2. Dunia ya kidini inaamini kwamba maandiko yote yametolewa na msukumo wa Mungu na yote ni maneno Yake; kwa nini mtazamo huu si sahihi
Maneno Husika ya Mungu:
Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufahamu wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni ufahamu sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa yaliyotokana na uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umeagizwa na Mungu binafsi: Unabii wa mifano ya Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu; watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa moja.
Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, idadi kubwa ya manabii iliinuliwa na Yehova, walizungumza unabii kwa niaba Yake, walitoa maelekezo kwa makabila mbalimbali na mataifa, na wakatoa unabii juu ya kazi ambayo Yehova angefanya. Watu hawa ambao wameinuliwa wote walipewa na Yehova Roho ya unabii: Waliweza kutazama njozi kutoka kwa Yehova, na kusikia sauti Yake, na hivyo walivuviwa Naye na wakaandika unabii. Kazi waliyoifanya ilikuwa udhihirisho wa sauti ya Yehova, udhihirisho wa unabii wa Yehova, na kazi ya Yehova wakati huo ilikuwa ni kuwaongoza watu kwa njia ya Roho Mtakatifu; Hakufanyika mwili, na watu hawakuona uso Wake. Hivyo, aliwainua manabii wengi kufanya kazi Yake, na akawapatia mashauri ambayo waliyapelekea katika kila kabila na ukoo wa Israeli. Kazi yao ilikuwa ni kusema unabii, na baadhi yao waliandika maelekezo ya Yehova kwa ajili yao ili kuwaonesha wengine. Yehova aliwainua watu hawa kuzungumza unabii, kutoa unabii wa kazi ya wakati ujao au kazi ambayo ilikuwa bado haijafanyika wakati huo, ili kwamba watu wangeweza kutazama maajabu na hekima ya Yehova. Vitabu hivi vya unabii vilikuwa tofauti kabisa na vitabu vingine vya Biblia; yalikuwa ni maneno yaliyozungumzwa au kuandikwa na wale waliopewa Roho ya unabii—na wale ambao walipata njozi au sauti kutoka kwa Yehova. Kuacha vitabu vya unabii, kila kitu kingine katika Agano la Kale ni rekodi zilizochukuliwa na watu baada ya Yehova kukamilisha kazi Yake. Vitabu hivi haviwezi kusimama badala ya unabii uliozungumzwa na manabii walioinuliwa na Yehova, kama ambavyo Mwanzo na Kutoka haviwezi kulinganishwa na Kitabu cha Isaya na Kitabu cha Danieli. Unabii ulikuwa unazungumzwa kabla ya kazi haijafanyika; wakati huo, vitabu vingine viliandikwa baada ya kuwa kazi imemalizika, kazi ambayo watu walikuwa wanaiweza. Manabii wa wakati huo walivuviwa na Yehova na kuzungumza unabii, walizungumza maneno mengi, na walitoa unabii wa mambo ya Enzi ya Neema, na vilevile uharibifu wa dunia katika siku za mwisho—kazi ambayo Yehova alipanga kufanya. Vitabu vilivyosalia vyote vinarekodi kazi iliyofanywa na Yehova katika Israeli. Hivyo, unaposoma Biblia, unakuwa unasoma kile ambacho Yehova alifanya katika Israeli; Biblia ya Agano la Kale kimsingi inarekodi kazi ya Mungu ya kuwaongoza Israeli, kumtumia Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri, aliyewaondoa katika shida za Farao, na kuwachukua na kuwapeleka jangwani, ambapo baada ya hapo wakaingia Kaanani na kila kitu baada ya hapa ilikuwa ni kuanza maisha yao Kaanani. Yote, isipokuwa hii ni rekodi za kazi ya Yehova katika Israeli yote. Kila kitu kilichorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, ni kazi Aliyoifanya Yehova katika nchi ambapo Aliwaumba Adamu na Hawa. Kuanzia wakati ambapo Mungu alianza rasmi kuwaongoza watu duniani baada ya Nuhu, yote ambayo yamerekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Israeli. Na kwa nini hakuna kazi yoyote iliyorekodiwa ambayo ni nje ya Israeli? Kwa sababu nchi ya Israeli ni chimbuko la binadamu. Mwanzoni hakukuwa na nchi yoyote tofauti na Israeli, na Yehova hakufanya kazi katika sehemu nyingine yoyote. Kwa namna hii, kile kilichorekodiwa katika Agano la kale la Biblia ni kazi ya Mungu katika Israeli pekee wakati huo. Maneno yaliyozungumzwa na manabii, na Isaya, Danieli, Yeremia na Ezekieli … maneno yao yanatabiri kazi Yake nyingine duniani, yanatabiri kazi ya Yehova Mungu Mwenyewe. Yote haya yalitoka kwa Mungu, ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, na tofauti na vitabu hivi vya manabii, mambo mengine yote ni rekodi ya uzoefu wa watu juu ya kazi ya Yehova wakati huo.
Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Huu ni ufahamu wenye makosa wa mwanadamu, na hauafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, sembuse kuona maono ambayo Yohana aliona. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. Na hivyo, nyaraka za Paulo za Agano Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Ni maneno tu ya kushawishi, faraja, na kutia moyo ambayo aliyaandika kwa ajili ya makanisa wakati wa kazi yake. Na hivyo pia, ni rekodi zaidi ya kazi na muda ya Paulo. Ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada wote katika Bwana, na zilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya kaka na dada wa makani yote ya wakati huo kufuata ushauri wake na kudumu siku zote katika njia zote za Bwana Yesu. Kwa namna yoyote ile Paulo hakusema kuwa, iwe ni kwa makanisa ya wakati huo au makanisa ya wakati ujao, yote yanapaswa kula na kunywa vitu alivyoandika, wala hakusema kwamba maneno yake yote yalitoka kwa Mungu. Kulingana na mazingira ya kanisa wakati huo, aliwasiliana tu na kaka na dada, na aliwashawishi, na akawaimarisha imani kwao; na aliwahubiria na kuwakumbusha watu na kuwashawishi. Maneno yake yalijikita katika mzigo wake mwenyewe, na aliwasaidia watu kupitia maneno haya. Alifanya kazi ya mitume wa kanisa wa wakati huo, alikuwa mfanyakazi ambaye alitumiwa na Bwana Yesu, na kwa hivyo lazima achukue jukumu kwa ajili ya makanisa, na lazima afanye kazi ya makanisa, alipaswa kujifunza kuhusu hali za ndugu—na kwa sababu hii, aliandika nyaraka kwa kaka na dada wote katika Bwana. Yote aliyoyasema ambayo yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hayakuweza kumwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na makufuru makubwa sana kwa watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa! Hiyo ni kweli kabisa tunapokuja katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa ajili ya makanisa, kwani nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada kulingana na mazingira na hali ya kila kanisa kwa wakati huo, na yalikuwa ni kwa ajili ya kuwashawishi kaka na dada katika Bwana, ili waweze kupokea neema ya Bwana Yesu. Nyaraka zake zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaamsha kaka na dada wa wakati huo. Inaweza kusemwa kuwa huu ulikuwa ni mzigo wake mwenyewe, na pia ulikuwa ni mzigo aliopewa na Roho Mtakatifu; hata hivyo, alikuwa ni mtume aliyeyaongoza makanisa ya wakati huo, ambaye aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa na kuwashawishi, huo ulikuwa wajibu wake. Utambulisho wake ulikuwa tu ni mtume anayefanya kazi, na alikuwa ni mtume tu aliyetumwa na Mungu; hakuwa mtabiri, wala mtoa unabii. Kwake, kazi yake mwenyewe na maisha ya kaka na dada yalikuwa na umuhimu mkubwa sana. Hivyo, asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu. Maneno yake hayakuwa maneno ya Roho Mtakatifu, wala yasingesemwa kuwa ni maneno ya Mungu, maana Paulo hakuwa chochote zaidi ya kiumbe wa Mungu, na hakika hakuwa Mungu aliyepata mwili. Utambulisho wake haukuwa sawa na ule wa Yesu. Maneno ya Yesu yalikuwa ni maneno ya Roho Mtakatifu, yalikuwa ni maneno ya Mungu, maana utambulisho wake ulikuwa ule wa Kristo—Mwana wa Mungu. Inawezekanaje Awe sawa na Paulo? Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na hivyo, unasemaje—kwamba nyaraka alizoandika kwa ajili ya makanisa haziwezi kutiwa doa na mawazo yake mwenyewe? Inawezekanaje zisitiwe doa na mawazo ya kibinadamu? Aliandika nyaraka kwa makanisa kulingana na uzoefu wake binafsi, na maarifa yake binafsi. Kwa mfano, Paulo aliandika waraka kwa kanisa la Wagalatia ambao ulikuwa na maoni fulani, na Petro aliandika waraka mwingine, ambao ulikuwa na mtazamo mwingine. Ni upi kati ya hizo ulitoka kwa Roho Mtakatifu? Hakuna anayeweza kutoa jibu, hakika. Hivyo inaweza kusemwa tu kwamba wote wanawiwa na mzigo kwa makanisa, lakini barua zao zinawakilisha kimo chao, zinawakilisha vile wanavyowapatia na kuwasaidia kaka na dada, na vile wanavyowiwa na makanisa, na zinawakilisha tu kazi ya binadamu; hayakuwa ya Roho Mtakatifu kabisa. Ikiwa unasema kwamba nyaraka zake ni maneno ya Roho Mtakatifu, basi wewe ni mpumbavu, na unafanya makufuru! Nyaraka za Paulo na nyaraka nyingine za Agano Jipya ni sawa na kumbukumbu za viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni. Zipo sawa na vitabu vya Watchman Nee au uzoefu wa Lawrence, na kadhalika. Ni vile tu vitabu vya viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni havijajumuishwa katika Agano Jipya, lakini hulka ya watu hawa ni sawa: Kulikuwa na watu ambao walitumiwa na Roho Mtakatifu wakati fulani, na hawakuweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.
Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili