje? Watu daima wanadhani kwamba Mungu ni rehema na upendo, kwamba Mungu ni mwema, na kwamba Mungu yuko tayari kupokea mawazo mapya, jinsi alivyo tayari kupokea mawazo mapya kama bahari isivyo na mipaka. Wanadhani kwamba Hayakumbuki makosa ya mwanadamu, kwamba Yeye huyaacha yaliyopita yapite kuhusu makosa ya zamani ya mwanadamu na matendo ya awali. Lakini Yeye huacha tu yaliyopita yapite na mambo madogo, Hawezi kuruhusu mambo makubwa yapite.

Watu wanaamini katika Mungu lakini hawamwogopi. Wanapopatwa na hamaki na kukasirika, wao husema wanachotaka. Kwa hivyo wanapaswa kulipa gharama ya kile wanachosema, na hili si jambo rahisi. Wakati watu wengine wanakufuru, wanapomhukumu Mungu, wanajua mioyoni mwao wanayosema? Wote wanaosema mambo haya wanajua mioyoni mwao kile wanachosema. Mbali na baadhi ambao wamepagawa na pepo wachafu na ambao mantiki yao si ya kawaida, watu wa kawaida hujua mioyoni mwao kile wanachosema. Wakisema hawajui, basi wanasema uongo. Wanapozungumza, wanafikiri: "Aa. Wewe ni Mungu na najua kwamba Wewe ni Mungu. Ninasema kuwa hufanyi vizuri, hivyo Utanifanya nini? Utafanya nini wakati nimekwisha maliza kuzungumza? Wanafanya hivi kwa makusudi, ili kuwavuruga wengine, kuwavuta wengine katika upande wao, kuwafanya wengine waseme mambo kama hayo, kuwafanya wengine kufanya mambo sawa. Wanajua kwamba wanachosema ni uasi kwa Mungu, kwamba ni kuenda kinyume na Mungu, kumkufuru Mungu. Baada ya kutafakari juu yake wanafikiri kwamba walichofanya si sawa: "Nilikuwa nikifikiria nini, nikisema mambo hayo? Ulikuwa ni wakati wa harara na mimi najuta kabisa! "Majuto yao yanathibitisha kwamba wanajua hasa walichokuwa wakifanya wakati huo; sio kwamba hawakujua. Ikiwa unafikiri kwamba walikuwa hawajui na walichanganyikiwa kwa muda mfupi, kwamba hawakuwa wameelewa vizuri, basi hili si sahihi kabisa. Watu huenda hawakuwa wameelewa vizuri, lakini ikiwa unamwamini Mungu basi lazima uwe na kiwango cha chini cha maarifa ya kawaida. Kumwamini Mungu unapaswa kumwogopa Mungu na kumheshimu. Huwezi kukufuru dhidi ya Mungu, au kumhukumu au kumkashifu vyovyote upendavyo. Unajua nini maana ya "kuhukumu," "kukufuru" na "kukashifu"? Unaposema kitu, hujui kama wewe unamhukumu Mungu au la? Ili kusababisha shauku kati ya wale walio chini, watu wengine hutumia mifano, wakisema: "Mungu ni mgonjwa sasa ilhali bado nyinyi bado hamuichukulii kwa uzito imani yenu!" Wanasema maneno haya, na inawezekana kwamba hawajui wanachomaanisha wenyewe, na labda malengo yao ni mazuri kwa wale walio chini. Lakini hawapaswi kutumia mfano huu au kusema maneno haya kuwatia moyo watu. Kuna mambo mengine mengi ambayo wanaweza kusema ili kuwatia moyo watu, kwa nini lazima waseme haya? Sababu ya msingi ya mtu kusema hili ni kwamba kimsingi hana moyo wa kumcha Mungu, na hamwogopi Mungu. Baada ya watu wengine kurudia maneno haya, wanahisi majuto na kusema: "Niliwezaje kusema jambo kama hilo? Sijakuwa na raha tangu nilipoyarudia maneno hayo. "Hili ndilo linalotokea wakati mtu hana moyo wa kumcha Mungu! Hatetemeki na hofu kabisa na, wanasema mambo kama haya kama wanavyopenda. Hawana heshima kuu kwa Mungu, hawana moyo wa kumcha Mungu. Wanawezaje kutenda na kupayuka mbele za Mungu? Mungu ni mwenye hadhi. Wangalitambua jambo hili, basi wangeweza kusema mambo kama hayo? Hawana moyo wa kumcha Mungu. Ili kufikia malengo yao wenyewe na kufikia malengo yao binafsi, wanasema kama wanavyopenda, wakisema hili kuhusu Mungu, wakisema lile kumhusu Mungu, na hata kumkufuru Mungu na kumhukumu. Kama vile watu wengine ambao sasa wanaeneza injili na ambao, ili kuwafanya watu kujiunga, wanafuata mkondo na kusema: "Mwanga wa Mashariki ni dhehebu bovu. "Haijalishi nia ya kusema maneno haya ni nini, si sawa kusema mambo kama haya. Je, hakuna kitu kingine unachoweza kusema badala yake? Kwa nini lazima useme hili? Je, huku sio kukufuru dhidi ya Mungu? Maneno haya yanatoka kinywani mwako mwenyewe, hivyo ni wewe ndiye uliyekufuru. Kwa nini unatumia maneno haya? Unayasema ili uweze kuwafanya watu wajiunge na kukamilisha kazi yako. Unalipa gharama ya maneno haya ili kuwapata watu, lakini si wewe unakufuru dhidi ya Mungu? Bila kujali kama unayasema kwa makusudi au sio kwa makusudi, maneno haya ni ya kukufuru na huna moyo wa kumcha Mungu hata kidogo. Unatumia maneno ambayo yanakufuru dhidi ya Mungu ili kuwapata watu—wewe huna heshima hata kidogo! Je! Mungu yuko kwa ajili ya wewe kumchezea kama unavyopenda? Kuhukumu kama unavyopenda? Kuzungumza bila kujali kama unavyopenda? Hili ni jambo la kutisha. Utaangamizwa ukisema chochote kibaya; ni suala la kufa kupona! Watu wengine wanafikiri: "Kwa kuwa imekwisha, alisema mambo haya, kama nilivyosema mimi, kwa hivyo sisi si sote tumemalizika? Watu wangapi wataachwa? "Ni wangapi watasalia? Inakubalika kusiwe na mtu yeyote aliyeachwa. Nani aliyewafanya nyote mseme mambo haya? Wote wanaosema mambo haya wamemalizika. Je, unadhani kuwa mwanadamu ana thamani yoyote? Kwa hakika huna ufahamu wowote kuhusu kile ulicho, na kwa kweli unafikiri kwamba una thamani fulani! "Ikiwa sote tumemalizika, basi si Mungu amefanya kazi bure? " Ikiwa ilifanyika bure basi ilifanyika bure; si jambo kubwa. Unafikiri kuwa una thamani, kwamba Mungu hawezi kumwacha mwanadamu, na kwamba hatua nzima ya mpango Wake wa usimamizi ni kuwasimamia watu, hivyo Mungu Akimwacha mwanadamu basi usimamizi Wake hautakuwako tena. Umekosea kufikiria hivi! Mungu anaendelea na mpango Wake bila kujali ni nani Anayemwacha nyuma. Watu hufukiri sana kujihusu na hawana moyo wa kumcha Mungu. Hawana uchaji hata kidogo mbele za Mungu, wala hawana mtazamo wowote wa tabia nzuri. Kwa kuwa mwanadamu anaishi chini ya umiliki wa Shetani na wao ni wa miliki hiyo, wanaweza kumhukumu Mungu na kumkufuru Mungu wakati wowote na mahali popote. Hili ni jambo la kutisha sana. Kama wengine wenu wanaothubutu kuwa na wazo la aina hiyo: "Nataka kuchapisha kitabu pia. Nitakitoa na kitarithiswa kutoka kizazi hadi kizazi. "Je! Somo lililopewa kwako na mfano wa Paulo halikuwa la maana sana vya kutosha? Bado unataka kuandika kitabu na bado unataka kufanya "tawasifu ya mtu mashuhuri. "Bado unataka kuunganisha kitabu cha "muhtasari wa ukweli. "Hakika wewe ni mjinga. Je! Hujapitia shida za kutosha kwa miaka hii ya kumwamini Mungu? Je! Bado hulielewi jambo hili kabisa? Mwanadamu anaelewa nini?

Mafundisho machache ambayo unaelewa hayawezi hata kukukimu wewe mwenyewe na bado unataka kuwakimu wengine. Hujui kimo chako mwenyewe. Tazama, watu wote ni tofauti. Ingawa watu wengine hasa hawaelewi kila kitu kilichopangwa na aliye juu, bado wao hutii na kusema: "Kila Afanyacho Mungu ni sahihi. Ingawa hatuwezi kulielewa vizuri, bado tutaendelea kumtii. Hakika hatupaswi kumhukumu Mungu.

Tunapaswa kusikiliza hata kama haionekani kuwa sawa, kwa sababu sisi ni watu na hakuna kosa katika kile ambacho Mungu hufanya. Kuna maana katika hayo yote, lakini sisi wapumbavu tunaweza kuona maana ipi? Tutamfuata tu Mungu na kutii mipango ya Mungu, mpaka ile siku tutakapoelewa. Hata kama bado hatutaelewa siku hiyo, bado tutatii kwa hiari. Sisi ni wanadamu, na hivyo tunapaswa kumtii Mungu. Iko kama inavyopasa kuwa. "Lakini watu wengine ni tofauti. Wanapoona kile ambacho aliye juu hufanya, wao kwanza hufikiri, wakisema: "Umesema hili, Mungu, na Umedai jambo hili. Nadhani jambo la kwanza ni sawa, lakini sidhani jambo la pili linafaa sana. Mimi nitalibadilisha kwa ajili Yako. "Je! Maneno haya yanaonyesha moyo unaomcha Mungu? Au wana dhana kuhusu mambo ambayo Mungu hufanya, na hivyo hawayafanyi katika viwango vya chini. Badala yake, wanazungumza kwa kawaida na kuzungusha dhana zao kama wanavyopenda kati ya wale walio chini, wakiwajulisha walio chini kwamba Mungu hakubaliani na dhana za mwanadamu. Kisha kila mtu atakuwa na dhana kumhusu Mungu. Kwanza, hawawezi kuutoa ukweli; pili, hueneza dhana; tatu, wanamjulisha kila mtu ili wote wataipinga njia ya Mungu ya kufanya mambo, watamlazimisha Mungu afanye mambo kwa njia tofauti na hatimaye kumfanya Mungu akubali kushindwa. Watu wengine wanaweza kufanya mambo kama haya ili kuwafanya watu wawe na dhana, kumfanya Mungu akubali kushindwa, kumlazimisha Mungu afanye mambo kwa namna tofauti na kumfanya Awaridhishe watu. Ikiwa watu hawa baadaye watahisi majuto na kulia machozi, je, hili linaweza kuhesabiwa kama wao kuwa na moyo wa kumcha Mungu? Baadhi yenu ni wenye shauku nyingi kupita kiasi na hamjui kuhusu jinsi ya kumhudumia Mungu, lakini unaweza kuhurumiwa kutokana na hili. Ukilifanya tena, basi itachukuliwa kuwa umelifanya kwa kujua. Kisha dhambi zako zitakuwa kubwa na nzito, na kitakuwa kitu cha kutisha. Mkilichukua suala hili kwa urahisi sana, kwamba si kitu tu, basi itakuja siku ambayo utamkosea Mungu. Nimewaona watu fulani kama hawa. Si lazima kuwafukuza, wala si lazima kuwaondoa, au kulitangaza. Kwa kweli, mwisho ambao unawasubiri watu hawa tayari umewekwa. Katika imani yao kwa Mungu, mwanadamu lazima awe angalau na moyo wa kumcha Mungu. Je! Unaelewa nini maana ya "uchaji"? Lazima umwogope Mungu, kila kitu lazima kifanyike kwa busara na lazima ujipe uhuru wa kuwa na matendo tofauti. Usifanye tu chochote unachotaka kufanya. Kama vile tu viongozi wengine walivyoondolewa, watu wengine walisema: "Ni vigumu kuzungumza kuhusu hili. Hatujui kile walichofanya hasa. Hata kama tungejua kile walichofanya, bado hangeweza kuelewa kabisa namna walivyofanya. Yote Afanyayo Mungu ni sahihi. Siku itakuja ambapo Mungu atatufunulia yote na Atatuwezesha kuyaelewa mapenzi Yake. "Huenda hujaelewa kwa nini Mungu anafanya jambo, lakini unaweza kuendelea kumtii. Basi wewe ni mtu ambaye ni mchaji kwa ulinganifu na anaweza kuchukuliwa kuwa mwenye moyo wa kumcha Mungu. Ikiwa huelewi na hata unaenda kinyume na Mungu, basi utazaa tu matunda yaliyooza. Wakati wowote ambapo kiongozi anaondolewa, daima kutakuwa na wafuasi wachache wasiokubali kushindwa katika viwango vya chini ambao watawafuata, ambao watawatetea kwa haki kwa ajili yao. Kwa sababu ya hili, wao wanamhukumu Mungu hadharani, na wanasema kwamba Mungu si mwenye haki na kumruhusu Roho Mtakatifu kufunua kila kitu. Hata kama watu hawa wanafikia matokeo bora zaidi katika kueneza injili, yote ni bure.

Usaliti mmoja unaamua majaliwa yako milele. Lazima uchukulie namna ya jambo hili kwa uzito. Usilichukulie bila uzito jambo hili. Inaweza kusemwa kuwa mmemkataa Mungu wakati fulani uliopita, lakini asili ya upinzani wenu ilikuwa tofauti. Asili ya suala hili ni zito. Watu wengine hukusanya vitabu na kuwapatia wale walio chini. Kwa nini hawaruhusiwi kuchapisha vitabu hivi au kuvitoa? Hamwelewi. Mngalielewa basi hamngalifanya kitu kama hicho. Kwa nini? Ingawa watu wanaweza kuuelewa ukweli, maneno mengine hayawezekani tu kuyaelezea kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Yanaweza tu kushirikiwa kwa mdomo, yakitatua matatizo kwa njia hii wakati yanapotokea. Hayawezi kurekodiwa katika andiko moja au mawili. Chukua uzoefu wa Petro—je! Unapatikana katika barua za Petro? Ikiwa watu wanaonyesha tabia nzuri mbele ya neno la Mungu, basi hawatafanya mambo kwa ari au mambo ambayo wanafikiri ni mema. Ikiwa unatambua udogo, umasikini na kusikitisha kwa mwanadamu, basi hutathubutu kufanya mambo jinsi unavyotaka—kuandika vitabu au kuandika tawasifu. Wote ambao daima wanataka kuandika vitabu au tawasifu, ambao daima wanataka kufanya kitu kwa jina la kutoa mchango ili kujiimarisha, ni watu wote ambao hujiharibia kwa kutaka kufanya kupita kiasi.

Iliyotangulia: Sura ya 23. Jinsi ya kuelewa Umoja wa Mwili na Roho

Inayofuata: Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki