3. Tofauti kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya Neema na katika Enzi ya Ufalme

Maneno Husika ya Mungu:

Wakati ambapo, katika Enzi ya Neema, Mungu alirudi kwa mbingu ya tatu, kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu wote ilikuwa kwa kweli tayari imeendelea katika tendo lake la kumaliza. Vyote vilivyobaki duniani vilikuwa msalaba ambao Yesu aliubeba, sanda ya kitani ambayo Yesu alifungiwa ndani, na taji ya miiba na joho la rangi nyekundu ambavyo Yesu alivaa (hivi vilikuwa vitu ambavyo Wayahudi walitumia kumdhihaki Yeye). Yaani, baada ya kazi ya kusulubiwa kwa Yesu isababishe mhemko mkubwa, mambo yalitulia tena. Tangu wakati huo na kuendelea, wanafunzi wa Yesu wakaanza kuendeleza kazi Yake, wakiyachunga na kunyunyizia katika makanisa kila mahali. Maudhui ya kazi yao yalikuwa haya: kuwafanya watu wote watubu, waungame dhambi zao, na wabatizwe; mitume wote wakieneza hadithi ya ndani ya kusulubiwa kwa Yesu na kile kilifanyika kwa kweli, kila mtu asiweze kujizuia kuanguka chini mbele za Yesu kuungama dhambi zake, na zaidi ya hayo mitume wakieneza kila mahali maneno yaliyonenwa na Yesu na sheria na amri Alizozianzisha. Kuanzia wakati huo ujenzi wa makanisa ulianza katika Enzi ya Neema.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika mikutano maalum ya zamani au mikutano mikuu iliyokuwa katika sehemu mbalimbali, ni kipengele kimoja tu cha vitendo kilichozungumziwa. Vitendo kama hivyo ni vile vilivyotiwa katika vitendo katika Enzi ya Neema na hapakuwa na mfanano wowote na ufahamu wa Mungu kwani maono ya Enzi ya Neema yalikuwa tu maono ya kusulubiwa kwa Yesu, na hapakuwa na maono ya juu zaidi. Mwanadamu hakuhitajika kujua zaidi ya kazi Yake ya ukombozi wa mwanadamu kupitia kusulubiwa, na kwa hivyo katika Enzi ya Neema hapakuwa na maono mengine ya kufahamiwa na mwanadamu. Kwa njia hii, mwanadamu alikuwa na ufahamu mdogo sana wa Mungu na mbali na upendo na huruma za Yesu, kulikuwa na vitu vichache tu vya mwanadamu kuweka katika vitendo, vitu ambavyo vilikuwa tofauti na hali ya leo. Zamani, haikujalisha mkutano wake ulichukua umbo lipi, mwanadamu hakuwa na uwezo wa kuzungumzia ufahamu wa vitendo wa kazi ya Mungu, sembuse kuwepo na yeyote aliyeweza kusema kwa dhahiri njia iliyokuwa sawa ya utendaji kwa mwanadamu kuiingilia. Mwanadamu aliongeza tu mambo kidogo katika msingi wa stahamala na uvumilivu; hapakuwa na mabadiliko yoyote katika kiini cha vitendo vyake kwani katika enzi hiyo Mungu hakufanya kazi yoyote mpya na matakwa ya pekee Aliyomwekea mwanadamu yalikuwa stahamala na uvumilivu, au kuubeba msalaba. Mbali na vitendo kama hivyo, hapakuwa na maono ya juu zaidi kuliko yale ya kusulubishwa kwa Yesu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kuanzia sasa kuendela, mazungumzo ya maneno ya Mungu yanapaswa kuwa kanuni ambayo kwayo unazungumza. Kwa kawaida, mnapojumuika pamoja, mnapaswa kushiriki katika ushirika kuhusu maneno ya Mungu, mkiyachukua maneno ya Mungu kama maudhui ya mwingiliano wenu, mkiongea juu ya yale mnayojua kuhusu maneno haya, jinsi mnavyoyaweka katika vitendo, na jinsi Roho Mtakatifu afanyavyo kazi. Alimradi unashiriki maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Kufanikisha ulimwengu wa maneno ya Mungu kunahitaji ushirikiano wa mwanadamu. Usipoingia katika hili, Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi; ukiufunga mdomo wako na usizungumze kuhusu maneno Yake, Hatakuwa na njia ya kukuangazia. Wakati wowote ambapo huna shughuli nyingine, zungumza juu ya maneno ya Mungu, na usijishughulishe na mazungumzo yasiyo na maana! Acha maisha yako yajazwe na maneno ya Mungu—ni hapo tu ndipo utakapokuwa mwumini mwenye kumcha Mungu. Haijalishi ikiwa ushirika wako ni wa juu juu. Bila ujuu juu hakuwezi kuwepo kina kirefu. Lazima kuwe na mchakato. Kupitia mafunzo yako, utafahamu kuangaziwa kwako na Roho Mtakatifu, na jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu kwa matokeo yanayotarajiwa. Baada ya muda wa uchunguzi, utaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ni ukiamua kushirikiana tu ndipo utaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

“Kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu” kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako. Na baada ya hayo, wengine wanatambua mambo haya, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli. Hakumaanishi tu kuwa na umaizi katika maneno ya Mungu ama sehemu ya wimbo wa kidini, na kuwasiliana upendavyo na kisha kutofanya mengine zaidi, na kutosema chochote kuhusu maisha yako halisi. Kila mtu huongea kuhusu maarifa ya mafundisho na ya nadharia, na hawasemi chochote kuhusu maarifa yaliyotoka kwa uzoefu halisi. Nyote mnaepuka kuzungumza kuhusu vitu kama hivyo, kuhusu maisha yenu binafsi, kuhusu maisha yenu katika kanisa pamoja na ndugu zenu, na kuhusu dunia yenu ya ndani. Kwa kufanya hili, kunawezaje kuwa na kuwasiliana kwa kweli kati ya watu? Kunawezaje kuwa na imani ya kweli? Hakuwezi kuwa hata kidogo! Iwapo mke hazungumzi kamwe kuhusu maneno ndani ya moyo wake kwa mume wake, wao ni wasiri? Je, wanaambiana siri? Tuseme kwamba siku nzima, “Nakupenda!” Wanasema tu haya, lakini hajawahi kuweka wazi wanayoyafikiri katika mioyo yao, kile wanachotaka kutoka kwa kila mmoja, ama ni shida zipi walizo nazo. Hawajawahi kuzungumza wao kwa wao kuhusu mambo kama hayo, wala hajawahi kuambiana siri—na iwapo hao wawili hawajawahi kuambiana siri, basi, je, wao ni wachumba wanaopendana? Iwapo hawana lolote isipokuwa maneno yenye kuvutia kwa mwingine wakiwa pamoja, kweli wao ni mke na mume? Bila shaka sio! Ikiwa ndugu wanaweza kuambiana siri, kusaidiana, na kuruzukiana wakiwa pamoja, basi kila mtu lazima azungumze kuhusu uzoefu wake binafsi wa kweli. Usipozungumza kuhusu uzoefu wako binafsi wa ukweli, na unazungumza tu maneno yenye kuvutia, na maneno ambayo ni ya mafundisho na ya juu juu, basi wewe si mtu mwaminifu, na huna uwezo wa kuwa mwaminifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Mnapokuwa na ushuhuda wa, mnapaswa kuzungumza hasa kuhusu jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwaadibu watu, ni majaribio yapi anayoyatumia kuwasafisha wanadamu na kubadilisha tabia zao. Mnapaswa pia kuzungumza kuhusu kiwango cha upotovu ambacho kimefichuliwa katika uzoefu wenu, kiasi ambacho mmestahimili na jinsi ambavyo hatimaye mlishindwa na Mungu; kiasi cha maarifa ya kweli ya kazi ya Mungu mlicho nacho, na jinsi mnavyopaswa kumshuhudia Mungu na kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake. Mnapaswa kuweka umuhimu katika lugha ya aina hii, huku mkiisema kwa njia rahisi. Msizungumze juu ya nadharia tupu. Zungumzeni mambo halisi zaidi, zungumzeni kwa dhati. Hivi ndivyo jinsi mnavyopaswa kupitia. Msijiandae kwa nadharia zinazoonekana kuu, zilizo tupu katika juhudi la kujionyesha; kufanya hivyo kunawafanya muonekane wenye majivuno sana na msio na maana. Mnapaswa kuzungumza zaidi kuhusu mambo ya kweli na halisi kutoka kwa uzoefu wenu ambayo ni ya kweli na ya dhati; hili ndilo la manufaa zaidi kwa wengine, na ndilo linalowafaa zaidi kuona. Ninyi mlikuwa watu waliompinga Mungu zaidi na ambao waliegemea kumtii Yeye kwa kiasi kidogo zaidi, lakini sasa mmeshindwa—msisahau hilo kamwe. Mnapaswa kutenga tafakari na fikira nyingi kwa masuala haya kwa bidii. Baada ya kugundua hili, mtajua jinsi ya kushuhudia; vinginevyo mnaweza kufanya vitendo vya aibu na vya kipumbavu.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 2. Tofauti kati ya ukweli ulioonyeshwa na Bwana Yesu na wa Mwenyezi Mungu

Inayofuata: 1. Maana ya kuokolewa na kufikia wokovu kamili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Tofauti kati ya kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho

Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki