3. Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haibadiliki kamwe
Maneno Husika ya Mungu:
Kila wakati ambao Mungu Atawasili hapa duniani, Yeye Atabadilisha jina lake, jinsia yake, mfano wake, na kazi yake; Yeye harudii kazi yake, na Yeye daima yu mpya na kamwe si wa zamani. Wakati Alikuja hapo awali, Aliitwa Yesu; Je, anaweza bado kuitwa Yesu anapokuja tena wakati huu? Alipokuja hapo awali, Alikuwa wa kiume, Ataweza kuwa wa kiume tena wakati huu? Kazi Yake Alipokuja wakati wa Enzi ya Neema ilikuwa ya kusulubishwa msalabani; Atakapokuja tena, je, bado Atawakomboa wanadamu kutoka kwenye dhambi? Je, bado Atasulubishwa msalabani? Je, huko hakutakuwa kurudia kazi Yake? Je, hukujua kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani? Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia. Hapo mwanzo, tabia ya Mungu ilikuwa siri kwa mwanadamu, na kamwe Yeye hadharani hakumfichulia mwanadamu tabia yake, na mwanadamu hakuwa na ufahamu kuhusu Yeye, na hivyo hatua kwa hatua Alitumia kazi Yake kumfichulia mwanadamu tabia Yake, lakini hii haina maana kuwa tabia Yake inabadilika katika kila enzi. Sio kweli kuwa tabia ya Mungu kila wakati inabadilika kwa ajili mapenzi Yake daima hubadilika. Bali, kwa kuwa enzi za kazi Yake ni tofauti, asili ya tabia Yake kwa ujumla hufichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, ili mwanadamu aweze kumjua Yeye. Lakini hii si kwa njia yoyote ushahidi kuwa Mungu hapo awali hakuwa na tabia fulani na tabia Yake imebadilika hatua kwa hatua kwenye enzi zinazopita—ufahamu kama huo ni wenye kosa. Mungu humfichulia mwanadamu tabia yake fulani ya asili, kile Alicho, kwa mujibu wa enzi zinazopita. Kazi ya enzi moja haiwezi kueleza tabia nzima ya Mungu. Na kwa hivyo, maneno haya “Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani” yanarejelea kazi yake, na maneno haya “Mungu habadiliki” kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima husonga kwenda mbele.
Kimetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi nyingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hakuna jambo lolote hapa lisilo la kawaida; ni kwamba tu watu ni punguani sana. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana. Unathubutu kudai kwamba Yesu milele ni jina la Mungu, kwamba Mungu milele na daima atajulikana kwa jina Yesu, na kwamba haya hayatabadilika? Unathubutu kudai kwa uhakika ni jina la Yesu lililohitimisha Enzi ya Sheria na pia kuhitimisha enzi ya mwisho? Nani anaweza kusema kwamba neema ya Yesu inaweza kuhitimisha enzi?
Kimetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu siku zote huwa Mungu, na kamwe Yeye hatakuwa Shetani; Shetani daima ni Shetani, na yeye hawezi kuwa Mungu. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, haki ya Mungu, na adhama ya Mungu kamwe hayatabadilika. Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na katika kila enzi Yeye huwaruhusu viumbe Wake kuona mapenzi Yake mapya na tabia Yake mpya. Ikiwa watu hawaoni dhihirisho la tabia mpya ya Mungu katika enzi mpya, wao si watamsulubisha msalabani milele? Na kwa kufanya hivyo, si watakuwa wamebaini Mungu?
Kimetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili