Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

274 Mungu Anatupenda Sana

1

Mwenyezi Mungu, nakuamini. Nikikumbuka jinsi nilivyozurura ulimwenguni,

Nahisi kwa undani unyonge na kutojali kwa watu. Nilihangaika na kupapasa gizani.

Mateso ya maisha hayana mwisho; nikiosha uso wangu kwa machozi, niliumia kwa miaka yote.

Bila tumaini, ningeweza tu kuishi bila msaada, kwa kukata tamaa.

Mwenyezi Mungu, Unatupenda sana. Maneno Yako yananiamsha.

Mwishowe narudi Kwako na kutupilia mbali maisha yangu ya uchungu.

Maneno Yako yananiangaza, naona maisha yanayong’aa.

Nafurahia maneno Yako na kuishi katika uwepo Wako, moyo Wangu umejaa amani na furaha.

2

Mwenyezi Mungu, nakuamini. Asili yangu yafunuliwa na maneno Yako.

Hukumu ya maneno Yako hunifanya nione jinsi nilivyopotoka sana.

Mwenye kiburi, mdanganyifu, mwovu na mwenye tamaa, sifanani na mwanadamu hata kidogo.

Najijua na naanguka chini mbele Yako kukubali hukumu na utakaso Wako.

Mwenyezi Mungu, Unatupenda sana. Hukumu Yako inaniokoa.

Unaninipa ukweli na uzima, na kunifundisha jinsi ya kuwa binadamu.

Sasa nimebadilika kidogo, nitakosaje kukushukuru na kukusifu?

Nafurahia maneno Yako na kuishi katika uwepo Wako, moyo Wangu umejaa amani na furaha.

3

Mwenyezi Mungu, nakuamini. Wanipenda kweli.

Moyo wangu umejaa mailioni ya maneno ya shukrani, lakini sijui nianzie wapi.

Kufurahia upendo Wako lakini siwezi kukushuhudia, moyo wangu unakua na wasiwasi.

Bado mimi ni hobelahobela na mwongo katika wajibu wangu, siwezi kuyaridhisha mapenzi Yako.

Mwenyezi Mungu, Unatupenda sana. Hukumu Yako ni baraka.

Hukumu Yako yanitakasa na naona utakatifu Wako na kupendeza Kwako.

Sasa nimepata wokovu Wako na naishi katika nuru, moyo wangu unahisi utamu usio na kifani.

Nafurahia maneno Yako na kuishi katika uwepo Wako, moyo Wangu umejaa amani na furaha.

Tutakutii katika kila jambo, tuishi kulingana na maneno Yako na tukupende milele.

Iliyotangulia:Ee Mungu, Nakukosa

Inayofuata:Upendo wa Mungu Umeuyeyusha Moyo Wangu

Maudhui Yanayohusiana

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…